Hawa mabinti wanaozaa hovyo hovyo nje ya ndoa wadhibitiwe mara moja

Mwanapropaganda

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
4,235
2,508
Sasa hivi suala la mabinti wengi kuzaa limekuwa kama mtindo wa kisasa(fashion).

Katika mambo yanayochangia umaskini na kuzorota kwa maadili kwenye jamii ni hili la watoto wengi kutopata malezi stahiki kutoka kwa wazazi wao.

Nimeona kwa sasa mabinti wadogo wanazaa tu bila utaratibu wala mipango kwa maslahi ya maendeleo ya mtoto siku za mbeleni. Vijana wanaowapa mimba hizo hutokomea na kuacha jukumu lao kuwa kama mzigo wa wenhgine, hivyo watu wengine wanajikuta wakilazimika kuwatunza watoto hao pasipo kitegemea.

Leo ukipita kwenye mitaa na kuona watoto wanaoishi mazingira magumu, wengi wao wametokana na hili ninalosema hapa.

Wito wangu kwa serikali ni kupiga marufuku watu kuzaa kabla ya ndoa na vile vile kuhakikisha hakuna atakayezaa nje ya ndoa ili kuwafanya watoto wapate malezi stahiki, hatua hiyo itapunguza vijana wa mitaani ambao wengi wao huishia kujiingiza kwenye magenge ya uharifu na matumizi ya dawa za kulevya.

Migogoro kwenye ndoa inayosabanishwa na tuhuma za kuzaa nje ya ndoa zinasababisha watoto kukataliwa na hatimaye kuathiriks kisaikolojia.


Serikali itamke wazi kwamba, kuzaa nje/kabla ya ndoa ni jinai, vile vile kuhakikisha watoto wote wanapata huduma za lazima kutoka kwa wazazi wao.
 
Mleta uzi nawe ni jipu kwakweli. Hao watoto ni wa wanawake tu hawana mababa? Mbona usiseme wanaume zao nao waache kuwapa mimba wasichana bila ndoa?
 
Hili ni tatizo kubwa sana katika jamii zetu. Wasababishaji wanakimbia majukumu yao. Dada zangu kuweni makini sana. Sisi wanaume hebu tuangalie actions zetu na madhara yake.

Tafakari chukua hatua
 
wanaume muwe mavaa condom kwa sababu nyie ndiyo waanzilishi wa mchezo na hao wanafunzi wengi mnawabaka tu na kuwalaghai so muhimu ni side zote mbili hakuna mimba inayotokea bila kuwa na mbegu za kiume acha kutupa lawama upande mmoja wote wanaounganisha vikojoleo kama hawapo tayari kuwa na mtoto ni vyema mkatumia condom au mkakojoa nje au muuche ngono
 
Hivi umejiandaaje na makombora maana asilimia kubwa katika JF aidha tumezaliwa kabla ya ndoa au tuna watoto tuliotunga mimba zao kwa raha zetu nje ya ndoa. Ngoja nisubiri CC lara 1, Heaven Gemmy


Sio kila aliye single mother amependa kuwa hivyo kuna mazingira yamewapush mpaka kuitwa single mother, Kuna waliowapenda wanaume na malengo yakawatofauti mwingine anawaza ndoa ili hali mwingine anawaza kuwa mzazi mwenza maisha hayana usawa kuna watu walikataliwa kwasababu ya jinsia , kuna watu walikataliwa kwa sababu baba kapata mwanamke ambaye kwa wakati huo anamuona bora zaid ya aliyemzalisha . Yote katika yote maisha hayana usawa sio kila unalolitaka linaweza timia kama ulivyolipanga
 
Hili ni tatizo kubwa sana katika jamii zetu. Wasababishaji wanakimbia majukumu yao. Dada zangu kuweni makini sana. Sisi wanaume hebu tuangalie actions zetu na madhara yake.

Tafakari chukua hatua
dini inasema zinaa mbaya na hatuelewi kabisa
 
Back
Top Bottom