Haya ndo niliyoyaona Mtwara katika ziara yangu

Haya ndo niliyoyaona Mtwara katika ziara yangu

mr. loner

Senior Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
168
Reaction score
229
Wadau,

Hatimaye nimeamua kufuata gesi ilipo ila kabla sijafika nimejionea mengi. Mtwara ni mkoa ila kuna baadhi ya wilaya zake ili huzifikie lazima upite mkoa wa Lindi hivyo nilipofika mnazi mmoja nikashuka ili niende wilaya ya Masasi.

Maajabu nilianza kuayaona njiani, kufika sehemu panaitwa mtama gari ikasimama nikaona watu wananunua mizizi fulani hivi testless kuila lazima utumie chumvi la sivyo haitashuka, wenyewe wanaita ming'oko na inapatikana huku tu.

Nikiwa kwenye gari nikaona neno ndanda nikashuka nijue inapatikana Ndanda FC, mwenyeji wa pale akanipeleka mahali panaitwa mkorosho haramu, kuna nyama za kila aina na ya bei ghali zaidi ni ya rats, kuuliza nikaambiwa jina halisi la eneo linaitwa Mpowora.

Katika tembea tembea nikauliza wanavyopata maji ndipo nilipoanza kujua lile eneo ni zaidi ya nchi. Pale kuna mission ya Ndanda ambayo inazilisha umeme na kusambaza eneo lote la mission, hospital pamoja na nyumba za watumishi. Wanachuo cha ufundi na kiwanda cha kuchapa vitabu ambavyo vinahudumia Mtwara mzima.

Wana kiwanda cha mawe ambacho kinachonga picha ya mtu yeyote unayempenda ama jiwe la pembe ama misalaba ila gharama yake unaweza nunua fuso na sijui kama uwa wanalipa kodi, katika kuuliza waliniambia ata picha ya Nyerere walishaichonga kitambo na ipo mnarani Mtwara mjini ila nilipofika sikuiyona, anayway haikuwa tatizo ila kazi zao nilizikubali. Hapa pia kuna kanisa kubwa sana la Father Benedict linaingia watu zaidi ya 800 ila j2 nilipohudhuria nilishangaa sadaka yao haizidi elfu 20, anayway nikaamua kuondoka kuelekea masasi.

Huku ndio mahali pekee majina ya vijiji yaanzia na chi, mfano nilipata chikundi, chipite, chipuputa, chinongwe, chimbele, chikamlapa, chimadeko mpaka nikaingia masasi.

Huku napo majina ya viungo vya mwili imepewa mitaa. Utasikia migongo, kuna mitumbo, mikifua nk, huku wanalima sana Mihogo kama zao kuu ila ndio sehemu pekee nilishangaa watu wengi wakitumia kile kijembe cha bustani kulimia shamba kubwa sana.

Niliingia ndani ndani kidogo nikashangaa vitoto vya miaka kumi hadi kumi na mbili vinafundishwa kuishi na mume wenyewe wanaita kumcheza ngoma, hii ipo huku mtwara tu na wanadai mara nyingi uwa ni kuanzia miezi hii maana korosho zinakuwa zimekomaa.

Nikaelekea ndani zaidi panaitwa likamdobe aiseee huku ndio hatari ngoma kila sehemu na watoto wanakata viuno hatari. Cha ajabu napo ndoa za mitara sio nyingi ila wajane ni wengi zaidi. Kuoa na kuacha ni jumbo la kawaida na hakuna tatizo, kuna jamaa mmoja yeye ana watoto 21 kila mmoja na mama yake.

Huku ndipo mahali kijana akishanunua godoro tu anaoa bila chenga.

Mtwara ndio sehemu pekee pia wanakula upupu ila ukikosea kuupika utajuta

Lami ya kutoka Masasi hadi Mtwara ndio lami pekee ya wakoloni iliyo imara ila ina mawimbi kiasi kwamba kama sio dereva mzuri unaweza angusha gari.

Mtwara ndio sehemu pekee kuna kipande cha reli inayaoanzia Nachingwea hadi bandari ya Mtwara na kwa bahati ndiyo reli pekee nchini wananchi waliamua kuigawana baada ya uhuru na kila mmoja kuondoka na chuma chake.

Ndio sehemu pekee tena bomba la gesi linatoka mnazi bei hadi bandarini na lingine linatoka msimbati hadi darisalama.

Mtwara stadium ndio uwanja pekee wa mkoa wenye ngazi jukwaaa kuu ila mzunguko ni mwendo wa kusimama wenyewe wanauita Nangwanda.

Huku kuna makabila mawili tofauti wanazungumza lugha moja. Wamakonde na Wamawia lugha yao moja tofauti makazi tu.

Nilipita naliendele na kushangaa pia Mihogo kupewa majina ya wanawake tu sijui walizingatia nini, mfano kuna Mwanaidd, Kristina, Hadija na Anes.

