kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,086
WIKI hii Kampuni ya Reli Nchini (TRL) imeanza kutoa huduma ya usafiri wa treni mpya inayotoka Stesheni hadi Pugu jijini Dar es Salaam.
Juzi na jana treni hiyo imeanza kufanya majaribio kwa kutotoza nauli ili kuwawezesha abiria kujifunza jinsi ya kuitumia pia kuwapatia TRL nafasi ya kujua changamoto kwa watumiaji. Hata hivyo leo huduma ya usafiri inaanza rasmi na abiria wataanza kutozwa nauli.
Treni hiyo itakuwa na mabehewa 10 na itapita katika vituo 10 vya Pugu Stesheni, Mwisho wa Lami, Gongo la Mboto, FFU Mombasa, Banana, Njia Panda Segerea Karakata, Vingunguti Mbuzi, Bakhresa, Kamata na Stesheni. Huduma inayotolewa na treni hiyo inasaidia kupunguza tatizo la usafiri kwa wakazi wa maeneo ambayo treni hiyo inapita.
Hakika hatua ya TRL kuanzisha huduma hiyo ya usafiri inapaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo kwa kuwa imeondoa kero ya muda mrefu ya tatizo la usafiri. Wananchi wanaotumia treni hiyo sasa wataweza kuwahi maofisini na katika shughuli mbalimbali za maendeleo bila kupoteza muda na kuunga mkono kauli ya Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano ya “Hapa Kazi Tu.”
Wananchi wanaotumia usafiri huo hawapati adha ya foleni. Pia treni hiyo itasaidia kupunguzia gharama za usafiri na kuboresha hali ya maisha katika kaya kwa kuwa awali walilazimika kupanda magari ya watu binafsi kwa Sh 2,000 na wakati mwingine walilazimika kulipa nauli mara mbili.
Napenda kupongeza uongozi mzima wa kampuni hiyo na kuwasihi kufanya tathmini ya watu wanaotumia usafiri hiyo ili kama itabaini watu ni wengi iwezi kuongeza idadi ya mabehewa ili kuepuka msongamano ulioonekana kwa siku hizo mbili. Ni dhahiri kuwa baada ya kufanya majaribio kwa siku mbili wameona mafanikio na changamoto katika njia hizo hivyo kuweza kufanyia kazi wakati wakianza kazi rasmi leo.
Katika baadhi ya mambo ya kufanyia kazi ni pamoja na kuhakikisha kunakuwa na usalama katika milango kwa kuweka wasimamizi kwani kumekuwa na abiria waliokuwa akining’inia milangoni jambo linaloweza kusababisha ajali wakati wa safari hizo.
Katika kuhakikisha usafiri huo unakuwa na tija zaidi ni vyema wananchi kuusimamia na kuwa sehemu ya mradi kuhakikisha kuwa miundombinu ya treni hiyo inalindwa ili huduma hiyo iweze kuwa endelevu.
Mbali na kuhakikisha wanafuata taratibu zote zilizowekwa na kampuni hiyo katika usafiri ni vyema abiria kuzingatia masuala ya usafi kwa kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenziwe kwa kuhakikisha vyombo vya kuhifadhia uchafu vinatumika ipasavyo.
Hakika pongezi ziende kwa menejimenti ya kampuni hiyo iliyoona mateso ya wakazi wa maeneo hayo na kuamua kuanzisha usafiri huo na kutanuka zaidi katika maeneo mengine yenye reli kwani inasaidia kupunguza misongamano barabarani.