Haya kizingiti kingine tena kwenye katiba

JOMAM

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2012
Posts
330
Reaction score
139
Hii nyingine tena naitoa fb
Anaandika John deya.

BARUA YA WAZI KWA MH SPIKA.
Salaam
Nimeamua kuandika barua kuja kwako ya wazi kama mwananchi wa kawaida kukuomba kutazama jambo linalonipa shida kwenye katiba. Kwa heshima na taadhima kubwa naomba kukieleza kiti chako, kumekua na utaratibu wa kujiuzulu kwa wabunge na kuhama vyama, jambo ambalo ni haki ya kikatiba ya raia, nahivyo kusababisha kurudiwa kwa uchanguzi katika kuziba nafasi hizo.

Hamahama hii imepelekea kubadilika kwa idadi ya wabunge kwa vyama tofautitofauti vilivyo na uwakilishi bungeni, jambo ambalo kwa muono wangu linaleta matokeo tofauti kisheria na kikatiba.

Mh Spika kwa mujibu wa taarifa ya Tume ya uchaguzi iliyotolewa kwenye vyombo mbalimbali vya habari mwaka 2015 baada ya uchaguzi ilisema " uchaguzi wa wabunge wa viti maalumu utazingatia tamko la katiba ibara ya 78 inayoonyesha watateuliwa kulingana na uwiano wa viti vya wabunge waliochaguliwa majimboni.

Yaan kwa vyama vilivyo pata uwakilishi. Aidha mtendaji mkuu wa tume ya uchaguzi bwana Kailima Ramadhani alifafanua kuwa endapo kutakuwa na nafasi wazi ya viti maalumu katika bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na sababu mbalimbali Spika wa Bunge humtaarifu Mwenyetiki wa Tume juu ya uwepo wa nafasi hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 37(3) cha sheria ya Taifa ya uchaguzi sura ya 343.

Mh Spika ni wazi baada ya hamahama ya vyama ya wabunge tayari uwiano umebadilika na ule wa mwaka 2015 kitu kinachonifanya kuona kuwa wapo wabunge wa viti maalumu wa chama kimoja wanaozidi ndani ya bunge kutokana na kupungua kwa wabunge wa kuchaguliwa wa chama chake, na wapo wa Bunge wa viti maalumu wa chama kingine wanaopungua kutokana na kuongezeka kwa wabunge wa kuchaguliwa wa chama chake, athari inayoweza kujitokeza hata kwenye utoaji ruzuku ya chama inayotokana na idadi ya viti vya wabunge kama tu maelezo yangu ya awali yatakua sahii. Ombi langu kwako kama Raia wa kawaida ni kukuomba kwa unyenyekevu mkubwa utazame ibara ya 78 ya katiba na kuwaandikia Tume ili kuruhusu watanzania wenzetu wa kike wasiostahili kuwa bungeni kupisha wale ambao sasa sifa zinawaruhusu kuwa.

Mh Spika huu ni Muono wangu kwa mujibu wa maelezo ya Tume na kifungu cha 78 cha katiba ila naheshimu na nitazingatia mwongozo wako ambao ndio dira ya bunge letu.
Mwananchi John deya.
 
Hii nyingine tena naitoa fb
Anaandika John deya.

BARUA YA WAZI KWA MH SPIKA.
Salaam
Nimeamua kuandika barua kuja kwako ya wazi kama mwananchi wa kawaida kukuomba kutazama jambo linalonipa shida kwenye katiba. Kwa heshima na taadhima kubwa naomba kukieleza kiti chako, kumekua na utaratibu wa kujiuzulu kwa wabunge na kuhama vyama, jambo ambalo ni haki ya kikatiba ya raia, nahivyo kusababisha kurudiwa kwa uchanguzi katika kuziba nafasi hizo.
Hamahama hii imepelekea kubadilika kwa idadi ya wabunge kwa vyama tofautitofauti vilivyo na uwakilishi bungeni, jambo ambalo kwa muono wangu linaleta matokeo tofauti kisheria na kikatiba.
Mh Spika kwa mujibu wa taarifa ya Tume ya uchaguzi iliyotolewa kwenye vyombo mbalimbali vya habari mwaka 2015 baada ya uchaguzi ilisema " uchaguzi wa wabunge wa viti maalumu utazingatia tamko la katiba ibara ya 78 inayoonyesha watateuliwa kulingana na uwiano wa viti vya wabunge waliochaguliwa majimboni. Yaan kwa vyama vilivyo pata uwakilishi. Aidha mtendaji mkuu wa tume ya uchaguzi bwana Kailima Ramadhani alifafanua kuwa endapo kutakuwa na nafasi wazi ya viti maalumu katika bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na sababu mbalimbali Spika wa Bunge humtaarifu Mwenyetiki wa Tume juu ya uwepo wa nafasi hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 37(3) cha sheria ya Taifa ya uchaguzi sura ya 343.

