Hebu tukumbushane kidogo kuhusu chandimu

Director Kenny

JF-Expert Member
Jan 11, 2020
347
837
BAADHI YA SHERIA ZA MPIRA WA CHANDIMU
.
1. Mchezaji mnene zaidi atakuwa Golikipa.

2. Mechi haitaanza mpaka mwenye Mpira awe amemaliza kazi za nyumbani kwao, ikitokea wachezaji wengine wanautaka Mpira huo basi sharti wamsaidie kufanya kazi zake ili ziishe mapema na mechi kuanza.

3. Viatu hutumika kuonyesha alama ya goli linapoanzia na linapoishia.

4. Ikitokea penati mchezaji ambae si Golikipa ataruhusiwa kukaa golini kisha ataendelea kucheza nafasi yake ya mwanzoni baada ya penati kupigwa.

5. Hakuna refarii, na ikitokea mchezaji kashika basi wale wababe wataamua kama ni penati au si penati.

6. Mchezaji ataweza kuingia tena kwa mara ya pili bila ya kujali kama tayari alishafanyiwa mabadiliko (substitution).

7. Ikitokea Mpira umepigwa umbali mrefu au umeingia kwenye fensi ya mtu basi wachezaji wote watapaswa kwenda kuusaka na yoyote atakayeonekana kutegea hataruhusiwa tena kucheza baada ya Mpira kupatikana.

8. Wale watakaoanza kufungwa goli watalazimika kuvua mashati yao ili kutoa tofauti baina ya timu A na timu B.

9. Mpira utaisha baada ya adhana ya Magharibi kupigwa na ikitokea mechi imenoga sana itapigwa hata kama kiza kimeingia.

10. Hakuna alama zinazoonyesha maeneo ya uwanja hivyo basi mchezaji ataruhusiwa kucheza kadri vile awezavyo hata kama ataweza kupiga chenga kwa kuzunguka magari ya watu haina shida.

11. Mchezaji ambae ni staa wa timu huvaa bandeji nyeupe mkononi au kitambaa cha usongo kwenye paji lake la uso.

12. Endapo mwenye Mpira ataitwa nyumbani kwao hapo mechi itakuwa imeisha rasmi maana ataondoka na mpira wake.

13. Hakuna mapumziko (half time) mechi itapigwa kadri ya uwezo wa wachezaji husika.

VIRTUAl%E2%9C%85%2020200403_011551.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom