haya mambo yote aliyaacha mwalimu ?nani kayaua? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

haya mambo yote aliyaacha mwalimu ?nani kayaua?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, May 2, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  -Wewe ulitaka tukipigwa na Amin tukae kimya alafu mwisho wake iweje?. Tuwe watumwa sio?.
  -Air Tanzania ilikufa chini ya Mwalu Nyerere au watudanganya?.
  -Shirika la reli aliliua Mwalimu au watudanganya?
  -UDA na KAMATA kaua Mwalimu au watudanganya?
  -Reli kazing'oa Mwalimu au watudanganya?
  -Kiwanda cha nguo cha urafiki kakiua Mwalimu au watudanganya?
  -Mwatex ya Mwanza na Mutex ya Musoma kaua Mwalimu au watudanganya?
  -Tanganyika Packers Arusha kaua Mwalimu au watudanganya?
  -Kiwanda cha Kiko Arusha na Karatasi Kaua Mwalimu au watudanganya?
  -Kiwanda cha Ngozi kule Mosho kaua Mwalimu au watudanganya?
  -Kiwanda cha Sukari kule TPC na timu yao ya mpira kaua Mwalimu au watudanganya?
  -Ushirika Moshi na Timu yao ya Mprira kaua Mwalimu au watudanganya?
  -Kiwanda cha Maziwa Arusha kaua Mwalimu au watudanganya?
  -Kiwanda cha magunia Moshi kaua Mwalimu au watudanganya?
  -Hoteli za Serekali kule Lake Manyara, Ngorongoro, Serengeti na Lobo Kaua Mwalimu au watudanganya?
  -Hotel ya Embassy na Kilimanjaro Dar es salaam kaua Mwalimu au watudanganya?
  -Shirika la kuchimba madini STAMICO kaua Mwalimu au watudanganya?
  -Mashule Mazuri tuliyosoma sisi kama LYAMUNGO, TECHNICAL, MAWENZI,ILBORU, TAMBAZA, NK kaua Mwalimu au watudanganya?
  -AICC kule Arusha umejenga wewe au Mwalimu kwa kodi za Watanzania?
  NOTE:
  Unajua Bwana kama unachuki na Mwalimu sema lakini sisi mpaka Sekondari tumesoma bure na kupata mlo bure, likizo warranti wa Serekali bure. Najua anayo makosa mengi sana yaliyotokea enzi zake za Azimio la Arusha na yeye alishasema kuna sehemu tulikosea. Tumsamehe alikiri. Lakini huwa najiuliza unaweza Mfananisha Mwalimu na Mkapa au Jakaya Mrisho Kikwete. Watu ambao wanatoa Madini yetu na ardhi yetu kw Mikataba ya miaka 90. Mimi nakushauri soma lama za NYAKATI na pekua vitabu vyote alivyotunga Mwalimu. Mwinyi, Mkapa,Jakaya wametunga vitabu vingapi hata vya hadithi?. Tujivunie Mwalimu watu wa nje wakisikia tunampenza watatuona Vi chaa au wenda wazimu.Wenzetu kule Ghana mpaka leo wanamuenzi Kwame Nkuruma sisi tunambeza Mwalimu tena kwenye vyombo vya habari kama vile tuna laana. Mimi nadhani kuna haja ya kurudia somo la Siasa mashuleni na kila mtoto nchi hii apite Jeshi akajifunze nidhamu. Hatuna nidhamu.Mwalimu na mabaya yake tusingepaswa tumkejeli ni kuwa ni Marehemu tunapaswa tusahau yote tumuenzi kama Babu, na Baba wa Taifa hili ambalo sasa ndio limeoza kabisa.Hatuna cha kujivunia Tanzania zaidi ya Mlima Kilimanjaro na Hifadhi za Taifa ambazo na zingine alianza kuziuza Mwinyi, Mkapa akamalizia Kikwete.Nenda sasa hivi Serengeti utashangaa kuna Sehemu Mtanzania hauruhusiwi kukanyaga. Maajabu ya 15 ya Dunia.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  usishangae kuwa hii post imeikuta katikati au imenyofolewa seheu ila nadhani ukiisoma utapata mantiki au sura ya halisi
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  jibu ni Mwinyi Mkapa Kikwete ndio wameviua,obama katunga kitabu na nyerere alitunga vitabu hiki sio kipimo cha rais bora offcourse lakini mimi nadhani viongozi wetu ni mambumbu na wachumia matumbo yao
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  CCM wabya sana, hawana hurruma na nchi yetu kabisa wanakata mti huku wameukalia ni kama tu kahifadhi uranium ndani kwenuye nyuma yake
   
Loading...