Hoja yake ni fikirishi... Sjui taratibu za bunge zinasemaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naona udhaifu kwenye Kutekeleza Katiba mana inawataja wabunge wa Aina Tatu tu.
Kuchaguliwa kupitia kura Majimboni.
Viti maalum
Wakuteuliwa na Mh.Rais.

Sasa wa kupita bila kupingwa wametokana na nini ?
Kwa nini asipigiwe kura yeye na kivuli ili zoezi likamilike kikatiba?

Mana anapofanya figisu na kubaki peke yake bado haimfanyi na kumpa uhalali wa kuwa ametumwa na wananchi wa jimbo husika mana hawakumpigia kura. Atakua anamuwakilisha nani?

Chama chake kilichomteua, na sio wananchi, maana hata hao waliochaguliwa bado wanawakilisha vyama vyao huko bungeni na sio wananchi waliowachagua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo spika kibaraka afanye atakavyo legacy yake ni spike dhaifu kutokea tangu uhuru hakuna cha kushangaza tuna puto tuu lile
Sasa povu la nini wakati ni matakwa ya kikatiba na upinzani pamoja na ile taasisi ya haki za binadamu na yule aliye kule kwenye chama cha wanasheria wamekua kila siku wakisoma katiba. Ngoja Tuheshimu katiba ila tuisome yote
 
Walishakula kiapo (viti maalumu) kulitumikia bunge, unawafukuzaje kwa mfano?
Hawafukuzwi ila katiba inawataka kuwapisha wengine! Yaan wanastaafu mpaka watakapohitajika tena. Kama kuna watu watajiuzulu kwenda kwingine. Ila itategemea tafakari ya mh Spika
 
Mimi naona udhaifu kwenye Kutekeleza Katiba mana inawataja wabunge wa Aina Tatu tu.
Kuchaguliwa kupitia kura Majimboni.
Viti maalum
Wakuteuliwa na Mh.Rais.

Sasa wa kupita bila kupingwa wametokana na nini ?
Kwa nini asipigiwe kura yeye na kivuli ili zoezi likamilike kikatiba?

Mana anapofanya figisu na kubaki peke yake bado haimfanyi na kumpa uhalali wa kuwa ametumwa na wananchi wa jimbo husika mana hawakumpigia kura. Atakua anamuwakilisha nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa kama amebaki peke yake kura za nini si niswala la kuokoa mapato tu.
 
Hawafukuzwi ila katiba inawataka kuwapisha wengine! Yaan wanastaafu mpaka watakapohitajika tena. Kama kuna watu watajiuzulu kwenda kwingine. Ila itategemea tafakari ya mh Spika
Aina mpya kabisa ya upupu, yaani spika akutafakarie?
Wabunge walioapa kulitumikia bunge haastaafishwi na tafakuri ya mtu! Ni muda au kushindwa kumudu kutekeleza majukumu ya kibunge,

Yaani umeweka msambwanda chini unasubiri busara kutoka kwa ******?
 
Kazi kwelikweli kwani ile miongozo wanayoomba kila siku wabunge huwa wanamwomba nani?
Katiba ndiyo inampa mtu ukomo kwenye kitu. Mpaka sasa kwa mujibu wa kikokoto kilichotumiwa na Tume ya uchaguzi tayari katiba inaonyesha kuna benchi wanazidi na kunabenchi wanapungua manake hapo ni swala la katiba na kiti kutazama kanuni ni zipi
 
Hii nyingine tena naitoa fb
Anaandika John deya.

