Haya yanatuangusha Chadema

Haya yanatuangusha Chadema

Yafutayo yanatuangusha chadema :-

1.ofisi za uhakika (makao makuu )
2.Gazeti huru la chama
3.Radio huru ya chama
4.Tv huru ya chama
5.Malipo kwa watendaje wake
6.vitendea kazi kama magari, pikipiki,vipeperushi,nk kuwafikia wapiga kura
7.Takwimu sahihi za wanachama
8.vitega uchumi vingine

mytake

kama viongozi wetu wa chama wataendelea kuona kama chama chetu ni cha mpito watapuuza haya. Wajijenge zaidi kuiandaa chadema kwa uzao ujao na kama chama kikubwa kilichomkomboa mtanzania kutoka kwa watanzania wachache waliojilimbikizia mali na tamaa ya madaraka na uhujumu uchumi.

viongozi wetu wa chama wasifanye chadema kama chama mkombozi wa taifa kwa kipindi tu wao walichokuwepo madarakani bali wajikite kwenye future ya chama na kuwa chadema si ya leo tu bali chadema ni ya leo na miaka ijayo kwa kuiandalia asset, resources, vitendea kazi na vitega uchumi vya kutosha

viongozi wetu waifanye chadema kama ni ya watanzania na ya uzao ujao wa watanzania na kuuandalia msingi mzuri uzao ujao utakaokuja kuiongoza chadema muda huo.Wakifanya hayo kamwe historia ya ukombozi wa taifa hili haiwezi kuwakwepa na hasa historia ya chama

kila la heri chadema
haya hatujaanza kuyasema leo lakini viongozi wetu wametia pamba masikiono . Tungekuwa hata na redio ingetosha kuweka kipindi cha kuelimisha wananchi kuhusu sera za chama hata haya tunayolalamika kuwa viongozi wameshindwa kupeleka sera vijijini lisingekuwepo maana wanakijiji wangesikia sera kupitia redio ya chama
Zamani akina j mnyika walikuwa wanapita hapa jf na kujibu baadhi ya hoja siku hizi wameridhika hawajali tena sisi ni sawa na kelele za mlango hazimyimi mwenyenyumba usingizi.
 
thinking very carefully.
SIUNGI MKONO
RADIO NA TV kwa chama chochote nchini.
kwa mazingira ya kidemokrasia NI ISHARA MBAYA SANA.
1.tutakosa balance ya habari.
2.kwa sasa tunataka kuongeza wafuasi,wale ambao ni ccm na vyama vingine tunawahitaji ila hawawezi kabisa kuangalia tv yetu wakiwa tayari wanatuchukia kama chadema wengi tulivyoacha kuangalia taarifa za habari TBC kwa sababu ni chombo kinachoegemea upande mmoja.
3.kikubwa ni kupigania uhuru wa vyombo vya habari ili viwe huru na viwe na balance ya habari,LEO hii MWANANCHI&ITV vimeunganisha watanzania wote na habari zote zinasomwa&kutazamwa na watu wa pande zote na hata mimi nasoma habari za CCM ila habari za ccm UHURU siwezi kusoma.
NIAMBIENI CCM mpaka sasa wamefaidikaje na gazeti LA UHURU,haliuziki hata kama limeandika ukweli,na limekuwa mzigo kwa kuingizia CCM hasara badala ya faida na hata wana ccm wenyewe ni wachache wanaolinunua mana hakuna uhakika wa kukuta habari zote ktk mitazamo yote ya hasi na chanya
4.TUNAHITAJI PIA KUKOSOLEWA
 
Nashukuru kwa mawazo na uzi huu, mie nadhani chama si viongozi ni sisi wenyewe, Nadhani tuweke kwenye mipango yetu ya muda mfupi, mrefu, na muda wa kati. Kwa kweli naanimini viongozi wetu naamininni wasikivu waelewa na wako tayari kwa mageuzi. Mie naamini tuanzishe mfuko rasmi ambao tutachangia wenyewe na kisha tuwaachie majukumuviongozi wetu na wao walichukue wazo hili na kuliweka kwenye mkakati kiasi wanapokutana na marafiki zetu wa ndani na nje ya nchi basi wafikishe maombi ya chama chetu kwa ajili ya kuwafikia wananchi wengi na hasa wa vijijini kuwaeleza sera, mikakati na mipango ya baadaye ya kuwakomboa kutoka kwenye minyonyororo ya Mafisadi. Hata wakati wa Ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika Nyerere alitumia Radio Tanzania wakati huo na ndio msingi wa kuwepo kituo kilichojulikana kama external service of Radio Tanzania DSM.
Nawasilisha,
 
Pamoja na wanachi wengi kukipenda CDM bado wengine tunaona kuna mapungufu ambayo yanaweza kuboreshwa zaidi kabla ya 2015. Mfano msisitizo wa kuwa na mising mingi iwezekanavyo nchi nzima.
Sioni sababu viongozi wa kitaifa kwenye mikutano yao mingi wanakikandia chama tawala tunataka watupe mbinu za kufungua matawi na mising kila mahali na jinsi ya kuelezea sera za chama kwa wananchi. Msisitizo wa vikao ngazi zote hasa wakati wa kipindi hiki cha uchaguzi. Mimi nasema hivyo kwa sababu sisikii yakisisitizwa na viongozi wakuu na huku tuliko tuna shauku lakini hatuna uongozi unaoelekea kutuweka sawa kupambana na chama tawala.

