Hawa ndio Manabii na Mitume matapeli, tumechoka kuwavumilia sasa

Yaani ww ndo unayajua maandiko na kuomba kuliko wengine huko ,mpk ufunuluwe!?

Trust mi Mungu huwa hafunui mambo yake hovyohovyo,kuna watu maalum waliotengwa wenye hekima zao ndo huwafunulia ciz they knw how to hundle kwa kufuata mapenzi yake Mungu!

Mnachokifanya nyie, mnachukua baadhi ya vipande vya masomo ili kuhalalisha mnachokiongea!
Mbona hamtuwekei wanayoyafundisha hapa na waiowajua wayasikie!?,coz tunayafuatilia ht u tube huko tunaona!

Biblia tunaisoma ,tunaomba na Mungu anatusaidia sn tu!
Usitudanganye mkuu
Sijakuona humu siku nyingi Christine. Umesema kweli coz Mungu hawezi kumfunulia mtu ili awatukane kwa kiwango hiki. What people cannot understand they criticize,the call names, they give slanderous remarks!!
 
Amani na iwe kwenu.

Hakuna mtu awezaye kumtumikia Mungu pasipo kusimama kinyume na nguvu za giza. Kama ilivyokuwa kwa vizazi vilivyopita, shetani anaendelea kutenda kazi kupitia makanisa. Shetani anaonekana kuwa ndiye mfadhili wa makanisa mengi kwa sasa wakati huo akitumia kila hila kuwazuia watu wasipate maarifa ya Biblia, ambayo yana maonyo juu ya udanganyifu wake.

Kwa sasa Limeibuka wimbi kubwa sana la mitume na Manabii, ndani na nje ya nchi yetu. Sipingi uwepo wa manabii na mitume, maana hizi ni karama za roho mtakatifu. Efeso: 4:11:14; "naye alitoa wengine kuwa mitume na wengine kuwa manabii, na wengine kuwa wanjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu"

Maana kazi ya karama ni kulijenga kanisa la bwana. Efeso 2:19-20 " Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, mmjengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni" .

Shabaha ya ujumbe huu si kumuhukumu yeyote wala kumchafua mtumishi yeyote wa Mungu au kuhuchafua ukristo bali ni kuwafichua hawa wanaojiita manabii na mitume uchwara wa sasa wanaotumia miamvuli ya dini kutapeli watu, kudhulumu watu, kutenganisha ndoa za watu, kubaka na kunajisi watoto. Wanatumia njia za mkato kuutafuta utajiri na umaharufu kwa kufungua makanisa kama maduka ya biashara, na kutumia kila njia kuvuta waumini ili kuwalaghai na kuwaibia. Hawana tofauti na wezi, majambazi, wauaji, wapiga ramli. Kutwa wanashinda kwa waganga wa kienyeji hata kutoa watoto wao, ndugu zao au waumini wao kafara " Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa kristo. Wala si ajabu maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru" (2 Wakoritho 11: 13 - 15).

Hawa mitume na manabii wamejaa ndani ya makanisa wanatumia Jina la Yesu huku wametumwa na shetani kuwadanganya wateule ili wapotee na kujitenga mbali na Mungu. "Watu hawa huniheshimu kwa midomo, ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisha yaliyo maagizo ya wanadamu...waacheni, hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake watatumbukia shimoni wote wawili" (Mathayo 15:8-14.)

Hatuwezi kuendelea kuona watu wakitapeliwa, wakidhumiwa, watoto wakibakwa, wakifarakanisha ndoa za watu. Hatuwezi kusubiri Mh Magufuli aje alikemee hili, japo Nchi yetu haina dini ila watu wake wana dini na watu ni sisi sasa iweje tuendeleea kuona ushenzi unafanyika, utapeli wawazi alafu tuendelee kunyamaza kimya?

Nimeshudia matukio mengi ya hawa watu wanaojiita mitume na manabii. Mama mmoja mjane kauza nyumba yake baada ya nabii mmoja kumwambia Mungu amempa maono ili apone kabisa maradhi yake aliyonayo anatakiwa amtolee Mungu sadaka kwa kila mwaka wake mmoja atoe elfu 50. Bibi ana miaka 58, sasa zidisha kwa kila mwaka mmoja atoe 50 Mara miaka 58 utapata bei gani. Je utapeli kama huu tuendelee kuuvumilia tu? Na sasa wametajirika kwa biashara ya mafuta, chumvi, vitambaa, maji ya upako. n.k wananunua watu kutoa shuhuda za uongo kuvuta watu. Mabinti wetu wanabakwa na wao, wanachukua hovyo wake za watu, wengine wanageuza waumini kuwa misukule hata akisema nini waumini wanafuta tu kama hamnazo vile.

