Tunajua fedha zinatengenezwa, na zingine zinachakaa. Sasa naombeni kujua ni namna gani fedha (note/coin) mpya zinaingizwa kwenye mfumo?
Na ni busara gani husaidia kujua ni fedha kiasi fulani mpya zitengenezwe?
__________________________
Nianze kufafanua kua,kazi kubwa ya mabenki ni kukusanya fedha zilizo kwenye mzunguko ambapo kwa njia ya mzunguko,tukisema mzunguko tunamaanisha kutoa na kupokea (kupokezana). Katika mzunguko huu,benki hupokea pesa kutoka kwa Benki kuu,nazo benki hugawa fedha kwa watumiaji.
Pia ieleweke kua sio kila benki hupokea fedha kutoka Benki Kuu,benki nyingine hupokea fedha kutoka benki nyingine.
Njia hii ya kupokezana fedha (Yaani mzunguko) husaidia kutambua fedha chakavu,fedha chakavu upokelewa na benki kwa njia ile ile benki huzipeleka Benki kuu. Benki kuu ndio yenye jukumu la kutoa Hela chafu kwenye mzunguko na kuleta fedha mpya. Benki kuu huwa inakusanya hizi fedha chakavu na kuziteketeza (Kwa njia zao sahihi) na kutengeneza fedha mpya. Benki kuu,kwakutumia takwimu za Kibenki hujua mzunguko halisi wa fedha,wana takwimu za fedha chakavu na wao ndio hutoa hizi hela kwa utaratibu usiku. Benki Kuu au kwa lugha ya kukopa (Central Bank) ndio inakaa kama muhimili wa Bank Zote,na mwisho wa siku fedha zote hurudi kwao.
Busara gani 👈 Sio Busara bali takwimu husika,zinajua hitaji la mzunguko na wanahakikisha wanapeleka kiasi sahihi.
Kumbuka hela yako haina thamani kama umeichimbia tu Chini na haipo kwenye mzunguko