Hekima ya baba huonekana kwa mtoto

Hekima ya baba huonekana kwa mtoto

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
282
Reaction score
275
Ukiwa mzazi mara nyingi hupenda kutumia ukali, fimbo na nyenzo kadha wa kadha katika kuwaelewesha watoto wetu katika makuzi yao.

Lakini leo nakupa changamoto kuwa kama mzazi kile kinachoonekana kwa mwanao, ndiyo kile ulichokihitaji.

Nadharia zinasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, lakini mimi ninaenda ndani zaidi ili kujenga zaidi. Hekima ya baba huonekana kwa mtoto, hivyo usipomfundisha hekima yako usitegemee yeye kujifunza kwa dunia.

Wengi tumekulia malezi ya fimbo na ukali kiukweli zinasaidia lakini hazijengi sana, fimbo zinatengeneza uoga, hofu, kutokujiamini, amri lakini hata uwezo mdogo wa kufikiri. Haya ni madhara ambayo huonekana baadaye sana.

Hekima ya baba inakua ni uoga, hofu, kutojiamini na kadhalika ambapo vijana wa leo ndiyo tatizo kubwa ufahamu (mentality) zimeharibika tangu wakiwa wadogo, halafu wakifika ukubwani ghafla wanatakiwa wajitegemee. Ni mtihani mkubwa zaidi kwao sababu hekima ya baba imepungua sana, tunakimbilia sana kuwalaumu watoto bila kutafuta chanzo. Samaki mkunje angali mbichi.

Haya twende kuangalia kwanini hekima ya baba na sio ya mama. Katika hili kwanza mtoto anazaliwa; kama mzazi tambua mtoto anaheshimu na kujifunza sana kwa kile unachokifanya siyo unachosema. Ndiyo maana ni rahisi kumkataza na kisha akarudia muda huo huo lakini akaacha kwa kile ambacho umekiacha.

Hivyo, hekima ya baba iko kwenye makuzi yake. Watoto hurithi 79% ya baba na 21% tabia za mama, hivyo mtoto huiga zaidi matendo ya baba kuliko ya mama.

Akili ya mtoto moja kwa moja huwa anazaliwa akiwa na ufahamu wa baba ni sauti ya mwisho, kiongozi. Hata wamama wengi hutumia neno "Baba yako akija nitamwambia" na mtoto anafanya hata kama hajajua; hii ni kwa sababu mtoto anaiga zaidi na kubeba vya baba.

Sasa, kabla sijaendelea nikujibu kwanini Biblia imeandika mwana mwenye hekima humfurahisha babaye, bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye. Malezi na makuzi ya mtoto husimamiwa asilimia kubwa na mama yake: kutungwa mimba, kubeba mimba, kujifungua, kunyonyesha, kumlisha na kadha wa kadha. Hivyo muda mwingi wa mtoto hupokea malezi na makuzi ya mama, lakini note hii point, "Mwana mwenye hekima" kwanini awe ni mzigo wa mama wakati amerithi tabia za baba? Ipo hivi, katika maisha ya kuishi pamoja mama ana nguvu kuliko baba ndani ya nyumba.

Ukiwa mwanaume, baada ya kuwa na mwanamke ndani, anakuwa na nguvu juu yako. Atakuchagulia nguo za kuvaa, chakula cha kula, muda wa kurudi hadi marafiki wa kuhusiana nao. Mwanaume husikiliza tu ni kwasababu mama huwa mkubwa ndani ya nyumba wa kubadilisha tabia na mienendo ya baba ambayo haitaki na baba akabadilika.

Mifano hai ni mingi. Watu hubadilika baada ya kuanza kuishi na mwanamke. Sasa kama mama ataziacha tabia mbaya za baba na mtoto akaja kurithi, hilo ni tatizo la mama kuziacha kwa baba ndiyo maana ni mzigo wake.

Biblia imeandika: Waheshimu baba na mama yako (Waefeso 6:2), lakini mstari wa 4 "Nanyi akina baba msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana"

Biblia inaanza kumheshimu baba sababu amepewa majukumu ya kuwa kiongozi / kichwa cha familia, hivyo mtoto anapozaliwa moja kwa moja anakuja na heshima zaidi kwa baba na ufahamu wake anaiga sana tabia za baba. Hivyo, hekima yako kama baba itaonekana kwenye matendo ya mwanao jinsi ulivyo muonesha tabia zako na vitu vya kuiga kutoka kwako.

