HAZINA YA MOYO

HAZINA YA MOYO

Wilinasi Petroleum

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2016
Posts
207
Reaction score
201
HAZINA YA MOYO

Mtu huwaza na kuyasema yale yalio ujaza moyo wake. Moyo wa mtu ukijaa mambo hasi unamfanya mtu huyo awaze na kusema mambo hasi. Lakini moyo ukijaa mambo chanya unakufanya uwaze na kusema mambo chanya. Hivyo Mtu mwenye moyo wenye hazina ya mambo mabaya hutoa mawazo mabaya na kutenda matendo mabaya. Lakini mtu mwenye moyo wa hazina ya mambo mazuri hutoa mawazo mazuri na kutenda matendo mazuri. Hivyo tabia ya nje ya mtu hutegemea hazina ya mambo iliyo ndani ya moyo wake.

Hata ktk hisia za mwili, moyo ulio jaa hisia hasi unamfanya mtu huyo kuwa na hisia hasi za mwili wake. Lakini moyo ulio jaa hisia chanya unamfanya mtu huyo atoe hisia chanya ktk mwili wake. Hisia chanya ni hisia nzuri ambazo hazileti matatizo ktk, mwili.

Hisia ni mihemuko ambayo inatokea moyoni na kwenye nafsi ya mwanadamu na kuuathiri mwili kupitia ubongo. Athari za hisia katika mwili zaweza kuwa hasi au chanya. Athari chanya zina ufaidisha mwili wako lakini athari hasi zinaleta madhara katika mwili. Mfano wa hisia zinazoweza kuwepo moyoni mwa mtu ni pendo, hamu, furaha, chuki, woga nk. Katika hisia hizi zipo zingine ambazo ni hasi na zingine ni chanya kwa kadri ambavyo zitakuletea faida au hasara katika mwili wako.

Hivyo basi ni jambo zuri tuwekeze mambo mazuri ndani ya mioyo yetu. Yale mambo tunayo sikiliza na kuyaona kila wakati ndio ambayo moyo huyahifadhi. Mtu anaye jijengea tabia ya kusikiliza na kuyatazama kila wakati mambo yaliyojaa maarifa ya maadili mazuri hujiwekea hazina ya mambo mazuri ndani ya moyo wake. Na yule anaye sikiliza na kuyatazama mambo yaliyo jaa maarifa ya maadili mabaya, yeye huyo hujiwekea hazina mbaya ndani ya moyo wake.

Tujitahidi kujiwekea hazina nzuri ndani ya mioyo yetu, ili tujazwe na mawazo yenye hekima.

Imeandaliwa na Mwinjilisti kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
 
Wasipokuelewa basi ujue ni ujeuri wa kimakusudi tu
 
Back
Top Bottom