DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @chadematzofficial Bara John Heche @hechejohn amesema Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu ni tunu ya taifa huku akishinikiza kuachiwa kwa kiongozi huyo bila masharti.
Heche ameyasema hayo leo Januari 3, 2026 katika hotuba yake kwa taifa akimtaja Lissu kama mtu anayesimamia haki na mtetezi wa watu ambaye msimamo wake unakubalika na wengi.
"CHADEMA na watanzania tunajivunia kuwa na Tundu Lissu kama tunu ya taifa, mtetezi wa haki. Kwa sauti kubwa tunataka Tundu Lissu aachiwe bila masharti yoyote".