Haya kizingiti kingine tena kwenye katiba

Haya kizingiti kingine tena kwenye katiba

Naamini ikiwa hoja hii itakuwa sahii, basi Spika anatakiwa kuwasiliana na Tume kwanza na kuijulisha kutoa kikokoto upya na kuwapa vyama ili kupitisha majina kwa mujibu wa uwiano uliopo. Kisha Spika kupitia bunge litangaze kuwepo kwa nafasi wazi baada ya vyama kupunguza wabunge wake
 
Nashukuru sana mkuu kwa busara yako kubwa ya kuwa tayari kukosolewa.
Maelezo ya katiba yameainisha wazi kabisa sababu za kuondoka kwa mbunge kwenye nafasi yake, kwanza haijataja aina ya uchaguzi kama kigezo. Imesema uchaguzi. Kwahiyo waweza kuwa mkubwa au mdogo. Lakini pia ile ya 71 imeweka bayana endapo atakosa sifa, inamaana anaweza kuwa alikua na sifa lakini kwa sababu mbalimbali kama mwandishi alizotaja akajikuta amepoteza sifa. Ambayo ni tabia ya asili ya dunia kuwa na sifa au kupoteza sifa.
Kwa muono wangu naamin ombi la Spika kutazama hili liko sawa kwakua muda wote bungeni uwiano unatakiwa kuzingatia matakwa ya kikatiba. Ila uwiano uliopo sasa unapishana na matakwa ya katiba. Hili linaitaji maelekezo ya Spika kwakua ndiye anaetajwa na sheria kuitaarifu tume kama kuna nafasi imekua wazi
ni vizuri pia kupitia sheria ya uchaguzi ili kuweza kuja na judgement nzuri kwenye hili.
 
Chama chake kilichomteua, na sio wananchi, maana hata hao waliochaguliwa bado wanawakilisha vyama vyao huko bungeni na sio wananchi waliowachagua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui umenielewa.

Akishateuliwa na chama chake anatakiwa apigiwe Kura ili awe na sifa ya kuitwa mbunge wa kuchaguliwa.

Sasa hii mambo ya kupita bila kupingwa inatoka wapi?
Huoni kuwa anakosa sifa ya kuitwa Mbunge wa Kuchaguliwa?

Chama kinateua wabunge wa Viti maalum tu na kupitishwa moja kwa moja kuwa wabunge kwa kura ndani ya Chama. Ndio maana hata akiondolewa anachukuliwa aliyefuata kwa kura nyingi ndani ya chama.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama amebaki peke yake kura za nini si niswala la kuokoa mapato tu.
Huoni kuwa anakosa sifa ya kuwa mbunge wa Kuchaguliwa?

Tukisimamia kauli ya kuokoa Mapato basi tusubiri kuizika Demokrasia muda sio mrefu .

Ikiwa Kila Mbunge wa Jimbo atapita kwa kura hata awe peke yake basi hata Haki ya watu kuchagua na Kuchaguliwa itakua imetekelezwa kivitendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naona udhaifu kwenye Kutekeleza Katiba mana inawataja wabunge wa Aina Tatu tu.
Kuchaguliwa kupitia kura Majimboni.
Viti maalum
Wakuteuliwa na Mh.Rais.

Sasa wa kupita bila kupingwa wametokana na nini ?
Kwa nini asipigiwe kura yeye na kivuli ili zoezi likamilike kikatiba?

Mana anapofanya figisu na kubaki peke yake bado haimfanyi na kumpa uhalali wa kuwa ametumwa na wananchi wa jimbo husika mana hawakumpigia kura. Atakua anamuwakilisha nani?


Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni HOJA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huoni kuwa anakosa sifa ya kuwa mbunge wa Kuchaguliwa?

Tukisimamia kauli ya kuokoa Mapato basi tusubiri kuizika Demokrasia muda sio mrefu .

Ikiwa Kila Mbunge wa Jimbo atapita kwa kura hata awe peke yake basi hata Haki ya watu kuchagua na Kuchaguliwa itakua imetekelezwa kivitendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa uelewa wangu, ili uchaguzi ni pale unapopata mtu wa kukupinga. Yaan iwe kwenye chama chake au vyama vingine. Ila unakosa mpinzani manake unakua umepitishwa kwa asilimia mia na watu wa jambo lile.
 
Hawafukuzwi ila katiba inawataka kuwapisha wengine! Yaan wanastaafu mpaka watakapohitajika tena. Kama kuna watu watajiuzulu kwenda kwingine. Ila itategemea tafakari ya mh Spika
Kura za urais hazihami Chama!! Wanazingatia uwiano wa kura za urais.
 
mpe mwongozi wa kikatiba coz wanafikiri wananchi hatusomi katiba na kuzielewa ndio maana wanatupeleka kama watoto
 
Kura za urais hazihami Chama!! Wanazingatia uwiano wa kura za urais.
We umeunda kifungu chako? Hiyo ni ibara ya ngapi kwani ile aliyosoma mkurugenzi wa uchaguzi ibara ya 78 na ile ya 71 haisemi hayo ya urais
 
Back
Top Bottom