Heche: Mkuu wa Mkoa anamuomba radhi Magufuli, CHADEMA kushinda kwenye udiwani, kuna haja ya sisi kushiriki uchaguzi?

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
Mbunge John Heche akichangia kwenye kongamano la Demokarasia amehoji kuna haja gani ya upinzani kushiriki kwenye uchaguzi ambao matokeo yake yameshapangwa?

ametolea mfano uchaguzi wa juzi ambao CHADEMA wameshinda kata 1 kati ya 43 na mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuomba radhi kwa Magufuli kisa CHADEMA imeshida kwenye kata yake

Watu wamepigwa na kuumizwa sana hata yeye alipokuwa akisimamia uchaguzi alipigiwa simu na waziri kuambiwa aondoke ili asipigwe

Amehoji Watanzania tupo tayari kuendelea na demokrasia hii ambayo matokeo yanafahamika kabla?
 
Jamaa ataagiza mawasiliano ya simu ya mkononi ya Heche kwa siku husika yachunguwe ili huyo waziri abainike na kisha apigwe cheni.

Mkisikia kuna mtu kapigwa chini basi mjue hii bila shaka ndio itakuwa sababu.
 
Refa ni wa Chama A, Mshika kibendera ni wa Chama A, Kamisaa ni wa Chama A, Walinzi ni Chama A. Na wachezaji wa Chama A wakimchezea Rafu na Kumwumiza wa Chama B wanasifiwa wanajisifia kwa mchezo usiokuwa wa Kiutu. Hakika, Haki huinua jamii iliyostaarabika bali Dhuruma na Uonevu ni Aibu Kubwa ktk jamii. Play 4 TL
 
Heche aoneshe Msimamo Yeye Mwenyewe kwa kutoshiriki Uchaguzi wa 2020 Kama Tume ya Uchaguzi haitokuwa Huru!

Ni sawa na Sheikh kuhubiri Nguruwe ni haramu lakin kila kwenye Mnuso wa Nguruwe anashiriki Halafu akishiba anakuja kulalamika waumini wake wanalishwa Nguruwe!

Angalau Seif Sharif kishawahi kususia Chaguzi kuonesha kutoridhika kwake!

Mkishiriki uchaguzi wa 2020 mkiwa mnajua Tume si huru Halafu mkishindwa mkilalamika tutawaona Wanafiki tu

Miaka 27 iliyopita Simba iliwahi kuingiza Timu kucheza na Yanga, baada ya kipindi cha kwanza kuisha walikataa kurudi Uwanjani kwa kisingizio Yule Refa walimkataa kabla ya Mechi, japokuwa Mie ni Simba lakin nikajiuliza ina maana Dakika 45 za Mwanzo tulikuwa hatujui kuwa Huyu ndie Refa tunaemlalamikia?
 
Wako tayari hata kuua raia ili wapate udiwani kweli ccm Mungu anawaona
 
Alafu iweje???jinga kubwa wewe
 
Wale jamaa wakibiti nilikua nawachukia sana lkn nimegundua kumbe walikua wanadai democrasia ila hatukujua tukawa tunawabeza
 
Madikteta uchwara ndivyo walivyo!!!! Haijawahi kutokea Mkuu wa mkoa miaka ya nyuma kuomba msamaha kwa Mkapa au Kikwete kwa kushindwa uchaguzi na upinzani.

Hii ni kutaka Wakuu wa Mikoa wafanye kila udhalimu kuhakikisha wanashinda chaguzi vinginevyo wanaweza kutumbuliwa na uchwara.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom