Hawa wanaovaa Vibarakoa kwenye magari private siwaelewi

Hawa wanaovaa Vibarakoa kwenye magari private siwaelewi

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
9,514
Reaction score
23,519
Naomba nitangaze nia. Mimi moja ya watu ambao niliipinga vikali corona kwa maombi. Sikuwahi kununua wala kuvaa barakoa.

Tena wakati watu walipokuwa wanakimbia DSM, Mimi nilipishana nao Singida nikienda hapo hapo DSM. Nilipita pote nilipotaka bila Barakoa. Niliwahi kunusurika kulambwa bakora Ilala boma baada ya askari kuzuia daladala na kutukagua tusio vaa barakoa.

Jambo la ajabu siku za hivi karibuni kuna jamaa naona kama hawaamini kwamba Mungu ameshakateketeza hako kadudu nchini. Kila nikitembea jijini nakagua Magari ya kifahari kwa siku naweza kuona mmoja au Wawili wamevaa.

Japo ni Uhuru wao kikatiba ila naona kama wanatutia nuksi. Wanatuarikia balaa ambalo tushaliondoa. Wakemewe aisee maana watu wakianza kuwaiga wataleta taaruki katika Jamii.

Nawasilisha.

Igweee!!!!
 
Hello everyone in Dsm

Today is the 17th of January 2021

There has been an increase in admissions into health facilities in the past week

I would like to advise you to maintain precautions as follows:

1. Avoid unnecessary gatherings
2. Wear face masks in public places
3. Adhere to hand hygeine and social distancing practises

Thank you

Please share this message and bring about awareness.

Dr. Murtaza Shk. Ayman - Saifee Hospital DSM
 
Binafsi jana nimeona watu kama familia hivi wamevaa barakoa ndani ya gari huku wamejifungia vioo full ac.
 
Hello everyone in Dsm

Today is the 17th of January 2021

There has been an increase in admissions into health facilities in the past week

I would like to advise you to maintain precautions as follows:

1. Avoid unnecessary gatherings
2. Wear face masks in public places
3. Adhere to hand hygeine and social distancing practises

Thank you

Please share this message and bring about awareness.

Dr. Murtaza Shk. Ayman - Saifee Hospital DSM
Huyu anapotosha na kutoa watu kwenye mstari. Atakuwa agent wa mabeberu huyu
 
Kama hayaja kukuta endelea Sana kumshukuru mungu lakini usiwabeze wenzako wanao vaa barakoa huu ugonjwa upo na sasa unatutesa Sana sema kila anae ugua anapambana kivyake
 
Back
Top Bottom