Kama hekima yako ni fimbo, usitegemee mwanao kuja kuwa na hekima ya uvumilivu. Kama hekima yako ni ukali, usitegemee mwanao kuja kujiamini kufanya maamuzi bila kusitasita. "Waleeni katika adabu na malezi ya Bwana"

Kila unachokifanya leo mbele ya mtoto wako, ndiyo atakachorudia kesho, hivyo kama mzazi jitahidi sana kujenga ufahamu wa mwanao kwa hekima na si tabia za ukali na fimbo. Wanajifunza zaidi kwa matendo yetu zaidi ya maneno na adhabu zetu.

Anza leo kujenga ufahamu sahihi kwa mwanao; wewe ndio unatengeneza ama kuharibu kesho yake akiwa mtu mzima.

Uwezo wa uthubutu, upeo mkubwa, heshima na adhabu anavirithi kwa kuviona na kujifunza.

Elisha Chuma

IMG_20191230_103024_989.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Riwaya nzuri, ila ndefu sana kwa standard ya kusoma habari kwenye social media. Hii inanikumbusha zile terms and conditions zinazowekwa na social media wakati wa ku-sign in as a new user
 
Mimi isingekuwa ni fimbo na ukali wa wazazi, ungekuta nimejifia na uzinzi au mihadarati. Nawashukuru sana wazazi wangu kwa kuwa wamenifanya niishi hadi leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
ni kweli yaani walichokiruhusu wazazi ndicho ulichokipata na walichokikataza ndicho ulichokiacha so kwa hulka za utoto na makuzi fimbo ilitumika kuonya sio kukuumiza ndio maana unaikumbuka leo na kuwaona mifano bora.
 
Riwaya nzuri, ila ndefu sana kwa standard ya kusoma habari kwenye social media. Hii inanikumbusha zile terms and conditions zinazowekwa na social media wakati wa ku-sign in as a new user
jitahidi kusoma tu,ni pana sana kwa kuifupisha ingepoteza dhima yake...
 
Je, kwa wale waliolelewa na mzazi mmoja hasa mwanamke tu, yaan watoto wa single mothers.

Hawa unawazungumziaje mkuu na hasa ukuzingatia baba hayupo au hayupo karibu na mtoto..?

hawa huwa wanaishi na wanaishi kwa nadharia na za maisha ya baba ndio maana mama akipanda chuki mtoto hakuelewi hata ubinadamu unapungua kwako,sababu mama alichukua nafasi ya baba hivyo alichukua nafasi ya baba hivyo ukirudi haelewi role yako ni ipi kwenye maisha mfano : Nassib Abdul ( Diamond Platnumz), Steve Jobs na mifano mingine.

lakini pamoja na yote hayo mtoto huwa anakuwa na maisha ya tofauti sana na yule wa wazazi wawili huwa anaonyesha zaidi tabia na hulka za malezi ya mama hasa ambae yuko mwenyewe,huwa kuna kukosekana fulani kwa hali ya uanaume ndani yake hekima,adabu,busara,maisha ya kiume huwa yanapungua haijalishi ni kwa namna gani ila huwa kuna hali fulani ya kiume inakuwa imepungua sababu ile hekima ya kiume ( ya baba ) haipo ndani yake.
 
Mithali : Mlango 22
6 Mlee mtoto katika njia impasayo,Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
1. Bar Jonah
2. Melchizedek
3. Baraka
4. Ethan/ Moses
5. Faith

Ni kweli kabis hapo kwenye "njia impasayo "ndio naweza kusema ni mbadala wa hekima,kizazi tulichonacho kinatokana na hekima za wazazi wao na,hii inaenda kizazi hadi kizazi kinachotengeneza mtoto,kijana wako ni hekima yako tena ile ya vitendo.
 
Mitoto mingi ya Kiafrika bila ya mboko za kutosha hua inakosa heshima na adabu.
Hata aliyetunga methali ya Punda haendi bila ya fimbo ni muafrika, sisi waafrika tulio wengi bado zile mentality za kitumwa hazijatoka katika damu yetu.

Mimi kwa upande wangu nasisitiza mboko iendelee kua nyezo ya mafunzo katika ukuaji wa watoto wetu.
Watoto wengi waliokosa nyenzo hii muhimu katika makuzi yao wamekua na tabia ambazo haziendani na mila, desturi pamoja nidhamu sahihi ya maisha halisi ya muafrika.

Hata mashoga wengi wakielezea maisha yao ya utotoni wanakuambia kabisa kua wao walikua hawachapwi fimbo na wazazi wao pindi walipokua wanakosea, sana sana walikua wanapigwa tu vibao vya matakoni.

Sent from my DUB-LX1 using Tapatalk
 
Riwaya nzuri, ila ndefu sana kwa standard ya kusoma habari kwenye social media. Hii inanikumbusha zile terms and conditions zinazowekwa na social media wakati wa ku-sign in as a new user
Hahaha ukikuta siku wame release identity yako ya JF usianze kulaumu. Kumbe tu hukuamua kusoma terms and conditions.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom