Hayati John Magufuli aliwezaje?

Hayati John Magufuli aliwezaje?

Kiturilo

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
706
Reaction score
2,859
Kwa watoto wadogo na wasiojua mambo wanadhani hayati Magufuli alianza kuwa mkali alipokuwa rais wa nchi tu wakati ukweli ni kwamba Magufuli alikuwa mkali na mfuatiliaji tangu akiwa naibu waziri, waziri na baadae rais wa nchi.

Katikati ya mafisadi wakubwa wa awamu za Mkapa na Kikwete lakini walimwogopa Magufuli na aliwashughulikia kila wizara aliyopelekwa, kwa waliokuwepo kwenye wizara ya uvuvi, aridhi na ujenzi enzi za waziri Magufuli watakwambia moto wake.

Swali la kujiuliza aliwezaje kutekeleza bila kutumbuliwa? Je kwenye baraza la mawaziri la sasa kuna waziri anayevaa viatu vyake?
Hata baada ya kuwa rais na kufariki dunia mpaka leo mwaka umeisha si Chadema , ACT Wazalendo wala CCM waliokuja na ushahidi usiotia shaka juu ya ufisadi wake licha ya kwamba waliahidi pindi tu atakapotoka madarakani basi watakuja na mikataba ya ufisadi na rushwa kubwakubwa zilizosainiwa na yeye.

Mwezi march 2022 umetimia mwaka mzima tangu atutoke duniani lakini mahasimu wake ikiwemo ,Lisu, Lema , Nape ,Makamba, Kigogo bado hawajawaletea watanzania ufisadi wa Magufuli.

kinyume chake wanaendeleza mafanikio na miradi ya awamu ya tano kwa kasi kubwa, walipinga kila kitu lakini sasa wanatumia kila kitu walichokipinga! Mbowe akimaliza kutukana anakimbilia kupanda ndege mpya ya Dreamliner impeleke KIA.

Walioahidi kuifunika legacy kumbe hawana uwezo kuifunika hata kidole chake tu!!

Muda utawaumbua zaidi.
 
Wenye hilo jukumu la kutoa ufisadi ni chadema ila ccm hawawezi kwa sababu wananufaika.

Hata wewe hapo nikikwambia taja ufisadi wa JK hakuna unapoweza thibitisha.

Viongozi hawafanyi ufisadi moja kwa moja bali hupitia watu wengine kwa kuninglience matakwa yao.Kwa mfano Mwendazake alikuwa anapewa tenda za bure za ujenzi kupitia kampuni ya Mayanga.

Mwendazake alipewa tenda ya kuweka vinasaba kwenye mafuta kupitia kampuni ambayo ilifutwa na Samia na hiyo Kazi kupewa TBS.

Hiyo ni kifano michache tuu hapo hujagusia madini na wateule wake kule bandari,Tanroads,Bwawa la Nyerere,ndege nk.

Ndio maana hatukonyeshwa hekalu lake kule nyumbani kwake ambalo ni kufuru kuzidi hata la Msoga.

Ila wajinga kama wewe au mnaojaribu kuwafool wajinga mnatumia nguvu Sana kumpamba.

Mzalendo wa kweli Tzn hii alikuwa Nyerere tuu hana kashfa zozote za wizi.
 
Magu alitumia kikosi kazi haramu kukandamiza.

Kikosi kazi kikiumbuliwa, kunahatari hats ya kuiharibu CCM yenyewe. Hivyo wale wanachama wa CCM nivigumu kumuumbua Mama CCM bado inakula mali za wizi wa nchi.

Kuhusu waoinzani, hawana access serikalini hivyo ni ngumu, kikosi kazi bado kipo kazini
 
Kwa watoto wadogo na wasiojua mambo wanadhani hayati Magufuli alianza kuwa mkali alipokuwa rais wa nchi tu wakati ukweli ni kwamba Magufuli alikuwa mkali na mfuatiliaji tangu akiwa naibu waziri, waziri na baadae rais wa nchi.
Hamna kitu alikua mkali kwa watendaji ila sio wanasiasa wenzake!! Jiulize Nchambi ni jangili mbona hakuwekwa ndani.

