Haya ndiyo majukumu mazito ya Mkurugenzi(DED), mwendokasi wataweza?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,045
114,509
KWA MUJIBU WA MEMORANDA YA FEDHA SERIKALI ZA MITAA(LGA) HAYA NDIO MAJUMKUMU MAZITO YA DED

1. Ensuring the existence of a formal and satisfactory system of financial administration;

2. Securing compliance with the prescribed financial procedures by operating departments;

3. Directing the work of the Internal Audit section, receiving their reports and after consultation with relevant head of departments, ensuring recommendations and acted upon and submitted to relevant authorities;

4. Overall management of Council’s expenditures, revenues, and all assets and liabilities;

5. Ensuring compliance of all statutory guidelines for the financial Management of Council affairs;

6. Responding to queries within given deadlines from the Office of the Controller and Auditor General, the Local Authority Account Committee (LAAC) and the Minister;

7. Making certain that councillors are kept regularly informed of the financial affairs of the Council;

8. Being secretary to the finance Committee;

9. Making sure that computerized system operates;

10. Keeping under good Custody all assets and property of the Council; and

11. Adhering to procurement functions stipulated in Public Procurement Act and its related

KWA TAFSIRI ISIYO RASMI

1. Kuhakikisha kunakuwa na mfumo rasmi na wakuridhisha katika usimamizi wa fedha

2. Kuhakikisha idara zinafanya matumizi kwa mujibu wa taratibu za fedha

3. Kuhakikisha kitengo cha ukaguzi wa ndani kinafanya kazi vyema, kupokea taarifa za ukaguzi wa ndani, na kwa kushirikiana na wakuu wa idara ahakikishe maoni ya mkaguzi wa ndani yanajibiwa na kutekelezwa na anawasilisha majibu hayo kwa mamlaka husika ambazo ni CAG, RAS na Chief Internal Auditor

4. Usimamizi wa matumizi, mapato, mali na madeni yote ya halmashauri kwa ujumla

5. Kuhakikisha sharia, sera, kanuni na miongozo yote ya usimamizi wa fedha za halamashauri inafuatwa.

6. Kuhakikisha kuwa anajibu kwa wakati hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) na wizara

7. Kuhakikisha waheshimiwa madiwani wanapata taarifa za fedha za halamashauri

8. Kuwa katibu wa Kamati ya fedha ya Halamshauri. Kamati hii wajumbe wake ni madiwani.

9. Kuhakikisha mifumo ya kompyuta inafanya kazi

10. Kuhakikisha utunzaji mzuri wa mali za Halmashauri

11. Kuhakisha sharia ya manunuzi ya umma na kanuni zake zinafuatwa

MAJUMKU MENGINEYO

1. Kuidhinisha malipo

2. Kuidhinisha mikataba yote ya halmashauri

3. Kuteua Bodi ya Zabuni kwa mujibu wa sharia

4. Kuteua Kamati ya Ukaguzi(Audit Committee) kwa mujibu wa sharia

5. Kuwa mkurugenzi wa uchaguzi ngazi ya wilaya pale inapotokea

6. Kuteua kamati ya upembuzi wakati wa manunuzi makubwa

MY TAKE

Hii kazi sio rahisi kama mashabiki wa mwendo kasi mnavyodhani. Huyu mtu anaenda kuwa msimamizi wa idara 19 pale halmashauri. Ikiwepo idara ya elimu na afya zenye changamoto za kufa mtu. Huyu mtu ndio anaenda kukuza uchumi wa wilaya na kuongeza pato la taifa kupitia wilaya yake. Mikataba mikubwa ya mabilioni ya fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo inaenda kuidhinishwa na yeye baada ya kujiridhisha kila kitu kiko sawa.

Anakwenda kusimamia matumizi ya mapato ya ndani ya zaidi ya bilioni 20 mfano Manispaa ya Kinondoni mpaka milioni 500 kwa halmashauri mpya. Anakwenda kusimamia ruzuku ya serikali mabilioni ya fedha.

