Heri kusema kuliko kunyamzaza 2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heri kusema kuliko kunyamzaza 2012

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanamageuko, Sep 6, 2012.

 1. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Ni matarajio yangu kuwa wengi wetu tu wazima humu JAMVINI, kwa wote wanaougua nakuuguliwa NAKUTAKIENI kupata nafuu na AFYA kwa haraka. Na KWA WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI NINI ZAIDI YA KUWAOMBEA KWA MAULANA AWAPUNGUZIE UZITO KAMA SI KUWASAMEHE WALIYOYATANGULIZA KATIKA MAISHA YAO!? Aamin.

  Narejea katika niliyotaka kusema hii leo;

  NI KATIKA KUKUMBUSHANA TU...

  NINAPOYATAZAMA YANAYOJIRI NCHINI MWETU SITOSHANGAA KUPATA MAJAWABU KUWA SIONI NINI HAKITOTUFIKISHA KUWA KAMA DRC, SOMALIA, LIBYA, IRAQ NA KWINGINEKO KAMA HUKO....

  NINASIKITIKA SANA PALE NINAPOONA WENGI WETU BADALA YA KUFIKIRI KWA KUTUMIA VICHWA VYETU TUNAFUATA MATAKWA NA FIKRA ZA MIOYO!!!

  IKIWA HATUWEZI KUJUA NINI TUNATAKA NA KIPI KINATUSTAHILI BASI VIPI TUTAWEZA KUTOFAUTISHA VIATU VINAVYOTUTOSHA NA VISIVYOTUTOSHA???

  IKIWA TUNAANDAA MIKUTANO NA HALI TUNAJUA MIKUTANO ILE KUNA WATU TUNAOWAPENDA WATAFIKWA MADHILA JE NI KWANINI TUENDELEE NA MIKUTANO ILE HALI YA KUWATUNAJUA MATOKEO YAKE??? JE NI KWELI NI MAPENZI HAYO AU NDIO WAHANGA WENYEWE???

  KWA KAWAIDA HATA JIPU HUANZA KAMA KIPELE... TUNAPASWA KUJITAZAMA NA KUJITATHMINI JE NI KWA KIASI GANI TUNAYO BUSARA YA KUPAMBANUA MAZINGIRA NA MASULUHISHO YA UTATUZI WA MASHAKA YANAYOTUZINGIRA???

  JE NANI HAJUI KWANINI WAHENGA WALISEMA "MOTO UAMBAE KICHAKA NA KICHAKA KIAMBAE MOTO???"

  JE KWANINI TUNASHINDWA KUTAZAMA VYOMBO VYA HABARI VYA NJE NA KISHA TUKAJUA KUWA WALE WANAOSEMA KWAO KUNA DEMOKRASIA NINI KINAJIRI KWAO???

  UKIITAZAMA "WALL STREET" NA HADITHI YA YANAYOJIRI PALE HAKUNA TOFAUTI NA YANAYOTOKEA HAPA KWETU... LAKINI WANAHARAKATI WAKO KIMYA KWA HILO KWA SABABU LINATENDEKA KATIKA NCHI WANAKOPATA UGALI WAO!!!

  IKIWA LEO TUNASHINDWA KUFIKIRI KITANZANIA, NA KUTATUA MATATIZO YETU KAMA SISI KWA KUTAZAMA WALIO MBALI NA SISI... SIJUI WAPI TUNAKWENDA... TUTAENDELEA KUTUMIWA NA WANASIASA AMBAO HAWAJALI MAISHA WALA UCHUMI WETU KWA SABABU YA KUTOKUJITAMBUA KWETU!!!

  IKIWA LEO HATUHAMASISHANI KUFUNGUA ALAU VITUO VYA ELIMU MITAANI KWETU BALI MADANGURO NA ZI-GROSARIZ!! VIPI TUTAZITAMBUA HAKI ZETU??? MAJUKWAANI??? Ambako wanasiasa wanatutumia kwa maslahi yao??? kwenye Mikutano ambako mtu anahamasika kama moto wa kifuu na ikishapita siku hiyo mtu akapata kibuku yake amesahau kila kitu???

