Heche aoneshe Msimamo Yeye Mwenyewe kwa kutoshiriki Uchaguzi wa 2020 Kama Tume ya Uchaguzi haitokuwa Huru!
Ni sawa na Sheikh kuhubiri Nguruwe ni haramu lakin kila kwenye Mnuso wa Nguruwe anashiriki Halafu akishiba anakuja kulalamika waumini wake wanalishwa Nguruwe!
Angalau Seif Sharif kishawahi kususia Chaguzi kuonesha kutoridhika kwake!
Mkishiriki uchaguzi wa 2020 mkiwa mnajua Tume si huru Halafu mkishindwa mkilalamika tutawaona Wanafiki tu
Miaka 27 iliyopita Simba iliwahi kuingiza Timu kucheza na Yanga, baada ya kipindi cha kwanza kuisha walikataa kurudi Uwanjani kwa kisingizio Yule Refa walimkataa kabla ya Mechi, japokuwa Mie ni Simba lakin nikajiuliza ina maana Dakika 45 za Mwanzo tulikuwa hatujui kuwa Huyu ndie Refa tunaemlalamikia?