Hayati John Magufuli aliwezaje?

You nailed it " !!! Obviously alikuwa na mapungufu yake kama binaadamu lakini katika ufisadi hakuwa fisadi !!
Kwanini alimpa Mwanyika ubunge mtu ambaye alitangaza hadharani ni fisadi aliyetuletea hasara ya Trillion 400+??

Mtuambie kwanni hakuna mwizi wa Escrow aliyefungwa mpaka Leo hii??

Vipi wezi wa makinikia na Tanzanite??

Anyway alijenga ukuta ila wizi ukaongezeka maradufu!!! Kuna aliyewahi kamatwa mpaka leo??

Mie sionagi mnachomkuzia nacho JPM zaidi ya kwamba alikua mtu wa chuki tu kwa watu waliomzidi mafanikio. Ila kma kweli alipinga ufisadi Sabaya kivipi alibaki uraiani?
 
Wenye hilo jukumu la kutoa ufisadi ni chadema ila ccm hawawezi kwa sababu wananufaika.

Hata wewe hapo nikikwambia taja ufisadi wa JK hakuna unapoweza thibitisha.

Viongozi hawafanyi ufisadi moja kwa moja bali hupitia watu wengine kwa kuninglience matakwa yao.Kwa mfano Mwendazake alikuwa anapewa tenda za bure za ujenzi kupitia kampuni ya Mayanga.

Mwendazake alipewa tenda ya kuweka vinasaba kwenye mafuta kupitia kampuni ambayo ilifutwa na Samia na hiyo Kazi kupewa TBS.

Hiyo ni kifano michache tuu hapo hujagusia madini na wateule wake kule bandari,Tanroads,Bwawa la Nyerere,ndege nk.

Ndio maana hatukonyeshwa hekalu lake kule nyumbani kwake ambalo ni kufuru kuzidi hata la Msoga.

Ila wajinga kama wewe au mnaojaribu kuwafool wajinga mnatumia nguvu Sana kumpamba.

Mzalendo wa kweli Tzn hii alikuwa Nyerere tuu hana kashfa zozote za wizi.
Hekalu unalosemea ndio Ile nyumba mama Janeth aliyokua anacheza wimbo wa harmonize?
 
Magufuli alikuwa na hofu ya Mungu.

Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa (Mithali 1:7).

No wonder alifanya makubwa yote yale.
Hofu ya Mungu afu uibe kura? Utembee na mke wa mtu?? Hofu ya Mungu ufananishwe na Yesu afu unacheka Cheka tu?? Yule alikua mpagani tu na sasa yupo kuzimu anateseka tu Hana ucha Mungu wowote!!!
 
Hamna kitu alikua mkali kwa watendaji ila sio wanasiasa wenzake!! Jiulize Nchambi ni jangili mbona hakuwekwa ndani.

Jiulize makonda na Sabaya kivipi uhuni wote ule waliofanya hawakuguswa?

Vipi Mafisadi wa ESCROW kupitia Stanbic mbona hawakufungwa?

Ripoti ya Tanzanite na Makinikia ilitaja wanaCCM zaidi ya 20 mbona hawakuwekwa ndani ila Cha kushangaza Lissu ndio akageuzwa adui kwenye madini???

Unamjua Mwanyika? Ilikuaje mtu aloyetusababishia hasara ya trillion 400 akapewa ubunge na JPM tena akaitwa mzalendo kwenye campaign??


JPM is overrated otherwise Wana CCM wote wangekua Gerezani
Embu nikumbishe vizuri akina Seth na Rugemalila walifikishwa mahakamani kipindi kipi?
Hata Kama unamchukia JPM lakini haziwezi kuondoka ukweli kwamba ndio raisi pekee aliekua na uthubutu.
 
Hofu ya Mungu afu uibe kura? Utembee na mke wa mtu?? Hofu ya Mungu ufananishwe na Yesu afu unacheka Cheka tu?? Yule alikua mpagani tu na sasa yupo kuzimu anateseka tu Hana ucha Mungu wowote!!!
Pole sana.

Go see a psychologist.
 
Embu nikumbishe vizuri akina Seth na Rugemalila walifikishwa mahakamani kipindi kipi?
Hata Kama unamchukia JPM lakini haziwezi kuondoka ukweli kwamba ndio raisi pekee aliekua na uthubutu.
Waliofikishwa but hawakukutwa na hatia so wats that?

