Hebu tujipongeze

Hebu tujipongeze

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,419
Reaction score
18,373
Kwakuwa ni lazima tupongezane ili tuonekane wazalendo basi pongezi ziwaendee

1. Wahandisi wote wanaojenga majengo marefu ya kisasa na yakaporomoka
2. Wanasheria wote wanaotetea majambazi na wabadhilifu nchini mwetu
3. Madaktari wote mliohitimu na kupasua watu vichwa badala ya magoti
4. Wanasiasa wote ambao siasa bora kwenu ni kuona unapanda cheo kwa kuongea uongo, kutotimiza ahadi na kudharau wananchi waliokuchagua
5. Waalimu wote ambao wanafunzi wako wakifeli haikusumbui akili
6. Wakulima wote ambao mnaweka nyanya,viazi, vitunguu, nazi na machungwa yaliyooza chini na mazima mnaweka juu na kuwauzia walaji
7. Madalali wote ambao mashamba na nyumba za watu ni vitega uchumi vyenu na mko tayari mkulima au mwenyumba aingie hasara ila nyie mpate faida
8. Wanausalama wote ambao hamuwezi kutafuta wahalifu bila ya wananchi. Na wananchi wakiwaonesha mnawakaanga.
9. Wazazi wote ambao mmekabidhi watoto mashuleni na unadhani ada inaingiza akili kichwani
10. Mimi na wewe tuaiofanya kazi ila tumekalia kulalamika na kudhani kuna mtu aliletwa hapa duniani kuishi kwa niaba yetu.

Kwa hakika tumefanikisha mengi yanayohitaji pongezi. Hata sasa naangalia mashindano ya dunia ya IAAF ambapo kuna wanariadha, waogeleaji, warukaji chini, warukaji juu, watupa matufe, warusha mikuki n.k. Sisi inaonekana hatuhusiki kabisa.



Hebu tuendelee kujipongeza
 
Back
Top Bottom