Help, blue screen of death | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Help, blue screen of death

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Isaac Chikoma, Jun 19, 2012.

 1. Isaac Chikoma

  Isaac Chikoma JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  nina laptop ya lenovo,nataka kuinstall windows,nikiweka flash inakopy vizuri mafile,wakati wa kustart inaleta blue screen,yenye error stop: 0X0000007B.
   
 2. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  nilishawahi post kuhusiana na blue screen of death(B.S.O.D), sababu sina link yake ya ile post ngoja ni paste tena ile topic kutoka nilipoisave, hope itakusaidia in one way or another:

  Watu wengi wemakuwa wakisumbuliwa na tatizo hili bila kujua ni kiti gani hiki na ni jinsi gani ya kulitatuwa. Mtu yeyote anayetumia Microsoft Windows (iwe XP vista au seven) anaweza kukutana au pengine alishakutana na tatizo hili. Heri yao wale waliowahi kutana nalo na wakajua nini cha kufanya ila kwa wale ambao waliwahi kutana nalo na hawakujua nini wafanye au hata wale ambao hamjawahi kutana na tatizo hili (naamini ipo siku litakukumba) basi si vibaya tukapeana somo hili. Hili ni tatizo la kawaida kabisa ambalo hutokea mara nyingi pale Windows senses a software, hardware, or driver error preventing it from operating properly. Hivyo basi, almost anything from a minor glitch to a major system malfunction inaweza leta hii kitu. Mara chache sana tatizo hili linaweza kuondoka kwa kufanya simple normal restart tu ya pc yako na ukaona mambo yakawa shwaaari na Blue screen isirudi tena ILA kaa ukijua ii ni dalili mbaya ya tatizo moja kubwa baya sana linalokujia. Sasa ukitaka kujua TIBA hasa ya tatizo hili ni nini hakuna ajuaye sababu inahitai mtu afanye diagnosis ya kina kujua nini hasa tatizo la pc yako.


  BLUE SCREEN OF DEATH (BSOD) ni nini?
  Sasa basi kabla ya kujua ni jinsi gani ya kutibu embu tujue ni nini hasa hii BLUE SCREEN OF DEATH...Simple. blue screen ni error message ambayo hutokea pale tu system inapotambua tatizo lolote lile litakalosababisha kuifanya system isiweze kuendelea na kazi zake kama kawaida kwa namna yoyote ile. Hapo ndipo system inaposimamisha shughuliii zooooote kwa pamoja na kukupa ujumbe huo kuwa system imejizima ili kuokoa pc yako isiharibike kutokana na tatizo lililotokea na ujumbe huu huwa unakuja ukiwa kwenye screen ya rangi ya BLUE (ndo maana ya BLUE SCREEN) ingawa maandishi yenyewe huwa meupe..na mara nyingi Windows Xp huwa inaleta na numbered error code ambayo inaelezea tatizo hasa nini ambayo ukiitafuta maana ya code hiyo (online) unaweza jua tatizo ni nini! Kwa windows zingine sijachunguza kwa kina kama mara zote huleta numbered code kama kwenye XP...ila ni vyema ku note down hiyo error pale linapotokea tatizo hili ili ufanye uchunguzi zaidi (ingawa ni vyema ku note kila error unayoipata pale linapotokea tatizo ili upate ufumbuzi wa kina maana mtu mwingine anaona message ya error imetokea hasomi afu anaclik tu YES au NO then kuanzia hapo matatizo tu kwenye pc na ukimuuliza alifanya nini utaskia ah ah skufanya kitu!! Pumbafu!)


