Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 58,047
- 134,343
Hapa duniani kila mbabe ana mbabe wake.
Nyoka koboko ‘‘kobra’’ pamoja na kuwa na sumu kali ya kunonoa mamia ya kondoo ndani ya mda mfupi lakini kiboko yake ni nguchiro au Simba kwa . Koboko akisikia mlio wa nguchiro anabaki tuliii shimoni
Dr. Magufuli ni rais aliyejitoa kufa na yupo tayari kufungwa akiwapigania watanzania wanyonge dhidi ya mafisadi majizi na wahuni wote katika serikali yake. Lakini kusema ukweli kila mbabe na mbabe wake kuna wababe ambao unapopata hamu ya kutumbua hamu lazima ikuishie. Pamoja na Rais kuwa na sumu kali ya kutumbua majibu hata kuweza kudonoa maelfu ya wenye vyeti feki ndani ya dakika, lakini naona kama anasinyaa kwa baadhi ya watu.
1. Wastaafu Benjamini Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete
Wakati Rais wa Malawi anaidhinisha kibali cha kumshitaki Rais mstaafu Joyce Banda kwa ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka, Rais Magufuli anawakingia kifua marais wastaafu wasisakamwe. Ajabu ni kwamba hakuna jukwaa alilowahi kupanda Magufuli bila kuzungumzia wizi wa awamu zilizopita. Ben Mkapa mpaka amepata kiburi cha kuwaita watanzania wapumbavu tena mbele ya mtetezi wao Rais Magufuli. Huwezi kuzungumzia ufisadi katika madini bila kuwagusa watu hawa wawili. Lakini haishangazi hawa ndio wakandarasi walioingiza serikali wa awamu ya tano madarakani
2. Beno Ndulu
Sina mengi ya kufafanua. Jinsi mafisadi wa Ecrow wanavyoshughulikiwa inashangaza sana. Ulishawahi kujiuliza Rugemalila na Singasinga nani aliwachotea fedha mafisadi hawa wa Tegeta Ecrow?Walienda wakajichotea? Yuko wapi Beno Ndulu katika sakata hili?
3. Dkt. Medard Kalemani
Kwa akili ya kawaida tu huwezi kuzungumzia ubovu wa mitakata ya madini bila kumtaja huyu. Huyu kwa sasa ni naibu waziri wa wizara ya nishati na madini na pia ni mbunge wa Chato. Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wizara ya madini toka 2013-2015 kabla ya kwenda kugombea ubunge. Na kabla zaidi alikuwa mwanasheria mwandamizi katika idara ya sharia ya wizara ya madini. Ukisema nchi imeliwa katika madini unazunguzia ubovu wa sharia na mikataba mibovu. Utaposema mikataba ya madini ni mibovu maana yake unasema Dr.Kalemani hakuwa mzalendo maana yeye ndio aliyekuwa anapitia na kushauri kuhusu mikataba kabla ya kusainiwa. Huwezi kula 10% kwenye mikataba bila mwanasheria kutia mkono.
4. Paul Makonda au Paul Bashite
Sina haja ya kumzungumzia.
5. Dotto James
Huyu ni Katibu Mkuu wizara ya fedha.
Katibu huyu ameshindwa kumshauri waziri wa fedha na rais mwenyewe juu ya matumizi yanayokosa nidhamu ya bajeti. Imeandikwa sana katika serikali ya awamu ya tano kumekuwa na matumizi makubwa ya fedha bila kuidhinishwa na bunge. Mifano ambayo imekuwa ikitajwa ni pamoja na ununuzi wa ndege, serikali kuhamia Dodoma nk. Lakini pia hali ya uchumi na mzunguko wa fedha umekuwa ukihatarisha jitihada ya kuelekea uchumi wa kati.
HITIMISHO
Vita dhidi ya ufisadi inapimwa kwa vitendo sio maneno. Na vita hii wana haihitaji kusema sana kwenye media. Haina haja ya kupiga mayowe...............Acha watu wayaone wenyewe
Ni maoni yangu.