The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,911
- 2,891
Necta wametoa matokeo ya kidato cha nne huku wakizipanga shule katika madaraja kulingana na viwango vya ufaulu necta hawishii hapo bali wanawapanga hata wanafunzi mbaya zaidi wale waliopata ufaulu dhaifu sana shule zao huchukuliwa hatua hapa ndipo najiuliza unamshindanishaje mwanafunzi anaesoma shule ya msingi lanzi yenye wanafunzi 350 waalimu wawili na Hao waalimu wanaishi kwenye tembe aliyojitolea msamaria mmoja huku wakilazimika kulala kwenye kitanda cha kamba kutokana na mazingira duni na mwanafunzi wa feza au St Francis ambazo zina kila kitu?? Huku ni kukatisha tamaa watoto wa maskini ili wajione hawana akili na kwa Jinsi hiyo hata washindi wanaopatikana sio halali kimantiki kama wana adhma ya kushindanisha shule ili kuinua viwango basi serikali itoe huduma sawsawa kwa shule zake zote ndipo wazishindanishe