Mnyonge Kabisa
Senior Member
- Nov 7, 2018
- 102
- 74
Salaam wakuu.
Heshima kwenu wakubwa.
Katika hali isiyo ya kawaida watoto kutoka familia masikini ndio hasa wamekuwa waanga wakubwa na wameathirika pakubwa na suala zima la kukosa mikopo ya elimu ya juu.Nakumbuka maneno ya rafiki yangu aliwahi niambia kuwa katika mataifa ya ukanda wa tatu umasikini ni tiketi ya kupoteza haki zako za msingi.
Kuna wakati kwa macho yako umeshuudia wazi wazi wale rafiki zako toka familia bora na zenye uwezo mzuri wakipata mikopo ya elimu ya juu, tena ambao tangu elimu ya awali mpaka kidato cha sita wamesoma mashule ya gharama.Ila wewe uliyesoma kwa shida tena katika shule za serikali na ukiwa umefiwa na mzazi au wazazi na bado mkopo umekosa.Unaweza jiuliza bodi wametumia vigezo gani kutambua mwenye uhitaji na asiye na uhitaji? Lakini hili ubaki kuwa fumbo na wenye majibu ni hao hao bodi ya mikopo.
Kama leo hii tukisema majina ya waliopata mikopo yachambuliwe hadharani basi naamini fika wenye uhitaji wa dhati hawafiki ata asilimia 50.Leo hii ndoto za watoto wa masikini zinaenda kuzimwa ghafla baada hiyo batch inayofuata kuja na majina machache na yenye majina yale yale.
Ngoja niigeukie RITA ambao kisheria wamepewa mamlaka ya kutoa vyei vya kuzaliwa na vya kifo.Je mlikuwa makinibkatika kutoa vyeti hususani vya kifo na mlikuwa mnatumia ushaidi gani kutoa hivyo vyeti kuthibitisha mtajwa kweli amefariki? Isije ikawa mamluki ni wengi kuliko wenye uhitaji wa dhati.
Pia bodi ya mikopo moja kati ya makundi mliyoyapa vipaumbele ni lile kundi wa yatima ambao wamefiwa na mzazi mmoja au wote.Sasa napenda kuuliza kuwa katika kundi hili palikuwa na idadi maalumu ya kupewa mikopo? Maana mpaka batch hii ya tatu kundi hili bado lina watu wengi walio mtaani.
Mwisho.