Mvua zimeleta majanga na kuacha majanga. Lakini Mvua zisingekuwa na maafa makubwa kama tungekuwa na mifumo mizuri ya maji taka. Kwa kuwa na mifumo mibovu maji yamejitengenezea njia zake na kuharibu miundombinu mingine. Barabara nyingi sana haziko katika hali nzuri na zinaweza kuharibu magari mengi sana nchini.
Kwa kuzurura sehemu chache tu, nimeona yafuatayo. Kona ya Shekilango (Dar), karibu na soko kuna bonge la shimo na lina maji mengi. Sijui kwa nini linaachwa hadi muda huu ikiwa serikali za mtaa zipo.
Barabara ya Temeke na Stand ya Temeke imejaa madimbwi na maji meusi ambayo ni tishio kwa magonjwa ya kuambukiza kama kipindupindu ambacho kwa sasa ni tishio kwa afya za waliowengi.
Madimbwi hayo na maji haya ni hatari kwa vyombo vya moto na kwa watoto. Je tunasubiri mtu afe?