Wilguy kwanza kabisa unaposema kiwango cha elim hakija shuka unamaanisha nini? takwimu tunazosomewa na ndalichako zina incluide wanafunzi wote hata waliopata 4 ambao wanaweza kupata academic certificate hawa mara nyingi ndio wanao kwendaga vyuo vya ualim au unesi. pia wanafunzi wanaopata daraja la 1 ni wachache ukilinganisha na miaka ya nyuma na hii inathibitika unapoangalia idadi ya wahitimu with respect to daraja husika. pia siku hizi div 3 scoreres ni wengi sana kuliko 1&2.Kutakana na Takwimu, ufaulu uweshuka.
UKIANGALIA KWA KINA: kiwango cha ufaulu hakijashuka! Kilichotokea ni kwamba; kutokana na pupa za serikali, serikali imelegeza masharti kiasi kwamba waalimu na wanafunzi wasio na uwezo wanaingia shule za sekondari. Mfano Mwalimu aliyefeli kuruhusiwa kufundisha, mwanafunzi asiyejua kusoma na kuandika kuingia sekondari, ambako anafundishwa na mwalimu aliefeli, mwalimu aliyefeli anapewa darasa lenye wanafunzi 70+ ili awafundishe.
Miaka ya nyuma ilikuwa yeyote anayeingia sekondari anastahili, hivyo wengi walikuwa wanafaulu.
Tunakoelekea: tunaelekea nyakati ambazo kutakuwa na kundi kubwa wa wahitimu (takribani kijiji kizima) waliofeli sekondari i.e Form IV. Hivyo thamani ya elimu ya sekondari kuwa kama elimu ya darasa la saba.
Suluhu ipo ila kunahitajika utashi wahali ya juu katika kuutekeleza ipasavyo. majibu yapo ila hakuna ujasiri wa kutekeleza.
mshamu nafikir kuna haja ya dhat ya kujadili mustakabali wa elimu ya tz na ifanyiwe ufumbuzi mapema sana vinginevyo, hili taifa litakwisha kabisa. Tz will become an extinct nation very soon.Hoja nzuri sana hii nami tu niseme kuwa serikali imeshindwa kuboresha sekta ya elimu baada ya kupeleka walimu wasio na uwezo katika shule za msingi na wanafunzi wengi kufeli wakabadili mfumo wa mitihani wakaleta maswali ya kuchagua mpaka hesabu sasa hapo wameboresha au wameboronga. Tena tusubiri na sekondari sasa hivi watafanya maswali ya kuchagua. Elimu ya msingi siyo msingi tena bali ni bora liende zamani darasa la saba angekuwa polisi au nesi sasa darasa la saba hajui kusoma na kuandika.
Jamani, naomba nami niongee haya machache! Shule nyingi zinazofanya vizuri ni zile za st., ambazo walimu malipo yao mazuri na zile zinazozalisha 3 & 4 na 0 ni zile za serikali na nyingi za KATA ambazo walimu malipo yao hayaendani na hali ya maisha!
serikali, kama haitawathamini walimu kila siku matokeo kwa xcul za goverment yatakuwa mabaya hadi mwisho wa dunia....Hebu, linganisha malipo ya mbunge na mwalimu, kuna uwiano?
Aikasa hayo unayosema ni kweli kabisa lakn je tutasomesha bila miundombinu mizuri na yenye tija? mathali sidhan kama kuna shue zenye archives au geography room kwa siku za leo.sioni kama mashuleni kuna library furnished, agriculture rooms hakuna, maabara za sayans zipo kwa uchache sana na vifaa hakuna vitabu hakuna hata kama utapewa mshahara milion 8 kwa mwezi utawezaje kupandisha uelewa wa wanafunzi hali vitenea kazi hakuna?serikali, kama haitawathamini walimu kila siku matokeo kwa xcul za goverment yatakuwa mabaya hadi mwisho wa dunia....Hebu, linganisha malipo ya mbunge na mwalimu, kuna uwiano?