Hebu tujikumbushe kuhusu mwl. Nyerere


K

kdany

Senior Member
Joined
Jul 20, 2012
Messages
150
Likes
13
Points
35
K

kdany

Senior Member
Joined Jul 20, 2012
150 13 35
Hotuba ya mwl.Nyerere march 13,1995:

Zamani tulikuwa na kitu kinaitwa miiko ya uongozi wakati wa TANU, zilikuwa zinaitwa Kanuni za TANU. Na kanuni moja ya TANU, ambayo baadaye tukarithi katika CCM au tukairithisha CCM, inasema; "Rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala sitapokea rushwa".

Usije ukadhani kwamba wakati wa awamu ya kwanza palikuwa hapana rushwa; ilikuwapo, lakini tulikuwa wakali sana. Siku za mwanzo kabisa, tulitaka watu wajue hivyo .Tulitaka watu watu wajue kwamba tutakuwa wakali sana na wala rushwa ndani ya serikali na wale wanaotoa rushwa. Mwanzo kabisa wakujitawala tulitaka kila mtu ajue. Tukapitisha sharia kwamba mtu akila rushwa, eh!

Kiongozi wetu anakula rushwa: anayetoa, aliyepokea, wazanaki wanasema manzi ga nyanza yaani, wote wanapata msukosuko.
Hatukuwa tunatania. Kwa hiyo, tukatengeneza sheria kwamba tuwafundishe watu hawa kuwa jambo hili hatulipendi. Akishakuthibiti ka mahakamani kwamba kala rushwa, akithibitika mahakamani kwamba katoa rushwa, hatukumwachia hakimu uamuzi wa adhabu.

Tukasema anakwenda ndani muda usiopungua miaka miwili atapata viboko ishirini na vinne: kumi na viwili siku anayotaka akamwonyeshe mkewe. Wengine wadogo hamjui. Tukapata habari kwamba waziri wetu wa sheria amehongwa. Hatukuwa na utani hata kidogo. Tukampata aliyemhonga. Akakiri kwamba amemhonga.

Akaingia ndani akapata vile viboko vyake. Lakini ndio siku zetu za mwanzo zile tunataka kuwaonyesha hawa wakubwa "hakuna upuuzi" hapa. Lakini kulikuwa kuna mahakimu wetu wa wakati ule, waingereza. Najua mahakimu hawapendi sheria ile hata kidogo. Kwanza, inawalazimisha adhabu. Hawapendi sheria inayowalazimu, inayowatamkia adhabu. Kwamba wao hawana hiari, wakishasema mtu amekosa, basi.

Hakuna tena kusema tumpe adhabu gani, imetumika ndani ya sheria. Hawapendi kabisa sheria hiyo. Pili, hawapendi mtu kutandikwa. Mimi sipendi, lakini nilikuwa sipendi rushwa. Nilikuwa naichukua zaidi kuliko kumtandika mtu. Rushwa ni adui wa haki mkishakuwa mna rushwa, watu masikini hawana kitu. Sheria lazima itishe wala rushwa. Kwa hiyo mimi sipendi kumtandika mtu. Lakini naichukia rushwa sana. Kwa hiyo tukapitisha sheria majaji hawa waingereza hawapendi. Nasema kwanza, hawapendi kuwawekea adhabu ambayo wao hawana hiari.

Pili ni kutandika na hawapendi kutandika. Tatu wanamheshimu sana mheshimiwa Yule alihongwa. Basi wakatafuta tafuta njia wakamwachia kwa sababu sheria na haki ni vitu viwili mbalimbali. Siyo! Nautoa mfano huo kuwaambieni tulikuwa makini kwelikweli na wakali hasa. Hatukuwa tuna utani utani juu ya mambo haya ya rushwa hatukuwa na utani na mtu. Haki hainunuliwi, thamani yake ni shilingi ngapi?

Lakini sasa tumetikiswa;Ufa mmoja mkubwa. Rushwa ya Tanzania siku hizi haina adabu Tanzania! Natembea tembea hivi, watu wananiheshimu heshimu kidogo huko nje kwa sababu tulijenga taifa hapa lenye heshima heshima hivi. Sasa kananuka. Nazungumza habari za kutokusanya kodi. Kutokusanya kodi ni sifa moja ya viserikali vya wala rushwa popote pale yake hata Italia pale. Italia, serikali iliyotoka hii ina mzigo wa madeni.

Hawatozwi kodi. Serikali ya wala rushwa popote pale wala usifikiri ni Tanzania peke yake au Kenya peke yake hata Italia pale. Italia serikali ya wala rushwa popote haitozi kodi. Serikali ya wala rushwa inatumwa na wenye mali "utalipa, uspolipa utakiona! Atacheka tu huyu. Atamwambia "unaniambia hivyo wewe; basi kesho siji!" Serikali ya wala rushwa haikusanyi kodi. Itabaki kufukuzana fukuzana na vijitu vidogo vidogo mabarabarani hivi tu basi. Hili jambo ni sheria kama ile ya kwanza niliyowaambieni kuhusu ubaguzi mkianza ubaguzi, mtaendelea moja kwa moja; hamna mahali pa kusema simama hapa. Mkisha kuwa wala rushwa mtaabudu wenye mali.

Rushwa: Sasa Tanzania inanuka kwa rushwa. Ufa mwingine tulioupata. Tunataka kiongozi anayejua hivyo ambaye atasema "rushwa kwangu ni mwiko." Mwaminifu kabisa kabisa, hawezi kugusa rushwa na wanamjua watoa rushwa: watamjua hivyo. Lakini hatutaki aishie hapo tu. Maana haitoshi wewe mwenyewe uwe mwaminifu. Mambo haya yana matatizo. Unaweza ukawa wewe mwenyewe mwaminifu kabisa lakini una shinikizo za ndugu zako, jamaa zako na marafiki zako.

Kwa hiyo, sio kwamba inatosha wewe kuwa na marafiki zako. Kwa hiyo, sio uwezo wa kuwaambia jamaa na rafiki zako kwa kauli ambayo wataiheshimu na hawatarudia tena. Unawaambia na rafiki zako kwa dhati kabisa ‛Ikulu ni mahali patakatifu. Mimi sikuchaguliwa na wananchi wa Tanzania kuja kupageuza kuwa pango la walanguzi."

Ukishakuwaambia hivyo ndugu na rafiki zako na ikajulikana hivyo, mtu wala hakusogelei. Nafsi yake haimtumi kukusogelea.
 
M

Manyerere Jackton

Verified Member
Joined
Dec 11, 2012
Messages
2,402
Likes
808
Points
280
M

Manyerere Jackton

Verified Member
Joined Dec 11, 2012
2,402 808 280
na kwa kuwa tunakaribia ukingoni kuizika Tanzania, huyu mzee mtamkumbuka sana. wale wao wanaopuuza maono yake!
 

Forum statistics

Threads 1,273,817
Members 490,485
Posts 30,492,935