Nitawataja hawa manabii na mitume wa uongo. Yesu alisema kwa matendo yao tutawajua. " Jihadharini na Manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa- mwitu wakali . Mtawatambua kwa matendo yao." (Mathayo 7 :15-16 )

1: BG: Malisa wa kanisa la Ukombozi ministries for all nations.
2: Nabii na Mtume Peter Nyaga wa kanisa la Miracle center,
3: Nabii Frank Kilawah, wa kanisa la Shiloh Ministries.
4: Nabii George David Kasambale.(Geordivie) wa kanisa la Geordivie Ministries au Ngurumo ya Upako.
5: Nabii na Mtume Boniface Mwamposa (Buldozer ) wa kanisa la Inuka uangaze.
6: Nabii Frora Peter wa kanisa la Yesu kristo, huduma ya maombezi na uponyaji. Mbezi.

Hawa ni wachache nitaendelea kuwafunua kwa kadri Mungu atakavyonipa mafunuo juu ya watumishi hawa. Sitaogopa kuwataja kwa majina yao. Katika kila kizazi Mungu ametuma watumishi wake kukemea dhambi duniani na kanisani pia.
BM pesambili, ungetwambia na wewe ufunuo wako umeupata wapi, kutoka kwenye chuki na wivu au kutoka kwenye "Upendo". Napata mashaka na ufunuo wako kama unatoka katika upendo au kwa jina ulilozoea MUNGU . Labda kama ulifunuliwa vyote alafu umeamua kutufunilia robo. Umekuwa specific kwa kuwataja watumishi hawa majina kitu ambacho kila mmoja anaweza kufanya kutokana na hisia zake ambazo umeziita ufunuo. Nikupongeze tu kwa kutaja baadhi ya maovu ambayo mtu yeyote akiyaona kwa anayejiita Mtumishi wa Mungu basi anaweza kutambua ni mtumishi feki. Lakini tukija kwenye hitaji la watu wanaowasikiliza hawa watumishi na kuamin kinachohubiliwa, ni kwamba watu hawa wanakiu, wanatafuta faraja, amani, na tumaini kutoka kwa kristu, na hayo yote yanapatikana kwa kusikiliza neno na kulitenda. Inakuwa ngumu kuwabadilisha au kuwatoa kwa mtumishi ambae anawafafanulia neno vizuri na wao kazi yao ni kiskiliza tu. Kwa maana wameagizwa wasikilize kile watumishi wanachowambia si kufuata matendo yao kwa maana wale ni binadamu na shetani anayo mamlaka ya kuwapepeta na wao kama mkulima apepetavyo ngano. Ndio maana ukiwaandikia watu hiki ulichoandika wanasoma lakini kwenye makanisa namikutano ya hao watumishi unakuta watu wamejaa wakisikiliza neno la Mungu. Mungu anaweza kutumia mtu yeyote kufikisha ujumbe wake kwa maana vigezo anavyotumia si kama vya mwanadamu.
 
Chukua like mkuu naongezea nyama tuu kwenye uzi wako tangu Mungu ameumba kuanzia kwa Adam pale edeni Mpaka Yesu kuja ni vizazi vitatu kila kizazi kina nabii wake na kiongozi wa kizazi,Musa alikua nabii kizazi cha 1,Eliya mtishibi alikua nabii kizazi cha 2,Yesu alikua nabii kizazi cha 3,hao ndio waliopewa agizo na Mungu kwa ajili ya kanisa,ikumbukwe kanisa sio dini au dhehebu flani wala kanisa halitoki italy au uingereza au amerca au popote pale duniani Bali kanisa linafunuliwa na Mungu mwenyewe mathayo16:16-19,bila shaka mmewahi kusikia kwenye History before christ na after Christ,after Christ ni nabii wa kizazi cha 4 ambaye tayari ameshakuja na alichotumwa kakamilisha na ameshaondoka,kifupi hao wote huko mjini ni matapeli sawa na waganga wa kienyeji tuu
 
Mhh huyo ni shida..mzee wa upako me simuaminigi...kuna siku nilikuwa naangalia ibada yake akawa anawaambia waumini anatoa sabuni za utajiri eti lakini ukiogea useme kwa jina la mungu anayemuabudu mzee wa upako sabuni hii inipe utajiri sasa mtu mwenye akili lazima ujiongeze kuwa kuna mungu wangapi mpaka useme anayemuabudu yeye...wezi tu hawa
 
Amani na iwe kwenu.

Hakuna mtu awezaye kumtumikia Mungu pasipo kusimama kinyume na nguvu za giza. Kama ilivyokuwa kwa vizazi vilivyopita, shetani anaendelea kutenda kazi kupitia makanisa. Shetani anaonekana kuwa ndiye mfadhili wa makanisa mengi kwa sasa wakati huo akitumia kila hila kuwazuia watu wasipate maarifa ya Biblia, ambayo yana maonyo juu ya udanganyifu wake.

Kwa sasa Limeibuka wimbi kubwa sana la mitume na Manabii, ndani na nje ya nchi yetu. Sipingi uwepo wa manabii na mitume, maana hizi ni karama za roho mtakatifu. Efeso: 4:11:14; "naye alitoa wengine kuwa mitume na wengine kuwa manabii, na wengine kuwa wanjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu"

Maana kazi ya karama ni kulijenga kanisa la bwana. Efeso 2:19-20 " Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, mmjengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni" .