Ghorofa refu mkoa mzima lina floor tatu tu, mkoa huu unakua kwa kasi sana ukichangiwa na vitu viwili tu. Chuo cha SAUT na Mradi wa gesi.

Bandari ya Mtwara ndio bandari pekee marekani wanamilki kaeneo eneo, mfano zinapofunga gati pale niliona silinda tano ndefu sana za blue nikaambiwa ni mitambo ya wamarekani ya kuchimbia mafuta baharini japo uhakika sina. Pia ndio bandari pekee kuna boti za askari wa marekani zinazopiga doria.

Naelekea msimbati kwenye chanzo cha gesi mniombee.

Wanadaa mnipokee nakuja kesho nadhani scorpion keshakamatwa
 
Watu na majungu yenu, mbona usiishngae Dar kuzungukwa na Pwani ukaishangae Mtwara na Lindi kuingiliana!! Kitu kidogo tu hapo barabara ya Mtwara Masasi imefuata mpaka wa Lindi na Mtwara, so bara bara imenyooka ila mpaka umekaa kama zigzag kuikatiza barabara unatoka Mtwara unapita Lindi unapita Mtwara tena unaenda Lindi ukirudi Mtwara umeingia Masasii!!!

Kuhusu ngoma; Wazaramo na Waluguru huko kwenu Dar wanacheza disco ila Wamakonde huko Mtwara ndiyo umeona wanacheza ngoma siyo??

Heshimu chakula cha watu, mizizi test-less si lugha nzuri ila sema wewe ulishindwa kuila kama ambavyo wazee wa kijijini kwenu (najua Dar si origin yenu) wanavyoiona soseji (sausage) test-less!!

Kuna Kimawia na Kimakonde, japo zinafanana lakini si lugha moja!! Ni kama Kiswahili cha Zenji na Bara, kama unajua tofauti yake utanielewa vizuri
 
Niliishi Newala kitongoji cha Nangwala, , niliishi pia tandahimba, nikaishi nanyumbu , masasi na Mtwara mjini Nilikua nakaa shangani, uongo umeongea mwingi kuliko ukweli
Wewe utakuwa uliishi ila ukutaka kuijua vema ama ikute wewe ni ndugu zake na kina msemo
 
Uliwahi kutoa historia ya uongo ya mkoa wa kigoma nikakuchora tu, Lindi na Mtwara INA mengi pia mazuri ya kujifunza na zaidi watu wa Mtwara Ni wakarimu sana,
Wewe unaiyona ya uwongo kama upo mtwara kweli kesho asubuhi twende msanga mkuu usiishie kukaa mjini tu
 
Watu na majungu yenu, mbona usiishngae Dar kuzungukwa na Pwani ukaishangae Mtwara na Lindi kuingiliana!! Kitu kidogo tu hapo barabara ya Mtwara Masasi imefuata mpaka wa Lindi na Mtwara, so bara bara imenyooka ila mpaka umekaa kama zigzag kuikatiza barabara unatoka Mtwara unapita Lindi unapita Mtwara tena unaenda Lindi ukirudi Mtwara umeingia Masasii!!!

Kuhusu ngoma; Wazaramo na Waluguru huko kwenu Dar wanacheza disco ila Wamakonde huko Mtwara ndiyo umeona wanacheza ngoma siyo??

Heshimu chakula cha watu, mizizi test-less si lugha nzuri ila sema wewe ulishindwa kuila kama ambavyo wazee wa kijijini kwenu (najua Dar si origin yenu) wanavyoiona soseji (sausage) test-less!!
Huna lolote umejaza uongo na unafki tupu
Pia unaonekana ni mshamba ndio first time unazunguka tzn . South inavingi vuzuri history yakutosha wewe unasifia jina la kijiji
Wew bila shaka ni mwanaume wadar ....
Mkuu mmakonde kwenu lazima usifie usiposifia wewe atasifia nani? Vizuri vipo maa
Huna lolote umejaza uongo na unafki tupu
Pia unaonekana ni mshamba ndio first time unazunguka tzn . South inavingi vuzuri history yakutosha wewe unasifia jina la kijiji
Wew bila shaka ni mwanaume wadar ....
Mkuu mmakonde mjanja lazima kwenu upasifie la sivyo hakuna wa kukusaidia kusifia, vizuri vipo havikosekani maana kama ni korosho nimekula za kutosha alfu 7 unapata kilo na nusu ila mji ndio unakua sasa sipati picha uko nyuma ulivyokua nahisi nyumba za nyasi zilikuwepo hadi mjini bima maana mitaa ya Chikongola nimeona nyumba kama tano hivi zimeezekwa kwa nyasi
Kuna Kimawia na Kimakonde, japo zinafanana lakini si lugha moja!! Ni kama Kiswahili cha Zenji na Bara, kama unajua tofauti yake utanielewa vizuri
 
Shangani hotel mtwara
20140904_163944.jpg
 
Back
Top Bottom