Nina imani kuna namna ya kupenyeza sera za chama kutoka juu hadi chini bila kuptia vikao vya hadhara! Wakati ni sasa.
Big up mleta uzi.
 
Kama hayo yasemwayo kweli, basi yote dugu moja hakuna mkombozi wa kweli

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
haya hatujaanza kuyasema leo lakini viongozi wetu wametia pamba masikiono . Tungekuwa hata na redio ingetosha kuweka kipindi cha kuelimisha wananchi kuhusu sera za chama hata haya tunayolalamika kuwa viongozi wameshindwa kupeleka sera vijijini lisingekuwepo maana wanakijiji wangesikia sera kupitia redio ya chama
Zamani akina j mnyika walikuwa wanapita hapa jf na kujibu baadhi ya hoja siku hizi wameridhika hawajali tena sisi ni sawa na kelele za mlango hazimyimi mwenyenyumba usingizi.

Mnyika siku hizi anajibu hoja za Ridhiwani. Hana time na vidampa. Ndio maana hakujibu hoja za elimu yake mpaka alipoulizwa na Ridhiwani.
 
Isaac JK

Asante sana kwa ushauri wako wenye nia njema ya kujenga na kuimarisha harakati za mapambano ya ukombozi wa pili wa Mtanzania kutoka kwenye makucha ya mkoloni 'mjomba, shangazi, kaka, dada, rafiki, bibi, babu, mama, baba', walioko kwenye mwamvuli wa CCM!

Mtu akipitia andiko lako kwa umakini atabaini kuwa vitu ulivyoviandika viko very vague. Haijulikani hasa unataka kusema au kushauri nini. Mathalani vitu vyooooooooote ulivyoorodhesha hujasema vinawaangusha namna gani CHADEMA na namna gani ushauri wako ufanyiwe kazi. Lakini si mbaya, tutakujibu kwa mantiki hiyo hiyo iliyoeleweka kwenye ujumbe.

Lakini pia labda ni tabia yetu Watz kutopenda kutafuta taarifa kwanza kabla ya kusema, masuala ya media za CHADEMA, mfano tv, redio na gazeti, yameshajibiwa hapa mara kadhaa. Kuna masuala na hatua kadhaa za kupitia. Imeshaelezwa hapa, siku moja hadi nikaenda mbali nikasema watu wengine wanashangaza wanataka tuje tujadili mpango kazi na mkakati wa wa chama kwenye vyombo vya habari, kwa faida ya nani?

Takwimu sahihi za wanachama zimekuwaje? Malipo kwa watendaji wake yamekuwaje? Vitendea kazi kama magari, pikipiki, vipeperushi, vimekuwaje? Vitega uchumi vingine, vimekuwaje? Very vague, utaishia kupata majibu vague vile vile.

Chama cha mpito! Sikuwahi kufikiria mwanaCHADEMA makini anaweza hata kuwaza eti chama hiki ambacho kimeweza kuiweka kwenye kona CCM na serikali yake, kikiendesha harakati za ukombozi wa kifikra kwa miaka zaidi ya 20 mfululizo, kinaweza kuwa chama cha mpito.

Chama cha namna hiyo kinaweza kuwa CHADEMA kweli? Vyama vya mpito vingi tu tunavyoviona kwa matendo na maneno, bungeni, na nje kwenye mikutano ya hadhara na press conference, vikifanya kazi ya CCM...

Pasi na shaka, viongozi wa CHADEMA pamoja na wanachama wake makini, wanaotambua wajibu wao, wameendelea kukijenga chama hiki kwa ajili ya vizazi vilivyopita, vilivyopo na vijavyo, ndiyo maana daima kimejikita katika sera makini, mikakati endelevu na oganaizesheni thabiti, kuibua dhana za mabadiliko mapya ya kimfumo na kiutawala kwa ajili ya kuzungumzia maendeleo ya zaidi ya miaka 50 hadi 100 ijayo.

Nikushukuru tena Isaac.

Sehemu kubwa ya masuala ambayo umejaribu kushauri hapa, ama yako katika hatua mbalimbali za utekelezaji, mengine ni sehemu ya misingi ya uanzishwaji wa CHADEMA, hivyo imekuwa ni sehemu ya majukumu ya kila siku katika kuwatumikia Watanzania, zinaweza kuwa zinabadilishwa modus of operandi, kwa nia ya kuboresha, lakini lengo, dhamira na nia ikabaki pale pale.

Kitu kikubwa sana cha msingi, saidia kuwatia shime wanachama wenzako (kama nawe ni mwanachama) kushiriki katika mpango wa sasa wa kukiweka chama mikononi mwa wanachama. Masuala mengine mengi tu uliyoshauri hapa si lazima yafanywe kuanzia makao makuu, ungeweza hata kusaidia yafanayike katika ngazi ya msingi au tawi. Hivyo Isaac kama hujajiandikisha, nenda ukafanye hivyo kwenye msingi wako na ulipie kadi yako.

Bila shaka huko pia utapata fursa ya kushiriki vikao na kupata jukwaa murua la kupenyeza mawazo yako na kupata fursa ya kufuatilia na kusukuma utekelezaji wake.

Karibu.

Makene

0752 691569/ 0688595831

Lengo letu sote ni kuuondoa mfumo mbovu wa utawala kwa hiyo juhudi ziongezwe kila pahala.
 
Back
Top Bottom