Haya yanawezekana vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya yanawezekana vipi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Raia Fulani, Jun 21, 2010.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ukitaka kujua tofauti ya kimitazamo hasa kuhusu siasa na uendeshaji wa serikali yetu basi tazama bunge. Bado bajeti za mawizara zinaendelea kujadiliwa huko. Juzi msemaji wa kambi ya upinzani anasoma hotuba yake pale, unaona kabisa kuna mapungufu ya dhahiri, na hasa walipokuwa wakiijadili wizara ya utumishi. Halima Mdee alisimama na kuzungumza kwa kujiamini na takwimu sahihi kabisa na unaona kuna mapungufu. Tatizo wakisimama watu wa chama inakuwa ni kinyume kabisa. wanatetea madudu yanayofanywa katika wizara ya utumishi pamoja na wizara zingine.

  Nauliza. inakuwaje mtu anaona hapa pana kosa kabisa na bado anatetea? kuna faida gani ya kuupinga ukweli wa mwenzako? hawa watu wanadhani sisi tunajisikiaje? ukweli ni kwamba taarifa kuhusu nchi hii za kimaendeleo na za kishenzi wanazo wananchi wachache sana. Mtaji wa chama tawala ni umasikini wa wengi (watanzania) ili siku wakienda kupuliza maumivu, mwenye kidonda anaona nafuu. ndivyo mambo yanavyoelekea kufanyika hasa kipindi hiki cha uchaguzi mkuu. nchi zilizoendelea huwezi kumdanganya mwananchi kwa maji au barabara. hivyo vipo. mtazamo wangu ni kuwa, mapinduzi ya kiitikadi (sera za ccm) yatatokea endapo asilimia 90 ya watanzania watakuwa na taarifa muhimu kuhusu nchi yao na yale yanayotendeka. ama mapinduzi yatakuja kwa njia ya ghasia na fujo. binafsi sipendi hata kumtazama rais akiongea, anavyonyenyekewa, n.k kwani anajua fika kuwa hastahili hayo. yeye ndiye anayesababisha hata wabunge kuongopea bungeni na kupinga hoja za kweli na kutetea unafiki. nsio maana nasema kuwa umasikini na taarifa haba na zisizo sahihi ndio mtaji wa ccm
   
Loading...