Helkopta ya Kijeshi ya Marekani yaangushwa kwa Risasi

Helkopta ya Kijeshi ya Marekani yaangushwa kwa Risasi

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
5,547
Reaction score
14,210
Hii ni aibu kubwa sana
20200815_020832.jpeg
 
Dah!...yaani ndege ya kijeshi kuangushwa ni aibu ? Au sababu ni ya Marekani ?
 
Ndege imeangushwa na risasi sio jiwe au wewe unaichukuliaje risasi kwa mfano
 
Dah!...yaani ndege ya kijeshi kuangushwa ni aibu ? Au sababu ni ya Marekani ?
Kwa kawaida helicopter ya kijeshi kuangushwa kwa risasi moja ni aibu kubwa sana. Kwani hiyo risasi ilimpata rubani?
 
Kwa kawaida helicopter ya kijeshi kuangushwa kwa risasi moja ni aibu kubwa sana. Kwani hiyo risasi ilimpata rubani?
Aibu ipo wapi hapo? Ulitaka iangushwe kwa risasi ngapi ili aibu isiwepo?
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Inaonekana tukio la kushangaza kwa vile ni Marekani.Mbona kuna matukio mengi yanayokea huku kwetu na hayaripotiwi? Piga chini.
 
Hebu soma kwanza hapa.

Ndege ye jeshi la Marekani yaangushwa na watu wasiojulikana

14 Agosti 2020

[https://ichef]

CHANZO CHA PICHA,US AIR FORCE

Maelezo ya picha,

Helikopta ina ya UH-1N Huey

Shirika la Ujasusi la Marekani limeanzisha uchunguzi baada ya helikopta ya kijeshi kupigwa risasi ilipokuwa inafanya mazoezi ya kawaida katika jimbo la Virginia.

Mtu mmoja alijeruhiwa katika tukio hilo Jumatatu na helikopta hiyo ikalazimika kutua kwa dharura.

Maafisa wanasema kwamba ndege hiyo ilikuwa inapaa umbali ya takriban futi 1,000 (mita 300) kutoka ardhini wakati ilipopigwa risasi.

Tukio hilo lilitokea mapema Jumatatu mchana kilomita 16 (maili 10) kutoka uwanja wa ndege wa Manassas, kaskazini mwa Virginia.

Helikopta hiyo ilitua kwa dharura katika uwanja wa ndege baada ya kupigwa risasi.

Mfanyakazi wa ndege hiyo aliejeruihiwa alipelekwa hospitali lakini ameruhusiwa kwenda nyumbani. Jeshi la Angani limesema kuwa ndege hiyo ya helikopta aina ya UH-1N Huey imeharibika kiasi.

Helikopta hiyo huwa inasafirisha wanajeshi waandamizi, viongozi wa kiraia pamoja na wageni wengine waheshimiwa, na kushughulikia uhamisho wa wagonjwa wakati wa dharura.

Shirika la Upelelezi la Marekani limesema linashirikiana na mashirika mengine ikiwemo afisi ya jeshi la angani inayoshughulika na uchunguzi maalum kutathmini kile kilichotokea.

Maafisa wamesema kwamba risasi hiyo ilifyatuliwa na mtu aliyekuwa ardhini lakini bado haifahamiki ikiwa ndege hiyo ilipigwa risasi kimaksudi au ilikuwa ajali iliyosababishwa na mtu ambaye alikuwa anafyatua risasi hewani kiholela.
 
Kwa nilivoelewa ilivyofyatuliwa risas ikatua kwa dharura haijaanguka Kama mnavozan ingeanguka Kama mnavozan ingelipuka
 
Kama ni ivyo basi ata manati inaweza kuiangusha iyo helcoppteer
 
Back
Top Bottom