Hazard: Tofauti ya Antonio Conte and Jose Mourinho

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
33,064
40,311
615844746.jpg


Hazard ameweka wazi utofauti mkubwa wa namna ya ufundishaji wa soka kati ya makocha hawa wawili.
Mafunzo ya kocha mpya Conte yanaeleweka zaidi kuliko ya kocha wake aliyetangulia Mourinho. Tunajifunza zaidi kwenye ufundi (tactics) na uwe wapi kwa wakati gani (positions) tukiwa na Conte tunajua kabisa nini cha kufanya tukiwa uwanjani.

Kwa Mourinho yeye alitufundisha mfumo wa uchezaji lakini hatukufanyika kazi kwa ndani kujua nani awe wapi na kwa wakati upi. Tulijua hivyo sababu sisi ni wachezaji lakini kulihitajika kitu zaidi yaani (automatisms).

Kwa mfano mfumo wa Mourinho, Nemanja Matic alicheza nyuma yangu kwa msimu wote tuliochukua kombe, na kuna muda mimi nilibakia mbele tu na Matic alifanya kazi yote wakati kwa Conte ni tofauti, nakuwa ndani zaidi sababu Marcos Alonso anacheza kama winger beki, mimi natakiwa kuwa pale tayari kwa shambulizi lolote la ghafla litakalotokea.

Wakati huo huo kuelekea mchezo kati ya Chelsea na Arsenal Hazard ametoboa siri kwamba yeye akicheza kushoto anakuwa hana madhara makubwa sababu hawezi ku- dribble mpira na kuingia ndani na kama akifanya hivyo pia hawezi kupiga cross na hata kama akipiga cross inakuwa dhaifu haina madhara makubwa.

Kwa hiyo yeye akicheza winger ya kushoto mara nyingi akipata mpira atatoa pasi na hivyo huwa hana madhara kwa timu pinzani tofauti na kama anavyopangwa kulia, maana yeye anatumia mguu wa kulia zaidi na akiwa winger ya kulia huwa ni hatari mno.


Mimi naona Conte ni kocha anayefundisha mpira kwa undani, hana makuu hana majigambo. Pia anajua kutengeneza wachezaji kuwaweka kwenye ubora wao; Kwa Conte sidhani kama Progba angelikuwa kwenye kiwango hicho. Angalia Progba alivyokuwa Juve chini ya Conte na Progba aliye Man United chini ya Mourinho.
 
Kweli kabisa. Conte yupo karibu zaidi na wachezaji na anajua namna ya kuwajenga kisaiklojia kuliko morinho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom