MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Kuna watu wanajitahidi kupindisha ukweli lakini tatizo ni kuwa ukweli huwa haupindi.
Suala la uchaguzi Zanzibar halijawahi kuwa ni tatizo katika serikali ya Marekani hasa ikichukulia hata waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar walikuwa Wamarekani kama inavyobainishwa katika nakala za nyaraka zilizo katika Maktaba ya Lyndon Baines Johnson huko Texas, Marekani ambazo zinahusu mawasiliano baina ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani, mawaziri wa wizara hiyo, mabalozi na majasusi wa Kimarekani waliokuwako Afrika Mashariki. Wamarekani waliasisi muungano ili utumike kama buffer zone.
Kwa macho ya Marekani, CUF ya Zanzibar ni kama kikundi cha Hamas ambacho kimeachwa kwa makusudi na Israel ambaye ni mshirika wa Marekani katika eneo la Gaza Strip ili kisaidie katika utawala kwa kutumia mlengo wa divide and rule. Mapambano kati ya Fatah na Hamas ni silaha ya Israel akisaidiwa na Marekani katika kutawala kwa mabavu. Marekani/Western World hawezi kuiacha CUF ya Zanzibar ikue na kuimarika mpaka iwe unmanageable threat bali inaiacha iwe kama instrument ya check and balance kama ilivyo Hamas katika kusimamia maslahi ya Marekani/Western World nchini Tanzania. Hata CUF 'wanashangaa' wanapoona eti Marekani anawatetea.
Marekani anafahamu vizuri siasa za Zanzibar ambazo mzizi wake siyo political ideology bali ni ubaguzi. Marekani anafahamu vizuri ubaguzi ambao umeota mizizi haumalizwi kwa kutumia sanduku la kura bali unatumika vizuri katika kuendeleza inhuman agenda.
Hoja za uchaguzi wa Zanzibar kwa sasa zinatumiwa na Marekani baada ya kugundua Maslahi yake nchini Tanzania yameanza kuguswa/kutingishwa. Hoja ya uchaguzi Zanzibar ni kichaka tu kwa kuficha ukweli.
Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 1995, Marekani walidhani mlengo wa kisiasa na kiuchumi wa Rais Mkapa ni kama wa Mwl. Nyerere hasa walipomuona Nyerere akipanda jukwaani kufanya kampeni, na kutokana na mawazo hayo walianza kutumia fimbo ya Uchaguzi wa Zanzibar na kukata misaada ili kumtingisha, lakini baada ya kugundua Rais Mkapa ni kibaraka wa maslahi yao, hata vikwazo vya kiuchumi walivyoviweka wakaviondoa (vikafa naturally).
Kwa sasa Wamarekani/Western World hawaja uelewa vizuri msimamo halisi wa Rais Magufuli katika kusimamia maslahi yao Tanzania, EAC and SADC. Watu kama Lazaro Nyalandu ambao walikuwa vibaraka wa maslahi ya Marekani/Western World kwa sasa wako nje ya meza ya maamuzi ya serikali (Baraza la Mawaziri) huku kundi la Nyalandu kutoka Marekani likigonga mwamba kukutana na Rais Magufuli kama ilivyoripotiwa hapa;
Wamarekani hawafurahi anaposimama Rais Magufuli na kusema hataki kumsikia Waziri au Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini akimshauri kuongeza mikataba wa kukodisha makampuni yanayozalisha umeme wakati chimbuko/mzizi wa Symbion power ni MCC huku mengine yakiwa katika harakati za kuingia katika mikataba mipya ya nishati.
Wamarekani hawafurahi anaposimama Rais Magufuli na kudai Tanzania ni tajiri na hapendi vimisaada misaada vya masharti wakati masharti ndio fimbo ya Marekani katika kuzitawala nchi zenye wananchi masikini lakini tajiri wa Maliasili.
Wamarekani hawafurahi kuona Rais Magufuli hana muda wa kulamba viatu vyao pamoja na wao kutumia njia mbali mbali kutaka kuonana naye wakati wanaamini bila wao hawezi kufanikiwa katika adhima yake kisiasa na kiuchumi.
Wamarekani hawapendi kiongozi wa nchi za Afrika mwenye haiba ya masikini jeuri.
Mbaya zaidi, Personally, Rais Magufuli na Balozi wa Marekani hawaivi chungu kimoja kwa sababu mmoja ni masikini jeuri na mwingine ni tajiri jeuri. Ieleweke Balozi wa Marekani nchini ndio msingi wa mahusiano kati ya Tanzania na Marekani. Maoni yake (recommendations) mara nyingi hukubalika katika serikali ya Marekani.
Pesonally, Balozi wa Marekani anaiva chungu kimoja na Edward Lowassa kwa sababu wote ni tajiri jeuri na urafiki wao unachagizwa zaidi na maslahi binafsi.
