Hekaya za Marekani

Kanjwinjwi

JF-Expert Member
Jun 22, 2017
258
343
MICHEZO YA KIPUMBAVU INAYOENDELEA KTK DUNIA HII

1.Trump alisema bora ya ISIS kuliko waasi wa Kikurdi maana Wakurdi ni wabaya na wao si malaika.

2.Trump akasema temewamaliza hawa ISIS asilimia mia hatuna haja ya kupigana vita Syria isiyo na faida na mumuache Bwana Assad atawalinda Wakurdi dhidi ya Ukatili wa Turkey.

3.Trump akasema Turkey ina maslahi makubwa kwa Marekani kuliko hao vidaso wa Kikurdi.

4.Trump akasema tunayatoa majeshi yetu syria na kuyapeleka iraq kuendelea kuwapiga ISIS.
๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜

Hapana, huyu Trump hana ugonjwa wa akili tuseme amechanganyikiwa. Wanachokiongea ndicho kinachoakisi yaliyo katika mioyo yao na wakati mwingine hupaswi kuamini wanayoyasema bali angalia wanachokifanya na hicho ndicho walichokusudia.

UPUMBAVU WAO NI

๐Ÿ‘‰Anaonesha kumkubali Assad kwa sasa kumbe ni kwa kuwa NATO na Marekani vita dhidi ya Assad imewashinda na uhakika walikuwa Syria kumpiga Assad na siyo ISIS. Ushahidi upo hata wa waziwazi.

๐Ÿ‘‰Marekani haieleweki ima inawasapoti Wakurdi ama Turkey. Kimsingi, Wakurdi bado wana umuhimu kwao kwa kuwa ado pia wanaihitaji Syria. Hivi unaamini kuwa bado hawaisakami Syria na kuimezea mate?

Pia, Turkey ana umuhimu kwao kwakuwa ni mwanachama mwezao wa NATO. Nikwambie tu miongoni mwa nchi kadhaa hivi ambapo Marekani inahifadhi silaha zake za nyuklia, Uturuki ni moja wapo, ukiachilia mbali masuala ya kibiashara.

๐Ÿ‘‰Marekani ikifika kipindi cha uchaguzi watu kama huyu mwehu Trump utasikia wanasema oh, "Tutawarejesha wanajeshi wetu nyumbani." Unayatoa majeshi Syria unayapeleka Iraq. Hivi Iraq ndiyo nyumbani kwenu au siku hizi Iraq ni Marekani?

๐Ÿ‘‰Unasema umewamaliza ISIS asilimia mia halafu unasema tena unaenda kupigana nao.

๐Ÿ‘‰Mapimbi wa Kimarekani na mashosti zao wa NATO wanabase za kijeshi nchini Iraq zina zaidi ya miaka 10 lakini cha kushangaza ISIS ilizaliwa hapo, wao wakiwepo na mpaka ikavunjika wakiwa hapo hapo.

Ikumbukwe hawa ISIS walifanikiwa kuichukua sehemu ya ardhi ya Iraq na Syria inayolingana na ukubwa wa nchi ya Uingereza.

Wakawa na makao makuu Mosul (Iraq) na Raqqa (Syria).

Hawa mazezeta wa Kimagharibi (Marekani na NATO) walikuwa wanafanya nini na wakati wana nguvu za kijeshi ambazo kwa ISIS wao wana silaha hafifu? Bila shaka waliremba mwandiko - kupakana poda tu.

๐Ÿ‘‰Mamluki wa ISIS bado wanaishi na huyu gwiji wao Abubakr Al Baghdad anadunda tu na ku-survive huku akila bata. Nani kakwambia ISIS inapigwa vita vikali na Magharibi?
๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†

KAMWE HAWATOTOA MIKONO YAO AU KUIACHIA MASHARIKI YA KATI MPAKA WAFANIKISHE KILE WANACHOTAKA

โœ‹โœ‹โœ‹โœ‹โœ‹โœ‹โœ‹โœ‹โœ‹โœ‹โœ‹โœ‹โœ‹โœ‹
VITA INAMUDA MAALUMU NA MALENGO MAALUMU.
 
hivi naipataje namba ya uwoya

Hivi ulishindwa kwenda insta na facebook kutafuta namba ya Irene halafu unakuja hapa unazengua watu wanaleta news kulingana na jukwaa linavyosema. Kama hutaki Mambo ya nje basi usifungue jukwaa hili bali nenda shilawadu ama mitandao ya kimbea
 
Back
Top Bottom