Kashaijabutege
JF-Expert Member
- Oct 20, 2010
- 2,696
- 740
Nilifurahi sana jinsi madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba walisvyoshikamana kuipinga bajeti iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Wilaya. Walidai hawaipitishi kwa sababu kiasi kikubwa kimetengwa kwa ajili ya matumizi ya ofisi ambayo yanawanufaisha watendaji wa halmashauri; na kiasi kidogo ndicho kilitengwa kwa ajili ya maendeleo.
Mama (Mkurugenzi) alimwaga chozi na kuamuru watendaji wa halmashauri watoke nje.
Itapendeza kama madiwani wengine wataiga mfano huu mzuri.
Source: ITV
Mama (Mkurugenzi) alimwaga chozi na kuamuru watendaji wa halmashauri watoke nje.
Itapendeza kama madiwani wengine wataiga mfano huu mzuri.
Source: ITV