CHADEMA walipotoa tamko siku moja kabla ya kikao cha Bodi ya MCC kuhusu hatima ya Tanzania kupata msaada kutoka MCC haikuwa nikwa bahati mbaya bali ilipangwa!
Lowassa aliposema, “Rest assured that I’m going to be very active. I might have lost a battle, but not a war,” alikuwa na maana ya vita kama hii.
Kwa sasa maadui wakuu wa Rais Magufuli katika adhima yake ya kuibadili Tanzania ni hawa;
Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress akiongea kwa kusisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Edward Lowassa walipokutana kwenye hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akionyesha ufunguo wa Helkopta mara baada ya kukabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu & Rubani Mkuu wa Kampuni ya Helcopter Charter (EA), Peter Achammer kwa niaba ya Mfuko wa Howard G. Buffet ambapo ni moja ya utekelezaji wa ahadi za mmiliki wa Mfuko huo alizozitoka kwa Rais Jakaya Kikwete alipofanya ziara katika Mbuga za wanyama hapa nchini hivi karibuni. Wa pili kulia ni Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress naWaziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa .

Wataalam wa mambo ya siasa za kimataifa wanatuambia, ukiona kiongozi wa kisiasa katika nchi za Afrika anasifiwa sana na wanasiasa wa Marekani/Western World lazima uanze kujiuliza maswali magumu kama wewe ni African Nationalist. Hii ni red flag.
Wamarekani hawafurahi anaposimama Rais Magufuli na kusema hataki kumsikia Waziri au Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini akimshauri kuongeza mikataba wa kukodisha makampuni yanayozalisha umeme wakati chimbuko/mzizi wa Symbion power ni MCC huku mengine yakiwa katika harakati za kuingia katika mikataba mipya ya nishati.
Wamarekani hawafurahi anaposimama Rais Magufuli na kudai Tanzania ni tajiri na hapendi vimisaada misaada vya masharti wakati masharti ndio fimbo ya Marekani katika kuzitawala nchi zenye wananchi masikini lakini tajiri wa Maliasili.
Wamarekani hawafurahi kuona Rais Magufuli hana muda wa kulamba viatu vyao pamoja na wao kutumia njia mbali mbali kutaka kuonana naye wakati wanaamini bila wao hawezi kufanikiwa katika adhima yake kisiasa na kiuchumi.
Wamarekani hawapendi kiongozi wa nchi za Afrika mwenye haiba ya masikini jeuri.
Mbaya zaidi, Personally, Rais Magufuli na Balozi wa Marekani hawaivi chungu kimoja kwa sababu mmoja ni masikini jeuri na mwingine ni tajiri jeuri. Ieleweke Balozi wa Marekani nchini ndio msingi wa mahusiano kati ya Tanzania na Marekani. Maoni yake (recommendations) mara nyingi hukubalika katika serikali ya Marekani.
Pesonally, Balozi wa Marekani anaiva chungu kimoja na Edward Lowassa kwa sababu wote ni tajiri jeuri na urafiki wao unachagizwa zaidi na maslahi binafsi.
CHADEMA walipotoa tamko siku moja kabla ya kikao cha Bodi ya MCC kuhusu hatima ya Tanzania kupata msaada kutoka MCC haikuwa nikwa bahati mbaya bali ilipangwa!
Lowassa aliposema, “Rest assured that I’m going to be very active. I might have lost a battle, but not a war,” alikuwa na maana ya vita kama hii.
Kwa sasa maadui wakuu wa Rais Magufuli katika adhima yake ya kuibadili Tanzania ni hawa;
Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress akiongea kwa kusisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Edward Lowassa walipokutana kwenye hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akionyesha ufunguo wa Helkopta mara baada ya kukabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu & Rubani Mkuu wa Kampuni ya Helcopter Charter (EA), Peter Achammer kwa niaba ya Mfuko wa Howard G. Buffet ambapo ni moja ya utekelezaji wa ahadi za mmiliki wa Mfuko huo alizozitoka kwa Rais Jakaya Kikwete alipofanya ziara katika Mbuga za wanyama hapa nchini hivi karibuni. Wa pili kulia ni Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress naWaziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa .
President Kikwete akiwa na wageni wa Mbunge Lazaro Nyalandu ambao ni U.S. Congressional. Front Row (L-R): U.S. Ambassador Mark Green, Mr. Mike McIntyre, Senator Inhofe, Senator Enzi na Mr. Boozman.
Mbunge Nyalandu aliwapeleka Ikulu kuonana na Rais, Mwingine katika picha ni Samuel Sitta.
Hawa wageni wa Mbunge Nyalandu wamekuwa wakifika Tanzania kila mara kwa kazi ambazo haziko katika ratiba rasmi ya serikali.
Mwaka huu Rais Magufuli amekataa kuonana nao kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari.