Kama Una Baba yako, Mama Yako, Bibi Babu, Dada Na Hata wewe Mwenyewe na Wanyonge Wote Serikali ya Awamu ya Tano Imekaribia kuleta Mkong'oto Huu Huu hapa (Kilio na kusaga Meno)
Kuna mswada unakuja na kwa Bunge letu la Wangapi wanakubali Waseme Ndiyooooo "Ndiyoooooo" waliosema ndiyo wameshinda "Utapita"
MSWADA HUO Unaenda kuua wastaafu Na sisi Tunao karibia kustafu
Ni hivi Mafao ya wastafuu yatakuwa hivi Tega sikio, utalazimika kulipwa 38% tu na 62% utakuwa unalipwa kila Mwezi (monthly) hapa ili unielewe nikupe mfano. kama ilikuwa ulipwe milioni 100 kama hela yako ya kustafia maana yake kwa mswada mpya utalipwa pension ya mkupuo 38 milioni halafu milioni 62 ulipwa kila mwezi.
Ukistafu na umri wa miaka 61 utakula hicho kiasi cha million 38 kigingine utalipwa kidogo kidogo kila mwezi
Ubaya wa hili siku ukifa tu kila kitu kimekufa malipo kila mwezi nayo yanakufa. Hivyo hela nyingi zitabaki kwenye mifuko maana rekodi inaonyesha wastaafu wengi hawaishi muda mrefu na hasa ukizingatia mafao yatapungua.
2. Mume akifa Mke na wategemezi watahudumiwa miaka 3 tu kisha huduma itakoma wakati ungepewa yote ungewaachia miradi familia wakaishi hata kama haupo
3. March 2018 mifuko itaunganishwa kubaki mifuko 2 tu. Yaani LPF, NSSF PPF sijui nani sijui nani itafungwa na kubaki mifuko miwili tu (Vibarua vinaenda kuota nyasi)
4. April 2018 sheria itaanza kutumika Yaani Mwakani Kuna kilio kikuu kwa watumishi wa mifugo na wastafuu
My Take
Kwa ufupi bila kupindisha muswada huu utaumiza watumishi wote ,Bunge Mkafanye kazi yenu, sasa Hiki ni kipimo chenu cha kudhibitisha Mpo huru na kwamba ni muhimili unajitegemea ,Wabunge wetu msipoliona hili kuwasemea watumishi basi Mtawasononesha watumishi
Yaani Ufanye kazi miaka 61 ukitumikia umma uzeeni uporwe haki itasikitisha
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.