PreGE2025 Heche: Nimekutana na Lissu gerezani, amesema mapambano yaendelee

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,177
Reaction score
7,472
Makamu Mwenyeliti wa CHADEMAB(Bara), John Heche amesema kuwa amekutana na Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu katika Gereza la Ukonga anakoshikiliwa na kiongozi huyo amewataka wanachana wa chama hicho kuendeleza mapambano.

Lissu alikamatwa Aprili 12 wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma na kisha kuletwa Dar es Salaam ambako alifunguliwa kesi ya uhaini katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu.

Hata hivyo, jana April 18, kulikuwa kuna taarifa kuwa kiongozi huyo alihamishwa Gereza la Keko lakini haikujulikana amepelekwa wapi, hadi ilipojulikana leo kuwa yuko Gereza la Ukonga.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akizungumza leo Aprili 19 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Ukonga Mombasa, Heche amesema amekutana na Lissu Gereza la Ukonga.
Go6QDyMXsAAQCw_.jpg

Go6QDyTWEAEPF68.jpg

Go6QDyTWwAAhmtO.jpg

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Ukonga, Aprili 19, 2025

"Saa mbili zilizopita nimetoka gerezani na nimeonana na Lissu. Kama mnavyojua Lissu alikamatwa na alifunguliwa kesi kubwa ya uhaini, ambayo hukumu yake ni kifo.

"Mtu ambaye alipigwa risasi 16, Serikali imemfungulia kesi ya uhaini, hajaiba kitu cha mtu, hajamkosea mtu, kosa lake ni kitaka kila mtu achague kwa usawa," amesema.

Soma Pia: Brenda Rupia: Taarifa rasmi Tundu Lissu amehamishiwa gereza la Ukonga, Heche anatarajiwa kufika Ukonga leo kwa ajili ya kumwona

Heche amesema amemkuta Lissu akiwa anaendelea vizuri.
"Amesema mapambano yaendelee na mimi nasema mapambano yaendelee."

Kuhusu kuhamishwa gereza, Heche amekosoa kuhamishwa kwa kiongozi huyo bila kuwajulisha.
"Wamemhamisha kutoka Keko kuja Ukonga bila kutaarifu wanafamilia yake. Nchi hii sio kikundi fulani kinachoamua kila kitu.
"Hata kina Mandela alipofungwa Robben island makaburu Wazungu walijulisha wanafamilia," amesema.
 
Makamu Mwenyeliti wa CHADEMAB(Bara), John Heche amesema kuwa amekutana na Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu katika Gereza la Ukonga anakoshikiliwa na kiongozi huyo amewataka wanachana wa chama hicho kuendeleza mapambano.

Lissu alikamatwa Aprili 12 wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma na kisha kuletwa Dar es Salaam ambako alifunguliwa kesi ya uhaini katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu.

Hata hivyo, jana April 18, kulikuwa kuna taarifa kuwa kiongozi huyo alihamishwa Gereza la Keko lakini haikujulikana amepelekwa wapi, hadi ilipojulikana leo kuwa yuko Gereza la Ukonga.

Akizungumza leo Aprili 19 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Ukonga Mombasa, Heche amesema amekutana na Lissu Gereza la Ukonga.
View attachment 3309682
View attachment 3309683
View attachment 3309685
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Ukonga, Aprili 19, 2025

"Saa mbili zilizopita nimetoka gerezani na nimeonana na Lissu. Kama mnavyojua Lissu alikamatwa na alifunguliwa kesi kubwa ya uhaini, ambayo hukumu yake ni kifo.

"Mtu ambaye alipigwa risasi 16, Serikali imemfungulia kesi ya uhaini, hajaiba kitu cha mtu, hajamkosea mtu, kosa lake ni kitaka kila mtu achague kwa usawa," amesema.

Heche amesema amemkuta Lissu akiwa anaendelea vizuri.
"Amesema mapambano yaendelee na mimi nasema mapambano yaendelee."

Kuhusu kuhamishwa gereza, Heche amekosoa kuhamishwa kwa kiongozi huyo bila kuwajulisha.
"Wamemhamisha kutoka Keko kuja Ukonga bila kutaarifu wanafamilia yake. Nchi hii sio kikundi fulani kinachoamua kila kitu.
"Hata kina Mandela alipofungwa Robben island makaburu Wazungu walijulisha wanafamilia," amesema.
Wana wa Mungu tuendelee kumpiga shetani kwa nguvu
 
Kuhusu kuhamishwa gereza, Heche amekosoa kuhamishwa kwa kiongozi huyo bila kuwajulisha.
"Wamemhamisha kutoka Keko kuja Ukonga bila kutaarifu wanafamilia yake. Nchi hii sio kikundi fulani kinachoamua kila kitu.
Watu inabidi waelewe maana ya jambo hili na ni hatari kubwa. Ndiyo maana sasa kuna makundi rasmi ya kuteka watu kinyemela. Ni serikali isiyo wajibika kwa yeyote. Inajifanyia mambo itakavyo yenyewe bila ya kufungwa na taratibu za kisheria au katiba.
 
Lissu kua Mwenyekiti wa Chama ilikua Mistakes kubwa sana kwa Wakubwa sijui walijisahau vipi Mwamba huyu hapa Nyuma yao Misimamo ya Lissu ni hatari
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom