Area 56
JF-Expert Member
- Dec 8, 2015
- 1,546
- 4,040
Haya yanayoendelea nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ni legacy ya mwendazake Magufuli.
Huko chamani Rais Samia amejipitisha bila kupingwa kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wote tunajua muasisi wa mchezo wa kupita bila kupingwa ni John Magufuli.
Kesi za jinai kwa wapinzania hasa kesi ya Uhaini aliyopewa Tundu Lissu ni matokeo ya mifumo ya uonevu aliyoianzisha John Pombe na Samia ameamua kuiendeleza, maana yake legacy inaishi. Wote mnakumbuka jinsi akina Kabendera, Rugemalira na wengineo waalivyopewa kesi za uhujumu uchumi.
Akina Soka na wenzake kupotea, kuuwawa kwa Mzee Ali Kibao
Hali inayoendelea nchini ni muendelezo wa legacy ya John Pombe, yaani tupo kwenye Umagufuli bila Magufuli mwenyewe.
Itachukua miaka mingi sana kurudi tulipokuwepo wakati wa awamu ya nne na kurudi nyuma.