Jiulize makonda na Sabaya kivipi uhuni wote ule waliofanya hawakuguswa?

Vipi Mafisadi wa ESCROW kupitia Stanbic mbona hawakufungwa?

Ripoti ya Tanzanite na Makinikia ilitaja wanaCCM zaidi ya 20 mbona hawakuwekwa ndani ila Cha kushangaza Lissu ndio akageuzwa adui kwenye madini???

Unamjua Mwanyika? Ilikuaje mtu aloyetusababishia hasara ya trillion 400 akapewa ubunge na JPM tena akaitwa mzalendo kwenye campaign??

JPM is overrated otherwise Wana CCM wote wangekua Gerezani
 
Kwa watoto wadogo na wasiojua mambo wanadhani hayati Magufuli alianza kuwa mkali alipokuwa rais wa nchi tu wakati ukweli ni kwamba Magufuli alikuwa mkali na mfuatiliaji tangu akiwa naibu waziri, waziri na baadae rais wa nchi.

Katikati ya mafisadi wakubwa wa awamu za Mkapa na Kikwete lakini walimwogopa Magufuli na aliwashughulikia kila wizara aliyopelekwa, kwa waliokuwepo kwenye wizara ya uvuvi, aridhi na ujenzi enzi za waziri Magufuli watakwambia moto wake.

swali la kujiuliza aliwezaje?? Je kwenye baraza la mawaziri la sasa kuna waziri anayevaa viatu vyake?
Hata baada ya kuwa rais na kufariki dunia mpaka leo mwaka umeisha si Chadema , ACT Wazalendo wala CCM waliokuja na ushahidi usiotia shaka juu ya ufisadi wake licha ya kwamba waliahidi pindi tu atakapotoka madarakani basi watakuja na mikataba ya ufisadi na rushwa kubwakubwa zilizosainiwa na yeye.

Mwezi march 2022 umetimia mwaka mzima tangu atutoke duniani lakini mahasimu wake ikiwemo ,Lisu, Lema , Nape ,Makamba, Kigogo bado hawajawaletea watanzania ufisadi wa Magufuli.
kinyume chake wanaendeleza mafanikio na miradi ya awamu ya tano kwa kasi kubwa, walipinga kila kitu lakini sasa wanatumia kila kitu walichokipinga!
Walioahidi kuifunika legacy kumbe hawana uwezo kuifunika hata kidole chake tu!!

Muda utawaumbua zaidi.
Vp zile nyumba alizohonga vimada wake na mdogo wake aliyekuwa mwanafunzi?

Huyu mungu wenu mwacheni aongoze malaika siyo kila siku kumwanzishia uzi mpya.

Anateseka eti huko aliko
 
Magufuli alikuwa na hofu ya Mungu.

Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa (Mithali 1:7).

No wonder alifanya makubwa yote yale.
 
Kwa watoto wadogo na wasiojua mambo wanadhani hayati Magufuli alianza kuwa mkali alipokuwa rais wa nchi tu wakati ukweli ni kwamba Magufuli alikuwa mkali na mfuatiliaji tangu akiwa naibu waziri, waziri na baadae rais wa nchi.

Katikati ya mafisadi wakubwa wa awamu za Mkapa na Kikwete lakini walimwogopa Magufuli na aliwashughulikia kila wizara aliyopelekwa, kwa waliokuwepo kwenye wizara ya uvuvi, aridhi na ujenzi enzi za waziri Magufuli watakwambia moto wake.

swali la kujiuliza aliwezaje?? Je kwenye baraza la mawaziri la sasa kuna waziri anayevaa viatu vyake?
Hata baada ya kuwa rais na kufariki dunia mpaka leo mwaka umeisha si Chadema , ACT Wazalendo wala CCM waliokuja na ushahidi usiotia shaka juu ya ufisadi wake licha ya kwamba waliahidi pindi tu atakapotoka madarakani basi watakuja na mikataba ya ufisadi na rushwa kubwakubwa zilizosainiwa na yeye.

