Hekima iliyotukuka ya mwalimu JK Nyerere

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
Amani iwe nanyi wanabodi!

Basi, ikatokea miaka ile msimu mmoja karibu na msimu wa baridi kwisha, Waziri mmoja mwandamizi katika serikali ya Mwalimu Nyerere akazuru shule moja ya sekondari ya wasichana. Hata asijizuie pepo la uzinzi, basi akatoa agizo kwa Mkuu wa skuli ile amtafutie binti mmoja ili ampe usingizi usiku ule wa baridi kali. Basi. yule Mkuu wa shule hekima ikamuongoza kuwa si vema kumtafutia waziri yule watoto anao walea kwani ni kinyume cha maadili. ili asionekane amekaidi agizo la mheshimiwa, akawauliza wale wanafunzi ni nani miongoni mwao ni ndugu wa yule waziri? mmoja miongoni mwao akajitokeza akasema, yeye ni mpwa wa yule Waziri,basi mkuu wa shule akasema hakika nimepata mtu niliye mhitaji hasa! akamwelekeza yule binti aende akamhudumie Waziri hata ikibidi alale hukohuko. Jioni ilipo wadia binti akaenda, yule Waziri akang'aka mbona hivyo? inakuwaje ameniletea aliye ndugu wa damu? akakasirika akamwambia yule binti rudi shuleni, huyu mkuu wa shule atakuwa punguani kweli.

Kesho yake kwa hasira waziri akamlima barua ya kumwachisha ukuu wa shule yule mama aliye tenda yaliyo mema.Akasikitika sana lakini hekima ikamuongoza aende wizarani akamshitaki waziri juu ya kadhia ile.Kwa ukubwa wa jambo lenyewe akaelekezwa aende kwa Nyerere.Kesi ikawa imefika kwa mwenye Nchi.Alipo simuliwa kisa kile chote , Nyerere akaagiza aitwe yule waziri ili kesho yake wawepo wote mshitaki na mshitakiwa ili haki itendeke.

Basi ikawa siku ya pili ilipo wadia Mkuu wa shule na Waziri wakaitwa ofisini kwa Nyerere. kuona vile yule Waziri nguvu zikamwishia kwani alijua kisa cha kumwachisha mkuu wa shule bila kuzingatia sheria, kanuni na taratibu kimetinga kwa Nyerere.Alipo ulizwa juu ya yasemwao kuwa alitaka atafutiwe msichana wa kulala nae hakubisha, akakiri kupotoka.

Basi kunako saa saba mchana siku iliyofuata baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, akatangaza kutengua uteuzi wa yule waziri na papo hapo akamteua yule mkuu wa shule kuwa mbunge na kuwa WAZIRI WA ELIMU !!

Nyerere alitambua haki ya mtuhumiwa kujitetea mbele ya sheria.Hakutumbua majipu bila kupata ukweli wa pande zote husika.nawasilisha kisa cha kweli kabisaaa.
 
Kama ni kweli basi hakika alilishughulikia suala hili kwa hekima sana. Ni kisa cha kusisimua sana. Tujiulize ni waziri gani wa elimu alikuwa mwanamke wakati wa mwalimu nyerer??? Bila shaka tutapata majawabu
 
Huyo waziri aliyetimuliwa kazi bila shaka atakuwa ni yule anayetoka upareni, kwa kuwa ndiye aliyefahamika kuwa hiyo ndiyo ilikuwa 'staili' ya uongozi wake.
 
Yapo mambo ya wazi ambayo hayahitaji utaratibu kama huo, kwa mfano kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa kwenye eneo lake hakuna wafanakazi hewa kunahitaji maelezo gani hapo ya kujieleza, ulitaka aitwe aseme alipotoshwa na wataalamu wake ili iwe nini kwa gharama ya nani. Sasa leo tanaambiwa wafanyakazi 102 wamegundulika ni hewa kwenye Mkoa wake huohuo. Unajua wamesababisha hasara kiwango gani mpaka sasa kwa serikali maana hata mwezi uliopita hawa watu hewa wamepata pesa kiulaini. Sasa swala hilo la kuomba kutafutiwa msichana wa shule kwa lengo la kufanikisha usingizi wake huyo Waziri, hilo ni jambo jingine kabisa maana linahitaji kujiridhisha zaidi kabla ya kufikia maamuzi maana kwanza halikupelekwa kama lalamiko kwa raisi bali lalamiko lililopelekwa lilikuwa ni kitendo cha kutimuliwa kazi kama mkuu wa shule bila kufuata taratibu kufuatwa. Sasa kwenye maelezo ndio kisa hicho cha kutafutiwa msichana wa shule ndio kikaelezwa kuwa kwa kushindwa kutekeleza matakwa ya Waziri ndiko kulikopelekea kufukuzwa ukuu wa shule. Hata mimi katika hali ya kawaida nitapenda nijiridhishe kabla ya kuchukua hatua. Ni maoni yangu kuwa umefika wakati tuwe serious na kazi tunazotumwa kuzitekeleza. Mfano mzuri ni Mkuu wa mkoa wa Rukwa kusimama kidete kwa kuikataa report ya watalaamu wake kuwa kwenye mkoa wa Rukwa hakuna wafanyakazi hewa. Baada ya kufanya ukaguzi upya wmegundulika wafanyakazi hewa kibao.
 
Back
Top Bottom