The Giant
JF-Expert Member
- Jun 24, 2012
- 504
- 96
Ni Bavarians au Mnyama Mweusi(The Black Beast). Mabingwa mara 22 wa Bundesliga, Mabingwa mara 15 wa Kombe la Shirikisho(DFB-Pokal), Mabingwa mara 4 wa Ngao ya Hisani(DFB-Supercup). Mabingwa mara 4 wa klabu Bingwa ya Ulaya, Mabingwa mara 4 wa Ligi ya Europa(UEFA Europa League) na Mabingwa mara 2 wa Klabu Bingwa ya Dunia.Ni kinara wa kukaza mwanzo hadi mwisho wa mechi. Mpaka sasa wanaongoza kwa pointi 69 kwenye msimamo wa bundesliga, akifuatiwa na Borussia Dortmund(BVB).Mbali na BVB, Leverkusen na Schalke04 pia zina upinzani mkubwa kwa klabu hyo. Manchester United, Real Madrid na AC Milan wamekeza mabilioni kuwapiku wajeruman hao, ila bado hawajafika kile kiwango kinachohitajika. Falsafa ya tikitaka ya Pep Guardiola itasaidia kuinyanyua Bayern kwa kiwango kikubwa, Barcelona wakae kando, sasa ni Bayern kutawala Ulaya na Dunia kwa ujumla. Longlive to you Glorious Bayern, We are with you all the way!