Mwezi march 2022 umetimia mwaka mzima tangu atutoke duniani lakini mahasimu wake ikiwemo ,Lisu, Lema , Nape ,Makamba, Kigogo bado hawajawaletea watanzania ufisadi wa Magufuli.
kinyume chake wanaendeleza mafanikio na miradi ya awamu ya tano kwa kasi kubwa, walipinga kila kitu lakini sasa wanatumia kila kitu walichokipinga!
Walioahidi kuifunika legacy kumbe hawana uwezo kuifunika hata kidole chake tu!!

Muda utawaumbua zaidi.
You nailed it " !!! Obviously alikuwa na mapungufu yake kama binaadamu lakini katika ufisadi hakuwa fisadi !!
 
Wenye hilo jukumu la kutoa ufisadi ni chadema ila ccm hawawezi kwa sababu wananufaika.

Hata wewe hapo nikikwambia taja ufisadi wa JK hakuna unapoweza thibitisha.

Viongozi hawafanyi ufisadi moja kwa moja bali hupitia watu wengine kwa kuninglience matakwa yao.Kwa mfano Mwendazake alikuwa anapewa tenda za bure za ujenzi kupitia kampuni ya Mayanga.

Mwendazake alipewa tenda ya kuweka vinasaba kwenye mafuta kupitia kampuni ambayo ilifutwa na Samia na hiyo Kazi kupewa TBS.

Hiyo ni kifano michache tuu hapo hujagusia madini na wateule wake kule bandari,Tanroads,Bwawa la Nyerere,ndege nk.

Ndio maana hatukonyeshwa hekalu lake kule nyumbani kwake ambalo ni kufuru kuzidi hata la Msoga.

Ila wajinga kama wewe au mnaojaribu kuwafool wajinga mnatumia nguvu Sana kumpamba.

Mzalendo wa kweli Tzn hii alikuwa Nyerere tuu hana kashfa zozote za wizi.
Sasa huu ndiyo ushahidi?

Hivi hata mimi naweza kumtuhumu mtu yeyote kwa kutaja tu tuhuma bila vielelezo.

Nilifikiri wewe great thinker unajuwa jinsi wenzio wanavyoweka ushahidi usio acha shaka.

Zipo tuhuma humu wenzio waliweka enzi za JK kila mtu alikubaliana nazo. Fuatilia kesi ya Maxence Melo alivyo lazimishwa atoe utambulisho wa hao wafichua ufisadi.

Zisome hizo thread zilizoleta shida utajua unadaiwa nini kwenye tuhuma ulizotoa.
 
Ushahidi usiowacha shaka ni unatafsiriwa mahakamani,hapa tunaweka msingi wa tuhuma.

Mtuhumiwa answeza Kuni sue kotini kama anaona nimemchafua then huko ndipo naweza thibitisha zaidi.

By the way matumizi mabaya ya madaraka ni ufisadi tosha..
 
unakuwa mkali kiasi cha kushindwa kumfanya chochote Sabaya, Makonda, Chambi,Kakoko? Huu ukali wa dizaini gani
 
Magufuli angekuwa mwadilifu na mchukia ufisadi, alipoingia Ikulu angeshughulikia suala la ESCROW bila kusita....kulikuwa na maagizo/maelekezo ya bunge! Hivi ni nani yule aliyekabidhi kile kivuko jeshini ili ufisadi uliokihusu usiongelewe?!
Ukali ili kuficha na kuyalinda maovu ya ccm hauifai nchi hii.
 
Back
Top Bottom