Hawa ndio aina ya Makandarasi wetu

Jamani mi natengeneza vitambulisho vya bima ya afya (NHIF) kwa kutumia check number za wabunge wa bunge maalum la katiba.kama uko tayari tuwasiliane
 
nakuunga mkono % 10000 kweli ukandarasi ni biznea na hautaji cv.....tushawaona wajanja wengi wakipewa deal za ujenzi lakini hawana sifa hata kidogo ya ujenzi.....
 

................... RUSHWA wakati wa kuteuwa wakandarasi...fully stop.
 

Hamna cha uchanga wa wahandisi, ni mfumo wa uongozi mbovu, hakuna usimamizi na ufuatiliaji wa sheria, na uhakika tanesco eneo husika wanataarifa za uwepo wa nguzo sehemu inapotakiwa kupita barabara lakini wakajifanya kichwa ngumu.
Unakumbuka magufuli alipopiga kelele kuhusu watu waliojenga road reserve ? Kikwete ndo alisema hatua yeyote isichukuliwe kwa watu waliopo road reserve, na katika ujenzi wa barabara ya magari yaendayo kasi, jengo la tanesco lilitakiwa liondoke lakini hawajaondoka matokeo yake wamejenga barabara nyembamba.
 
T A N E S C O
CLIENT: Tanesco Mbeya
CONTRACTOR: Mwananzengoo
CONSULTANT: Tanesco regional eng
PROJECT: Soil Stabilization along AK transmission line
CONTRACT NO.: TNSCO/MBY/2014/04

Kumbe siyo barabara hahahahaaaaaa!
 
Pamoja na maelezo yako lakini bado kuna mushkeli...Huoni ni hatari sana sana sana tena sana kwa hali ya namna hiyo? Busara zaidi ilibidi kutumika!

Ndugu naomba unijibu maswali yafuatayo:

Who prepares the following:

1. Engineer's cost estimates?
2. Bidding documents?
3. Tender documents?
4. Contract?

Who awards the contract?

Je umesoma contract ya huo mradi?

Busara ambayo ingetumika ni hii:

Kama kwenye contract hakukuwa na pay item for relocation of services (Section 1200 of Standard Specifications), Client (mwenye mradi) angeandaa addendum to include such missing pay item ili contractor afanye. Inavyoonekana Client hakufanya hivyo. Kwa hiyo hakuna kosa kwa upande wa mkandarasi. Mkandarasi hawezi kufanya kazi ambayo haiko kwenye mkataba!
 
Mimi ni kati ya Watanzania waliokuwa wakitetea sana Wahandisi wazawa kupewa kazi mbalimbali nchini lakini baada ya kuona picha hizi nimesikitika sana!

mbona kama hii picha ime editiwa?
 

Kaka umeongea fact maana watu wanakurupuka tu kuanza kulaumu. Hapo mzembe ni mwenye barabara hyo sijui halmashauri au tanroads
 


Mkandarasi wa barabara ataweza kuhamisha nguzo ikiwa kama amepewa fungu lakuhamisha na kama kampuni yake inashughulika pia na masuala ya umeme na pia tu kwa kushirikiana na tanesko.

Lakini muhusika wa power lines ni tanesko peke yao, haruhusiwi mtu yeyote kugusa.

Ningekuwa mimi ndio mkandarasi na nguzo haijahamishwa ningejenga barabara huko kote ila ningeacha bila kuijenga umbali wa mita 12 tokea kwenye nguzo kuelekea pande zote mbili, hadi nguzo itakapoondolewa ndio nitaunganisha.
 
Aisee,kama vile kivutio cha utalii.
Kituko kweli,inanikumbushe kule Spain kama sikosei,kuna Mzee mmoja aligoma nyumba yake kubomolewa,basi alikaa katikati peke yake,Nyumba ikawa kituko na kivutio fulani.
Mwisho wa siku alibembelezwa na wakuu ndio akatoka.
 


Kweli kila jambo lina faida na hasara. tumeliangalia hili kwa upande wa hasara tumeacha kwa upande wa faida zake.kama vile kuwa kivutio cha utalii maana sidhani kama kuna nchi nyingine ina kituko kama hiki.
 

mkuu utaumiza kichwa chako! wengine kuelewa ni mpaka uchukue nyundo ugonge gonge vichwa vyao! ndiyo maana nchi haziendelei kwa sababu hawa-deal na chanzo wana-deal na matokeo! jiji lina mkurugenzi, lina meneja wa tanesco, wahandisi wa jiji, madiwani, kamati ya mipango miji lakini watu hawahoji wanafanya kazi juu ya suala hilo lakini wachangiaji humu wamekomaa na mkandarasi tu! shame on them!

hizo data ulizompa sijui kama huyo macho_mdiliko & co watakuelewa!!
 
