mangikule
JF-Expert Member
- Jun 11, 2012
- 6,343
- 5,849
Maana rahisi ya uchochezi ni kuleta mitafaruku katika jamii bila kujali hisia za jamii husika! Uchochezi neno linalozaliwa na kitendo kuchochea ni kuhamasisha uhasama na majibizano yanayoishia katika mapigano na mitafaruku mingine. Mchochezi huwa hasikii ushauri wa aina yoyote wala kufikiria amani ya wanaomsikiliza au kumzunguka. Mchochezi ni mbabe, mshari na asiye staha.
1. Kuzuia mikutano ya hadhara ya kisiasa ni uchochezi tosha
2. Kauli za kibabe kuwa sijaribiwi, sipangiwi ni uchochezi mkubwa
3. Kubagua watanzania wakati wa utekelezaji wa sheria ni uchochezi wa hatari mfano kumlinda DSM RC dhidi ya tuhuma mbali mbali.
4. kutoa kauli kinzani dhidi ya taratibu za utawala bora kama vile kuelekeza polisi kuwa rushwa ya elfu tano siyo rushwa bali ni fedha ya kubrash viatu. huu ni uchochezi mwingine.
Yapo mengi yamefanywa na huyu kiongozi yanayoashiria uchochezi.
Wananchi wakisha choka kwa uchochezi huu wataamua la kuamua! Mnafahamu mchochezi mkuu wa karne hii Tanzania?