Heri kwenu ninyi wote, mwaka mpya, tabia mpya yenye tija katika mageuzi

Mghaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
320
127
Nadhani watu wajuvi wa masuala ya siasa mnatambua sasa kuwa siyo mtu anayependwa bali kusimamia agenda ambayo inakidhi matakwa ya umma ndiyo msingi wa kuwa upande wa umma na umma kuwa na wewe, siyo mtu anachukiwa bali kile anachosimamia kama kinakwaza juhudi zao ni adui yao, kama huwezi kusimamia haki na kuweza kujizuia kuikwaza haki wewe ni adui namba moja wa haki. Kuna wakati waJF mnahamaki na mnakosea sana kuchanganya demokrasia na haki za msingi za watu. unaweza kuwa na demokrasia katika nchi bila kuwa na utawala wa sheria wenye kuheshimu haki za msingi za raia, na unaweza kuheshimu haki za msingi za raia na bado usiwe a democratic state. Majority dictatorship wakati mwingine ndiyo misingi ya demokrasia.

Ugomvi wa Zitto na Wajf wengi ilikuwa ni mdogo sana na pande zote zilikuwa na haki katika yale waliyoyamini. Wale waliosema Mh. Zito ni kikwazo cha nguvu ya umma kwa sababu tu walimwona anaubinafsi ingawa alikuwa anatekeleza misingi ya asili ya haki zake za msingi za kushiriki katika mchakato wa Demokrasia, naye aliwaona wenzake wanaompinga ni wakora kwani wanahubiri demokrasia bila kutenda na kwamba walikuwa hawataki kuona anaitumia haki yake ya msingi ya kuchaguliwa au kuchagua. Makundi haya yote yalikuwa ni hatari kwa ustawi wa CDM na harakati zake za kuleta mabadiliko katika nchi hii.

Demokrasia bila ukomo ni vurugu na haki bila miiko na ukomo ni hatari. Wako watu ambao tunadhani kuwa Zito mbele na akifuatiwa nyuma yake na watu kama Tuntemeke lazima CDM ipate majeraha makubwa kisiasa katika kutafuta uraisi ndani ya Chama. Hatutaki kuingia mashindano na a lame horse we will be fighting a lost war na kwa busara zake Zito ametambua hilo na namwomba afanye hima kuwarudisha kundini wakina Tuntemeke. Pia wale ambao kwa kuipenda CDM kupita kiasi waliona hatua ya Zito ilikuwa ni kusaliti Chama warejee katika kundi na wamwone kila mwanachama ni sehemu ya CDM na waheshimu haki zake.

Nadhani Dr Slaa is not a spent force tumpatie nafasi nyingine angalau mwaka huu ili akakiuze vizuri na 2015 tufike salama. Itakuwa ni mokosa kumuengue Slaa katika kinyanga'nyiro cha Uraisi kwa CDM 2015 kama si kwa masilahi ya kundi ambalo limejificha nyuma ya mwavuli wa kutekeleza haki zao za msingi wakati agenda yao kuu ni kukimaliza chama. Haki yako ya msingi inayoteketeza matakwa ya wangi ni dhambi isiyosameheka.
 
Back
Top Bottom