barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,874
Kumekuwa na upotoshaji mkubwa ambao umeanza kuenezwa na baadhi ya watu kuwa Joshua Nassari,Mbunge wa Arumeru Mashariki ni mmoja wa vijana wa Kitanzania waliokuwepo ukumbini wakati Rosemary Odinga akidanganya dunia kuwa Olduvai Gorge ipo Tanzania.
Ukweli ni kuwa kwenye mkutano huo Joshua Nassari hakuwepo,mkutano huu ulikuwa 2015 August,wakati Joshua akiwa "busy" na kampeni.Na ukweli mwingine ni kuwa Joshua alihudhuria mwaka mwingine uliotangulia ambapo toka Tanzania Joshua aliambatana na Mbunge wa Shinyanga Mjini kupitia CCM Mheshimiwa Steven Massele na baadhi ya vijana wengine
Mkutano wa mwaka jana ambao Rosemary alitumia mkutano huo kuidanganya dunia,vijana waliohudhuria ni hiyo picha nyingine,ambapo yupo "bwana mdogo" wa kipindi cha ".....Agenda" cha TBC,hawa ndio walihudhulia mkutano huo kwa mwaka wa jana na si Joshua kama wengine wanavyotaka kumchafua.Hapa wa kuulizwa ni TTB na Wizara ya Utalii,wao toka mwaka wa jana 2015 August walikuwa wapi mpaka mitandao kama @JamiiForum imekuja kufukua upotoshaji huu??
Wakati Rose Odinga akimwaga uwongo huo,Watanzania vijana wetu walikuwa huko nje bustanini "wakirukaruka" na kupiga "selfie" za facebook na Instagram ili waje watuwekee huku mitandaoni.Sasa wenye "chuki" wanaanza kumvaa Joshua Nassari,basi wajue mkutano aliohudhuria Joshua Nassari ndio mkutano aliokuwepo Steven Massele mbunge wa CCM wa Shinyanga Mjini.