  JINSI YA KUTIBU BLUE SCREEN
  Sasa kama wewe ni mmoja wa wale wanaobahatika kutibu tatizo la Blue Screen kwa ku reboot tu basi pia itakubidi ukae chini na ufanye ucunguzi wa kina ili ujue tatizo hasa ni lipi la sivyo utakuja lia siku moja! Kutokana na uwezekano wa sababu nyiiingi wa tatizo hili inakuwa vigumu sana mtu kwa mara moja tu kusema tatizo la pc yako itakuwa ni hili baada ya blue screen.Ila unaweza tumia njia zifuatazo kukusaidia kutibu:
  Embu jaribu ku hisi labda tatizo litakuwa ni nini? Si unaijua pc yako vizuri? sasa ambu narrow down all possible causes za tatizo...mfano umeweka software mpya tu au hardware mpya tu ikaleta blue screen au unadhani baada ya kufanya nini ndo kumesababisha!!? Hii itakusaidia kwenye kuokoa kutumia mda mwiiingi kuanza kutafuta tatizo nini na kutibu yasiyohusika!
  Kama tatizo hujui basi washa pc yako kwa safe mode (naamini unajua safe mode ni nini wajameni...kama sivyo bas google it... ) na kama tatizo litakuwa linaendelea kujitokeza hata ukiwa ndani ya safe mode basi kwa kiasi kikubwa tatilo hili linasababishwa na hardware either mojawapo imekufa au kama kuna hardware mpya umeongeza kwenye pc yako. kama hi hivi just take it out na kama hujui ni nini kimekufa basi nakushauri ni vyema uipeleke kwa wataalamu zaidi wakusaidie ila kama unauhakika kuna kifaa kipya umefunga mda mfupi au siku chache zilizopita basi kitoe kwanza then ujaribu kutumia bila kifaa hiko...na ikiwezekana badilisha au angalia compatibility issues hapo!
  ikiwa umepita hapo na unauhakika hamna hardware iliyokufa wala hujafunga kitu chochote kipya (hivyo unauhakika kuwa hardware sio ishu) basi ukiwa katika safe mode kule kule scan computer yako for virus or spyware kwa antivirus iliyoapdated..fanya full scan( sku hizi kuna hadi antivirus unaweza ku install kwenye flash uka update then ukatumia kwenye pc nyingine) ila hakikisha una uhakika na hiyo antivirus..baada ya hapo kama utapata kitu safisha then iwashe pc yako kama kawaida(sasa angalia inawezekana hao virus wakawa waliharibu baadhi ya systems file na kusababisha pc yako isiwake kabis baada tu ya ku scan..hao inabidi ufanye windows repair).
  Kama scanning hukupata kitu na tatizo bado lipo basi sasa ukiwa kwenye safe mode fungua system restore utility (jinsi ya kuipata inatofautiana kulingana na windows gani unatumia ila pia waweza search google how to get system restore in windows (.....) ukaweka window yako na utaipata ila mara nyingi kwa xp huwa kwenye start>all programms>accessories>system tools utaona system restore hapo chagua tarehe ya nyuma ambayo walau una uhakika pc yako ilikuwa ipo poa).
  Sasa vipi kama hamna date yoyote zaidi ya tarehe hiyo hiyo ambayo inatatizo? au kama haija solve tatizo? Basi zima pc yako kisha unapoiwasha press F8 mara nyingi mpaka itakapoleta ile windows ya kuchagua safe mode ila usichague safe mode, chagua Run your system from the last known ‘good configuration'.... on the other hand, if you know a recent software installation is the cause, then restore to the point created at that date.
  Kama haya yoote hayaja solve tatizo lako basi sasa itabidi uingie ndani zaidi kutafuta suluhisho na hii itahusiana na kujua kwa ukamilifu code numberau hata sehemu u ya error code unayoonyeshwa pindi inapotokea blue screen, copy hiyo error then tafuta online habari zaidi kuhusiana na hiyo error. Kumbuka unaweza ukawa unasumbuka na tatizo kumbe kuna maelfu ya watu walishapitia tatizo hilo na walishalipatia ufumbuzi..hivyo na wewe unaweza pata majibu. Kumbuka blue screen sio tatizo kama matatizo mengine ambayo ukieleza tu utaambiwa aah hiyo..fanya hivi au toa hiki...NO! it differ from one pc to another wakuu..
  The bottom line with this error is that you will need to be patient as it may require a lot of trial and error.
  Sasa basi kwa wale waliokuwa hawajui, habari ndo hiyo..
  Nakaribisha maoni, ushauri au ujuzi zaidi...
   