  Wanajamvi tunapaswa kufikiri zaidi ya haya tunayodhani ni fikra sahihi!! Yapo mambo ya msingi ila zaidi ya yote hayo ni ELIMU na NGUVU YA UCHUMI. tutazame kizazi kinachomaliza darasa la saba na kubaki mtaani je kitakuwa wapi??? Je ukiingia madarakani halitokuwa bomu la kukulipua??? Tutazame jirani zetu... Je nini kinatokea na wana serikali ya umoja!!! sababu yake ni nini???

  Nisiwachoshe...

  TUTAFAKARI.....
   
 2. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Mkuu nimekupata kwa mbali, ila naona kuna vitu unafichaficha. lakini pamoja na yayotokea kwa wenzetu hatuwezi kufumbia macho yanayotokea hapa kwetu. Hapa kwetu ni dhahiri kabisa mambo haya fanyiki hata kwa kufuata sheria hizo tulizojiwekea baada ya kuziona zile za Mwenhezi Mungu zina "MAPUNGUFU" (KICHEKESHO). ni wazi serikali ya chama kilichopo madarakani imekiuka sheria nyingi tu, na hatuwezi kuiacha tu iendelee kufanya inavyotaka huku sisi tukilipa kodi zetu na wao wanazitumia kuishi maisha ya peponi huku sisi tukiishi maisha ya jehanamu.

  Hebu tujiulize, hivi ni kweli serikali hii imefanya jitihada za makusudi kujaribu kuboresha huduma za jamii??? tuna misitu mingi, lakini hatuna madawati mashuleni, misitu hiyohiyo ingetupatia karatasi kwa ajiri ya vitabu. Tuna mito, maziwa na bahari, je huduma ya maji inaridhisha??? kwa nini kumekuwa na tabaka la watu kujiona wao ndo wanastahili maisha ya anasa halafu wengine ni wasindikizaji tu??? Angalia wazee wa E.A walivyonyanyaswa, ili hali kuna wabunge waligoma mpaka hata kuchukua posho na bado wakalazimishwa kuzichukua, hii haikushangazi??? Binafsi huwa nasema, UNAHITAJI KUWA NA ROHO YA SHETANI KUIHURUMIA SERIKALI YA ccm HASA AWAMU ZA 2,3 NA 4.

  Polisi na wanajeshi wanaua kwa risasi hadi mifugo ya wafugaji, mifugo imekosea nini??? kama tuna utawala wa sheria, kwa nini mwenye mifugo asifikishwe mahakamani??? BADO KUNA RICHMOND, DOWANS, MEREMETA, KAGODA, EPA, RADA, MABLIONI USWISI, UFISADI KWENYE HALIMASHAURI, RUSHWA YA KIWANGO CHA JUU KILA KONA, MIKATABA MIBOVU YA MADINI, MISHAHARA DUNI YA WAFANYAKAZI HASA WAALIMU IKIWEMO KUNYIMWA STAHIKI ZAO ZINGINE na mengine mengi.

  Kama serikali ni nzuri haiwezi kuwa na matatizo mengi hivi, kama mabaya ni mengi kuliko mazuri, ni wazi hiyo serikali haifai, Serikali hii imethibiti kuwa na mabaya mengi kuliko mazuri.
   
 3. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mimi nakubaliana sana na wewe lakini je unafikiri twaweza kufanya nini ili ili kuyaepuka haya,na je huoni tukizidi kukaa kimya hali ya nchi na maisha kiujumla inazidi kudumaa.halafu kwa hali ya nchi yetu inapoelekea hata tusipotumiwa na wanasiasa itavurugika tu,kwa sababu upatikanaji duni wa chakula ndio hali pekee ya mwisho inayomaliza subira ya wananchi wa taifa lolote.kama unaona mbali machafuko nchini hayaepukiki hali ni mbaya sana labda ibadilike lakini kwa muonekano machafuko ni zaiddi kulinganisha na jambo jingine.halafu unafikiri kuandamana au kuandaa mkutano wa kisiasa ni uvunjifu wa amani,na kama unahisi ni uvunjifu wa amani katiba inasemaje kuhusu kuandamana na kufanya mikutano?na mbona vyama vingine vikifanya mikutano hakuwi na fujo.acha woga bana nchi kama imeandikwa kulipuka italipuka tu maana hata hao watawala wanataka madaraka na hawaaminiani.
   
Loading...