Kingine pesa zililiwa na Wana CCM wengi kuanzia Katibu wa Rais hadi wabunge mbona cjaona mwana CCM aliyekamatwa??

Uthubutu huku unaogopa Wana CCM haina maana yeyote. No wonder nchambi na mwanyika wako mtaani hadi Leo!!
 
Kwa watoto wadogo na wasiojua mambo wanadhani hayati Magufuli alianza kuwa mkali alipokuwa rais wa nchi tu wakati ukweli ni kwamba Magufuli alikuwa mkali na mfuatiliaji tangu akiwa naibu waziri, waziri na baadae rais wa nchi.

Katikati ya mafisadi wakubwa wa awamu za Mkapa na Kikwete lakini walimwogopa Magufuli na aliwashughulikia kila wizara aliyopelekwa, kwa waliokuwepo kwenye wizara ya uvuvi, aridhi na ujenzi enzi za waziri Magufuli watakwambia moto wake.

Swali la kujiuliza aliwezaje kutekeleza bila kutumbuliwa? Je kwenye baraza la mawaziri la sasa kuna waziri anayevaa viatu vyake?
Hata baada ya kuwa rais na kufariki dunia mpaka leo mwaka umeisha si Chadema , ACT Wazalendo wala CCM waliokuja na ushahidi usiotia shaka juu ya ufisadi wake licha ya kwamba waliahidi pindi tu atakapotoka madarakani basi watakuja na mikataba ya ufisadi na rushwa kubwakubwa zilizosainiwa na yeye.

Mwezi march 2022 umetimia mwaka mzima tangu atutoke duniani lakini mahasimu wake ikiwemo ,Lisu, Lema , Nape ,Makamba, Kigogo bado hawajawaletea watanzania ufisadi wa Magufuli.

kinyume chake wanaendeleza mafanikio na miradi ya awamu ya tano kwa kasi kubwa, walipinga kila kitu lakini sasa wanatumia kila kitu walichokipinga! Mbowe akimaliza kutukana anakimbilia kupanda ndege mpya ya Dreamliner impeleke KIA.

Walioahidi kuifunika legacy kumbe hawana uwezo kuifunika hata kidole chake tu!!

Muda utawaumbua zaidi.
JPM alivurunda vibaya mno ni siasa na ubabe tu vinamlinda ila hakuna kitu pale.
 
Pole sana.

Go see a psychologist.
I need no psychologist, what we object is y'all exaggerating matters about JPM. He was just a random. CCM hooligan; no wonder things are unfolding now on how Incompetent he was, ranging from diplomacy, management, to economics.
 
Hekalu unalosemea ndio Ile nyumba mama Janeth aliyokua anacheza wimbo wa harmonize?
Nasema hivi , Mwendazake alijenga jumba lake la kifahari kama Ikulu kwa Kodi yetu.

Kaweka wanyama humo,mahoteli na anasa nyingine kibao,mimi sio mjinga kama wewe napafahamu hapo vizuri.
 
Hakuna siku ufisadi ukiwahi kuisha ila wa awamu ya JK na hii ya mama ni kiboko

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
Nyie si mlitaka kuifunga mahakama ya mafisadi eti haina kesi tena baada ya majizi yote kudhibitiwa😂😂😂!!

Anyway hao wote ni CCM so bora umekiri kuwa hamna viongozi wazuri!!

Mara ooh system inaandaa Rais.... Cjui wazalendo hawakubali fisadi aingie ikulu!!! Sasa imekuaje system ikamuweka Samia?? Au nap hawana akili tofauti na mlivyokua mnawakuza!!!

Funny
 
Sasa huu ndiyo ushahidi?

Hivi hata mimi naweza kumtuhumu mtu yeyote kwa kutaja tu tuhuma bila vielelezo.

Nilifikiri wewe great thinker unajuwa jinsi wenzio wanavyoweka ushahidi usio acha shaka.

Zipo tuhuma humu wenzio waliweka enzi za JK kila mtu alikubaliana nazo. Fuatilia kesi ya Maxence Melo alivyo lazimishwa atoe utambulisho wa hao wafichua ufisadi.

Zisome hizo thread zilizoleta shida utajua unadaiwa nini kwenye tuhuma ulizotoa.
Huyu uliyemjibu ni nyumba ndogo ya mzee wa msoga ,mpuuze.
 
Back
Top Bottom