 3. Ndekirhepva

  Ndekirhepva JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  jamaa wala hajarejea ku press Like ya hiyo tiba aliyopewa??????
   
 4. m

  mokiwah Member

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huenda bado anaorodhesha possible issues ambazo anahisi zimesababisha hilo tatizo lake...

  Labda niulize swali muhimu, unatumia antivirus gani mkuu? Na je ipo updated? Kuna kirusi kinachohusishwa na file la rundll32 linalopatikana kwenye windows folder. Kirusi hicho husababisha errors za namna hiyo na katika conditions hizo hizo mara mara!!!

  Nawasilisha!!!
   
 5. nxon

  nxon JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,149
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  ilishawahi ntokea kwenye desktop yangu aina ya hp ila niliangaika nayo mpaka nikasolve tatizo. Cha kwanza nlicho fanya nlkongoroa pc yote kila kitu nlkitenganisha kesho yake ndo nikavirudishia kama ilivyo kuwa mwanzo. Ikawaka fresh nikaitumia siku nzima wakati likuwa hata haikai dk10 inaleta blue screen. Baada ya hapo nikafanya disk defragement na nika download avg pc tune up nikai clean pc mpaka sasa miezi mi4 imepita sijawahi ona tatizo kama hilo.
   
 6. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  unajua ndo maana inakuwa ngumu sana kutoa suluhisho la moja kwa moja juu ya blue screen...na watu wengi huwa wanadhani blue screen ni tatizo...ukweli ni kuwa blue screen si tatizo ila ni matokeo ya tatizo/hitilafu flani ndani ya system...sasa ni hitilafu gani hapo ndo ishu...!!
   
 7. P

  Prince Nyange Member

  #7
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kangu marehemu! yaani nimemaliza google sijapata solution. kibaya zaidi disk drive & usb port zote hazifanyi kazi . sababu; nilikuwa nataka fundisha dogo wangu how to use pc kwa uvivu nikaamua kurestart portable yangu kwa kuhold down the shutdown button, nilipoiwasha tu inarestart automatically na kuishia kwenye b.s.o.d kisha kujirestart simultaneosly maisha. kumbe ndiyo mgeni anaaga bye bye! now iko kule kwenye makorokoro store.
   
 8. Isaac Chikoma

  Isaac Chikoma JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Asanteni wadau kwa mchango wenu,laptop yenyewe,ukiwasha tu directly inakuletea blue screen,nimetumia hirens boot niliyoweka kwenye flashi,nikaona ngoja labda niformat,nimewipe drives zote,nikatengeneza partition upya, kwahiyo option ya safe mode tuseme haipo,nimeweka bootable xp kwenye flash,

  Ukianza installation inafanya kaz vizuri inacopy files zote ila inapofika,''windows is starting! Ndo hako ka screen kanatokea,kwa kutumia hirens,nimefanya diagnosis,hard disk sectors ziko fine,nimetumia pia master boot record tools kuchech tazizo,sijapata ufumbuz,nimegoogle error niliyopata kwenye net,

  Solution nyingi ninazoziona zinaelezea kusolve tatizo kama os ipo ndani,lakini hii haina hata os,reason ya kuiformat ni kwamba ilikuwa hata hairespond kwenye safemode wala kurepair zaid ya kuleta blue screen.

  Kama alivosema mkuu hapo juu,pengine ni registry errors,au boot sector virus,au kinginecho,nashindwa kujua namna ya kutatua haya matatizo kwasababu hakuna os ndani ya lap,
   
 9. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Kama hutajali, jaribu kutafuta cd ya ubuntu uweke then uone inakuaje...nayo ikigoma basi kuna uwezekano mkubwa tatizo likawa ni hardware (HDD) yako ina ishu..au kama unaweza unaweza kuitoa hiyo HDD na kujaribu kui format kwenye External HDD reader au kwa kutumia pc ingine..
   
 10. Isaac Chikoma

  Isaac Chikoma JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  poa kaka ngoja nicheck.
   
Loading...