Hebu mshauri..

SI unit

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
1,953
766
Pole na majukumu ndugu mwanaJF, natumaini ulitimiza wajibu wako wa kujenga taifa ipasavyo. Nimekumbuka enzi hizo ktk kupita vidato mbalimbali mpaka chuo kulikua na mitindo flanflan ya kupiga msuli (kusoma).
1. Msuli bed. Hukawii kupitiliza usingizini. Styl hii inafaa kwa masomo ya ungwini.
2. Msuli zima moto. Kusoma kufa na kupona inapokaribia mitihani/test.
3. Msuli triangle. Library [kusoma], Canteem [kula], bwenini [kulala]
4. Msuli sina ndugu. Unajisomea kivyakovyako. Possibility ya kufaulu hapa ni kubwa kwa ma'genious' tu.
5. Msuli sifa. Unabeba madesa/vitabu kibao kila mahali, ful kuuza sura..
6. Msuli kombi (O'level). Unasoma zaidi masomo ya kombi.
7. Msuli discusion. Huna tabia ya kujisomea mwenyewe. Kila group discusion wewe unavamia.
8. Msuli library. Husomei sehemu nyingine tofauti na maktaba.
9. Msuli kufwata mkumbo. Unajifanya kusomea library, ukifika unaanza kupiga magoli ya kichwa (kusinzia).
10. Msuli wa kusolve past pepa. Hii hufanyika zaidi kwa discusion
11.....
12.....n.k.
Naamin kati ya hizo styl, kuna mojawapo (au nyingine ambayo sijaitaja) uliitumia ndio maana ukafaulu.
Kama ni hivyo, ungemshauri mwanao, ndugu yako au rafiki yako atumie styl gan ili afaulu kama wewe?
....
....
SI unit
....
ALAMSIKI
 
Mimi nilikuja Msuli zima moto.... Mpaka kesho sitaacha.... It is the only way other studies are studied.....
 
zimamoto for life!

Hivi kwani kudesa sio msuli?
Si unasaidia kuklia lakini?
 
Dah mimi nilikuwa nasoma msuli sina ndugu afu zima moto..siingii darasani mpk kutangazwe test..jamaa wanashangaa huyu mshkaji anakuja kujibu nn?
 
Dah mimi nilikuwa nasoma msuli sina ndugu afu zima moto..siingii darasani mpk kutangazwe test..jamaa wanashangaa huyu mshkaji anakuja kujibu nn?

We ni mkali, genious!
 
Mimi nilikuja Msuli zima moto.... Mpaka kesho sitaacha.... It is the only way other studies are studied.....

Umechanjia kuzima moto nini. Hapo utakua unapiga makarai mwanzo mwisho..
 
Mimi nilikuja Msuli zima moto.... Mpaka kesho sitaacha.... It is the only way other studies are studied.....

huu tulikuwa tunauita msuli pepa, mtu hasomi mpaka mitihani ikaribie,, lol
 
Msuli discussion na zimamoto.. Imetosha! Kwenye discussion najua watapatikana misuli wote combined mapoint yanashushwa tu!
 
kitu cha discusion bana...
baada ya hapo napiga msuli SUNGURA...(najichimbia uwanjani alone)...
 
..
..
Teh, teh! We ni mkare. Kitu cha "chimbo", au siyo mkuu..?

sina khabari...
nameza vibaya mm...mpaka zile sehem nilizokata kwenye notes na kwenye paper naandika af nakata pia...LOL
 
Back
Top Bottom