Last edited by a moderator:

Ndugu, nadhani huelewi inclusion of addendum in engineering construction contracts.
Ni hivi: ikiwa kwenye mradi (in this case, road contract) kuna kazi ambayo kwenye mkataba was overlooked (au haimo kwenye mkataba which means mkandarasi hawezi kuifanya) na kwamba ni lazima ifanyike, Client (mwenye mradi) anaandaa addendum ili kuingiza hiyo kazi kwenye mkataba ili ifanywe na mkandarasi. Bila hivyo mkandarasi hawezi kufanya hiyo kazi maana akiifanya hatalipwa kwa kuwa haimo kwenye mkataba. Nadhani umeelewa!
Ni kweli wanaohamisha hiyo nguzo ni TANESCO lakini kimkataba anayejulikana ni mkandarasi, hivyo tunasema mkandarasi ame-hire services from TANESCO to relocate the power line.
 
Labda nikueleweshe kidogo...ni kwamba tanesco wamechelewa kung'oa nguzo yao na mradi unatakiwa ukamilike kwa wakati ili apsiwe na kelele za rushwa wala ufisadi...jawabu ndio hilo barabara inatengenezwa na Tanesco watakapoondoa nguzo yao kipande kilichobaki kinamaliziwa....Nawapongeza sana makandarasi hawa kwani walizingatia muda na gharama ambazo zingepanda iwapo wangewaendekeza Tanesco.
Mimi ni kati ya Watanzania waliokuwa wakitetea sana Wahandisi wazawa kupewa kazi mbalimbali nchini lakini baada ya kuona picha hizi nimesikitika sana!
 

Tatizo lao wanavamia fani za watu! Hawawezi elewa.
 

Maswali hayako hayana maana yoyote kwani sijasema mkandarasi ndio angehamisha hiyo nguzo... nimesema angetumia busara... eg kutojenga hiyo sehemu. Hii ni valid reason kuliko kuweka nguzo yenye umeme wa msongo mkubwa ndani ya barabara. Maafa yake ni makubwa! Binadamu hatufanyi kazi kama marobot!
 
Tatizo lao wanavamia fani za watu! Hawawezi elewa.

Mkuu watanzania wengi hawajitambui kwa mambo! nina shemeji yangu mmoja ni diwani na pia ni kiongozi wa chama tawala na ni mtetezi mzuri wa sera za chama chake na ana kaelimu kake ka form six na chuo! siku moja mkewe ambaye ni dada yangu akaugua na akalazimika kulazwa kwenye wodi ya hospitali moja wilaya na hapo ndipo kasheshe ilipoanzia! vitanda vilikosekana na ikabidi alazwe chini tena wakichangia godoro na mwanamke mwenzake! mh.diwani akaanza kumgombeza nurse na daktari wa zamu kuwa kwanini mkewe alazwe chini!

Ilibidi niingilie kati lakini baada ya kumcheka sana na kumwambia akumbuke wakati alipokuwa, yeye na chama chake, akiwatapeli wananchiwapiga kura kuwa wawachague yeye na chama chake ili WAWALETEE MAISHA BORA! nikamwambia kuwa kama alikuwa hajui sera nzuri za chama kilichoko madarakani ni kuwapelekea wananchi wao SOCIAL SERVICES na siyo kuwaimbia taarabu kila siku! !
 
wewe una matatizo makubwa kichwani mwako na nahisi una uhusiano mkubwa katibu mkuu wa ccm, abdi kinana! anaenda kulamikia watumishi wa serikali mitaani wakati chama chake ndiyo kinaongoza nchi!
 

Ohoo dear! Hapo kuna data au maswali! Haya tulazimishe na kukubali amenipa ''data'' kama unavyoziona wewe! Swali: Pamoja na kwamba halikuwa jukumu la mkandarasi kuhamisha nguzo (kitu amabacho wala sijapinga) je huoni kuwa kama ikotokea basi yenye abiria 60 ikagonga hiyo nguzo yanaweza kutokea maafa makubwa? Kwanini huyo mkandarasi haku-skip hicho kisehemu ili kuepusha ajali kama hizi? Yes... angeweza ku-skip na ukawa utetezi wenye kila chembe za busara kuliko kufanya mahoka aliyoyafanya.
 
wewe una matatizo makubwa kichwani mwako na nahisi una uhusiano mkubwa katibu mkuu wa ccm, abdi kinana! anaenda kulamikia watumishi wa serikali mitaani wakati chama chake ndiyo kinaongoza nchi!

Ahaa haa.. Macho_Mdiliko is whistling!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…