Bigbootylover
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 2,847
- 1,828
Yeye:Aiseee, vipi mbona unahama? Umekaa kidogo tu
Mimi:Aah nimepata chumba kingine tu huko mjini
Yeye:Aah sio mbaya, japo umejitahidi, wengi huwa hawadumu hapa, huwa wanakaa kidogo tu na mambo yao lazima yaende vibaya, na hatimae huondoka.
Mimi: (Nikashtuka kidogo sababu kilichonifanya nihame ni kweli, ni kutokana na hali mbaya iliyonikabili, niliona nisingeweza tena kulipa kodi ya chumba na sebule, self contained kwa hali yangu ilivyogeuka haraka, toka juu kwenda chini kwa haraka sana, hela inaisha kimazingara sana) Nikamuuliza, kweli? Kwa nini?
Yeye: Huyu boss wangu ni mtu "mbaya"(Ushirikina), inaelekea anamchezo mbaya huwa anafanya, hata baadhi ya wafanyabiashara wenzake wanamlalamikia, wateja wake pia(Maana, anaduka pekee mtaa mzima, wengine wameshindwa kuanzisha na watakaoanzisha duka lazima waibiwe).
Mimi:Nikamkumbuka kaka yangu ambaye alikuja tukae nae, yeye pia alikuwa analalamika mambo yake yameanza kuwa mabaya toka aje hapo kwangu, nikajumlisha na hali yangu then nikaunganisha dots, kiukweli niliwaza sana. Japo mimi siamini katika haya mambo lkn kiukweli nimeona hapa kuna chembe flan ya ukweli, najua ni muda ambao biashara haziendi sawa, lakini Mwenyenyumba wangu mambo yako vizuri tu.
Kilichokuja kunishtua zaidi huyu mfanyakazi katika maongezi yetu tuliligusia swala la yeye kulala, anafanya kazi kama mlinzi lakini hata ukifika mchana hana pa kupumzika, inamaana ye ni mlinzi forever, hajapewa chumba, nilipojaribu kumuuliza kuna uhaba wa vyumba?
Hapana kuna vyumba vingi lakini kuna viwili ni kwa ajili ya watoto wakija
likizo, kuna vingine VIMEFUNGWA KWA AJILI YA "VITU VYA DUKANI".
Aisee, Generally nimelifikiria sana hili suala, japo bado sijaelekea sana kwenye kuamini mambo ya kishirikina, lakini kama ni kweli basi sisi tusioyaamini haya mambo na IMANI ZETU HAZINA NGUVU SANA, AMBAO TUPO WENGI, TUNAONEWA SANA NA WATU WA AINA HII, pia tujitahidi kuulizia vizuri nyumba za kupanga, kisa cha waliopita kuhama.
TUMUOMBE SANA MUNGU AU KUVIOMBEA VYUMBA AU NYUMBA TUNAZOTAKA KUHAMIA. TUWE MAKINI NA MAJUMBA YA WATU TUNAYOPANGA AU TUNAYOTAKA KWENDA KUPANGA.
Hapa makazi mapya, japo sijapasoma vizuri ila naona wapangaji tupo wengi na watu wanamishe zao kama kawa. Kitu kingine pia kule nilipotoka, kipindi nahamia kuna jamaa chumba cha pili ndo alikuwa anahama sikupata hata muda wa kuongea nae, ile nyumba inavyumba viwili tu vya kupanga.
TUWE MAKINI