Zero Hours
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 12,943
- 18,665
Ni ukweli usiopingika kuwa sasa Watanzania tumepuuza mafunzo tulioachiwa na Hyati Baba Wa Taifa, Julius Kambalage Nyerere. Hya yote yanayotutokea sasa ni kwasababu tumepuuza wosia wake na tumejiona tunaweza kufanya tutakavyo kuanzia viongozi hadi Wananchi wake.
Tunatengeneza Taifa la vijana Wanafiki na Waoga. Tunavyozidi kuwa waoga ndivyo tunazidi kuwapa viongozi kiburi cha kuwajibisha wale wanao simamia ukweli na kuhoji.
Huwa nawaeleza watu kuwa wanakosea sana wanaposema kuwa serkali ya kikwete ndyo iliongoza kwa ufisadi kila kona. Serkali ya kikwete mpaka sasa ni serkal pekee iliyotengenezea mazingira ya wananchi wake kuhoji. Ndyo maana tukajua madudu yote yaliyotokea hata kwenye serkali ya Mkapa. Watanzania tusipokuwa makini tutarudishwa kulekule. Yani tutaibiwa huku tunaona na tutaogapa kuhoji.
Ni aibu kuona kuwa kazi ya kukosa serkali ni kazi ya vyama vya upinzani Tu. Ndyo maana siku hizi mtu akikosoa serkali kama ni mwana CCM anaitwa Msaliti.
Watanzania kumbukeni hii ni nchi yetu wote. Hii nchi sio ya Magufuli wala Bashite. Ni jukumu letu kukosoa pale wanapokosea. Maana makosa wafanyayo yanatuumiza sisi sio wao. Wao hawajui hata bei ya unga sokoni inauzwaje. Wanaletewa tu wanakuta chakula mezani kwa kodi zetu.