BARUA YA WAZI KWA MH SPIKA.
Salaam
Nimeamua kuandika barua kuja kwako ya wazi kama mwananchi wa kawaida kukuomba kutazama jambo linalonipa shida kwenye katiba. Kwa heshima na taadhima kubwa naomba kukieleza kiti chako, kumekua na utaratibu wa kujiuzulu kwa wabunge na kuhama vyama, jambo ambalo ni haki ya kikatiba ya raia, nahivyo kusababisha kurudiwa kwa uchanguzi katika kuziba nafasi hizo.
Hamahama hii imepelekea kubadilika kwa idadi ya wabunge kwa vyama tofautitofauti vilivyo na uwakilishi bungeni, jambo ambalo kwa muono wangu linaleta matokeo tofauti kisheria na kikatiba.
Mh Spika kwa mujibu wa taarifa ya Tume ya uchaguzi iliyotolewa kwenye vyombo mbalimbali vya habari mwaka 2015 baada ya uchaguzi ilisema " uchaguzi wa wabunge wa viti maalumu utazingatia tamko la katiba ibara ya 78 inayoonyesha watateuliwa kulingana na uwiano wa viti vya wabunge waliochaguliwa majimboni. Yaan kwa vyama vilivyo pata uwakilishi. Aidha mtendaji mkuu wa tume ya uchaguzi bwana Kailima Ramadhani alifafanua kuwa endapo kutakuwa na nafasi wazi ya viti maalumu katika bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na sababu mbalimbali Spika wa Bunge humtaarifu Mwenyetiki wa Tume juu ya uwepo wa nafasi hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 37(3) cha sheria ya Taifa ya uchaguzi sura ya 343.
Mh Spika ni wazi baada ya hamahama ya vyama ya wabunge tayari uwiano umebadilika na ule wa mwaka 2015 kitu kinachonifanya kuona kuwa wapo wabunge wa viti maalumu wa chama kimoja wanaozidi ndani ya bunge kutokana na kupungua kwa wabunge wa kuchaguliwa wa chama chake, na wapo wa Bunge wa viti maalumu wa chama kingine wanaopungua kutokana na kuongezeka kwa wabunge wa kuchaguliwa wa chama chake, athari inayoweza kujitokeza hata kwenye utoaji ruzuku ya chama inayotokana na idadi ya viti vya wabunge kama tu maelezo yangu ya awali yatakua sahii. Ombi langu kwako kama Raia wa kawaida ni kukuomba kwa unyenyekevu mkubwa utazame ibara ya 78 ya katiba na kuwaandikia Tume ili kuruhusu watanzania wenzetu wa kike wasiostahili kuwa bungeni kupisha wale ambao sasa sifa zinawaruhusu kuwa.
Mh Spika huu ni Muono wangu kwa mujibu wa maelezo ya Tume na kifungu cha 78 cha katiba ila naheshimu na nitazingatia mwongozo wako ambao ndio dira ya bunge letu.
Mwananchi John deya.
mkuu isome hiyo ibara na ibara inayozungumzia sifa gani zinamfanya mbunge akishachaguliwa kupoteza ubunge wake ndo utalielewa hili.
 
Ibara ya 71(1)Mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafatayo
(a)" ikiwa itatokea jambo lolote ambalo kama asingekuwa mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya katiba hii."
Mpaka hapo kwa mujibu wa hicho kifungu 71(1)(a) wabunge wa viti maalumu kwa upande wa upinzani wanakosa sifa ya kuendelea na ubunge kwani kama wasingekua wabunge Leo kikokoto kingegoma hiyo idadi. Na ndivyo ibara inavyosema anapoteza sifa kama asingekuwa mbunge angekosa sifa za kuchaguliwa/kuteuliwa.
 
mkuu uelewa wangu unanituma kuwa mazingira ya kipindi kile wanachaguliwa ndio mazingira yaliyomfanya achaguliwe. Then kumbuka uchaguzi mkuu unachukuliwa kama ndio basis ya kuchagua hao wabunge na siyo uchaguzi mdogo. I stand to be corrected
 
Nashukuru sana mkuu kwa busara yako kubwa ya kuwa tayari kukosolewa.
Maelezo ya katiba yameainisha wazi kabisa sababu za kuondoka kwa mbunge kwenye nafasi yake, kwanza haijataja aina ya uchaguzi kama kigezo. Imesema uchaguzi. Kwahiyo waweza kuwa mkubwa au mdogo. Lakini pia ile ya 71 imeweka bayana endapo atakosa sifa, inamaana anaweza kuwa alikua na sifa lakini kwa sababu mbalimbali kama mwandishi alizotaja akajikuta amepoteza sifa. Ambayo ni tabia ya asili ya dunia kuwa na sifa au kupoteza sifa.
Kwa muono wangu naamin ombi la Spika kutazama hili liko sawa kwakua muda wote bungeni uwiano unatakiwa kuzingatia matakwa ya kikatiba. Ila uwiano uliopo sasa unapishana na matakwa ya katiba. Hili linaitaji maelekezo ya Spika kwakua ndiye anaetajwa na sheria kuitaarifu tume kama kuna nafasi imekua wazi
 
Back
Top Bottom