Hemed PhD: Sitaacha kujipodoa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
hemedi_suleiman_06-220x300.jpg


MWIGIZAJI wa filamu na msanii wa Bongo Fleva, Hemed Suleiman ‘Hemedy PhD’, amesema kwamba hataacha kutumia vipodozi kwa kuwa humuweka nadhifu na humwongezea mvuto wa mwili wake.

Hemed anayetamba na wimbo wake wa ‘Imebaki stori’, alisema vipodozi anavyotumia zaidi ni poda, lipshine na pafyum na hataacha kujiremba.

“Sitaacha kujiremba kwa sababu kujiremba siyo kwa wasichana tu hata wanaume tunatakiwa tujipake vipodozi, kama poda na lipshine zinasaidia kuongeza mvuto na mwonekano nadhifu zaidi, mimi ni staa natakiwa niishi kistaa hivyo vipodozi ni kitu cha kawaida.

“Mara nyingi vipodozi navitumia nikiwa katika kazi zangu ili nionekane tofauti nyumbani na kazini hivyo nasisitiza kwamba siwezi kuacha kupaka vipodozi kwa kuogopa maneno ya watu,” alimaliza Hemed.

Source: Hemed PhD: Sitaacha kujipodoa kwa hofu ya watu
 
Kujipodoa!! huu msamiati nahisi unawahusu sana wakina Dada,,,anyway jirembe mwana
 
Kujipodoa!! huu msamiati nahisi unawahusu sana wakina Dada,,,anyway jirembe mwana
teh teh teh
wanaume wa siku hizi nao wanajipodoa aiseeee, full kushinda saluni wanafanya ma-scrub , mara sijui kujiangalia angalia kwenye vioo, yaani full mbwembwe
 
Vijana wa Dar sijui wamekumbwa na jinamizi gani....yaani maneno haya yanatoka kwenye kinywa cha mwanamume kabisaa.....???
 
Back
Top Bottom