Anakwenda kusimamia ufungaji wa hesabu na kujibu hoja ngumu za CAG kama tulivyoona hapo juu, matokeo yake unashindwa kuzuia au kujibu hoja unaanda maburungutu ya kuhonga wakaguzi

Kwa maoni yangu, serikali isione aibu, pangia hawa watu wasio na sifa majuku mengine mara moja. System inajua nani mwenye uwezo na asiye na uwezo

HITIMISHO

Kuna mahali pa kujifunzia lakini sio ukurugenzi. Mngeweza kuwapatia ukuu wa idara na vitengo kwa mujibu wa taaluma zao.
 
Mkuu ukiacha haya ya kwenye maandishi inahitaji mtu amabye anaexperience na LGAs kwa zaidi ya miaka 10.
Na ambaye amekuwa mkuu wa Idara kwa zaidi ya miaka 7,
Kwani anakuwa anazijua changamoto za LGAs vyema na namna ya kuzitatua
 
Anna C. Shija, Mkurugenzi Mpya wa Halmashauri ya Same, Kilimanjaro...
siha.jpg
 
Wangeongeza kwenye sifa tu kwamba Lazima Mkurugenzi yeyote awe na CPA (T). Hayo majukumu ni mazito na inahitaji mtu aliyebobea haswa kwenye mambo ya fedha na uchumi.
 
Nipo halmashauri kwa miaka 15 na ni mkuu wa idara kifupi kama wateule hawakuwahi hata kuwa wakuu wa idara na hawajafanya kazi halmashauri ni vema wakatae hizi teuzi wanaenda kufeli vibaya na hiki ni kipindi cha kufunga hesabu wanakwenda kuanza na kufunga hesabu ambazo hawajahusika nazo kabisa believe my words hii nchi inaenda ku collapse soon bora uDAS na DC lakini mkurugenzi hapana aisee
 
Wangeongeza kwenye sifa tu kwamba Lazima mkurugrnzi yeyote awe na CPA (T). Hayo majukumu ni mazito na inahitaji mtu aliyebobea haswa kwenyeakwenyeambo ya fedha na uchumi.
na ndiyo maana waweka hazina wazoefu wanapopewa ukurugenzi huwezea hii kazi.hakuna changamoto asiyoijua
 
Bora tu nitumie nguvu zangu za akili kujiajiri kuliko kutumia nguvu kubwaaa kwenye kutumikia watu mwisho wa siku nimeshatumia nguvu ya akili nyingi nakuja kutumbuliwa!
 
Nipo halmashauri kwa miaka 15 na ni mkuu wa idara kifupi kama wateule hawakuwahi hata kuwa wakuu wa idara na hawajafanya kazi halmashauri ni vema wakatae hizi teuzi wanaenda kufeli vibaya na hiki ni kipindi cha kufunga hesabu wanakwenda kuanza na kufunga hesabu ambazo hawajahusika nazo kabisa believe my words hii nchi inaenda ku collapse soon bora uDAS na DC lakini mkurugenzi hapana aisee
Mkuu, mimi nadhani hizi nafasi zingekuwa zinatangazwa kama position nyingine. Hapa sasa ndo wahasibu waliopiga huko nyuma wanaenda kuwachezea karata. Na wengi walioteuliwa hawana profession ya accountancy au the like. Nakumbuka Mhasibu wetu aliwayi kumchezeo CEO ambaye alikuwa hajui hata balance sheet inatengenezwa Baba wa watu akapoteza kitumbua chake baada ya CAG kuja kukagua. Mzee wa watu alikuwa anafuata kila analoshauriwa na mhasibu. Kibaya zaidi Mhasibu alikuwa anamshauri kwa mdomo tu CEO naye anatekeleza. Yaliyomkuta anajua mwenyewe. Mhasibu bado yupo kazini anadunda.
 
Wangeongeza kwenye sifa tu kwamba Lazima Mkurugenzi yeyote awe na CPA (T). Hayo majukumu ni mazito na inahitaji mtu aliyebobea haswa kwenye mambo ya fedha na uchumi.
Hayo majukumu yana uzito/ ugumu gani? Uongozi ni kipaji, but management is to get things done.

Ni usimamizi tu,
 
Back
Top Bottom