Shabaha ya ujumbe huu si kumuhukumu yeyote wala kumchafua mtumishi yeyote wa Mungu au kuhuchafua ukristo bali ni kuwafichua hawa wanaojiita manabii na mitume uchwara wa sasa wanaotumia miamvuli ya dini kutapeli watu, kudhulumu watu, kutenganisha ndoa za watu, kubaka na kunajisi watoto. Wanatumia njia za mkato kuutafuta utajiri na umaharufu kwa kufungua makanisa kama maduka ya biashara, na kutumia kila njia kuvuta waumini ili kuwalaghai na kuwaibia. Hawana tofauti na wezi, majambazi, wauaji, wapiga ramli. Kutwa wanashinda kwa waganga wa kienyeji hata kutoa watoto wao, ndugu zao au waumini wao kafara " Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa kristo. Wala si ajabu maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru" (2 Wakoritho 11: 13 - 15).

Hawa mitume na manabii wamejaa ndani ya makanisa wanatumia Jina la Yesu huku wametumwa na shetani kuwadanganya wateule ili wapotee na kujitenga mbali na Mungu. "Watu hawa huniheshimu kwa midomo, ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisha yaliyo maagizo ya wanadamu...waacheni, hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake watatumbukia shimoni wote wawili" (Mathayo 15:8-14.)

Hatuwezi kuendelea kuona watu wakitapeliwa, wakidhumiwa, watoto wakibakwa, wakifarakanisha ndoa za watu. Hatuwezi kusubiri Mh Magufuli aje alikemee hili, japo Nchi yetu haina dini ila watu wake wana dini na watu ni sisi sasa iweje tuendeleea kuona ushenzi unafanyika, utapeli wawazi alafu tuendelee kunyamaza kimya?

Nimeshudia matukio mengi ya hawa watu wanaojiita mitume na manabii. Mama mmoja mjane kauza nyumba yake baada ya nabii mmoja kumwambia Mungu amempa maono ili apone kabisa maradhi yake aliyonayo anatakiwa amtolee Mungu sadaka kwa kila mwaka wake mmoja atoe elfu 50. Bibi ana miaka 58, sasa zidisha kwa kila mwaka mmoja atoe 50 Mara miaka 58 utapata bei gani. Je utapeli kama huu tuendelee kuuvumilia tu? Na sasa wametajirika kwa biashara ya mafuta, chumvi, vitambaa, maji ya upako. n.k wananunua watu kutoa shuhuda za uongo kuvuta watu. Mabinti wetu wanabakwa na wao, wanachukua hovyo wake za watu, wengine wanageuza waumini kuwa misukule hata akisema nini waumini wanafuta tu kama hamnazo vile.

Nitawataja hawa manabii na mitume wa uongo. Yesu alisema kwa matendo yao tutawajua. " Jihadharini na Manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa- mwitu wakali . Mtawatambua kwa matendo yao." (Mathayo 7 :15-16 )

1: BG: Malisa wa kanisa la Ukombozi ministries for all nations.
2: Nabii na Mtume Peter Nyaga wa kanisa la Miracle center,
3: Nabii Frank Kilawah, wa kanisa la Shiloh Ministries.
4: Nabii George David Kasambale.(Geordivie) wa kanisa la Geordivie Ministries au Ngurumo ya Upako.
5: Nabii na Mtume Boniface Mwamposa (Buldozer ) wa kanisa la Inuka uangaze.
6: Nabii Frora Peter wa kanisa la Yesu kristo, huduma ya maombezi na uponyaji. Mbezi.

Hawa ni wachache nitaendelea kuwafunua kwa kadri Mungu atakavyonipa mafunuo juu ya watumishi hawa. Sitaogopa kuwataja kwa majina yao. Katika kila kizazi Mungu ametuma watumishi wake kukemea dhambi duniani na kanisani pia.
Mkuu sema watu wajitoa ufahamu unaweza kujua bila kuambiwa kwamba huyu nabii ni mwongo TUBADILIKE kila ninapotazama mahubiri ya hawa wanao jiita manabii sijui mitume kuna vioja vingi sana
 
Nabii Flora Peter wa mbezi beach!
1443196803586-jpg.291131
Shindwa kwa jina la yesu kristo flora mbona yuko kama wale wanaogiza wachawi kwenye Nigerian movies
 
Nilisikia mmoja kati ya hao manabii wa uongo akialika watu kwenda kwa mikutano yake akisema "eti watakaohudhuria mafundisho yake watapokea roho mtakatifu" matapeli wakubwa sana hao
 
Koran imeandikwa na khalifa Uthman.
Japo waliopaswa kuiandikwa ni waandishi wanne walioaminiwa sana na mohammad. Waandishi hawa Ibay ka'ab na wenzake hawakufikia consesus kuhusu koran original ilivyopaswa kua.

Bibilia ni mkusanyiko wa vitabu vilivyoandikwa na mitume, manabii wa Mungu.
Haya sasa!
 
Acheni kazi ya kuhukumu ibaki kwa Mungu tu unathubutuje kuita mtumishi wa Mungu tapeli ? Ulishawai hata kufika kanisani kwake ukamsikiliza ?
 
Back
Top Bottom