Ni kweli.Mimi sasa hivi ni mara chache sana naingia Benki labda iwe ni shida ya lazima. Mimi mara nyingi natumia SimBanking kutatua matatizo yangu ya kifedha. Nikitaka fedha taslimu natoa fedha kwenye SimBanking yangu na kuweka kwenye Namba ya Mpesa yangu na kwenda kutoa hela zangu kwa wakala, Vile vile nikiwa na fedha taslimu nataka kuweka kwenye akaunti yangu ya CRDB ninaenda kwa wakala wa Mpesa ananiwekea fedha kwenye namba yangu ya Mpesa na baadaye nazihamisha kupeleka kwenye akaunti yangu ya CRDB. Hakuna haja kutembea na fedha nyingi taslimu siku hizi jaribu kutumia simBanking.