Hawa airtel tatizo la laini kugoma kusajili alama za vidole limekaaje?

Statesmann

JF-Expert Member
Jul 16, 2019
2,344
3,460
Nipo sehemu Nida wameleta namba pamoja na mawakala mitandao ili mtu aliichukua no. amaenda kusajili fingerprints.

Tatizo lililojitokeza ni mtandao wa airtel namba zao nyingi zinagoma kusoma kwenye system yao kwamba hazipo.
Akiingiza no. ya simu kwenye mfumo inaandika "No file found" kwamba haipo kabisa.

Mimi laini yangu imegoma kwamba eti haitambuliki nikajua tatzo ni langu pekee kumbe raia kibao pale laini zinagoma kusoma kwamba hazitambuliki na Airtel.

Nimewauliza vijana wanaosajili wanadai kwamba laini za zamani eti hazisomi na hazipo kwenye system/database za Airtel hivyo inabidi usajili laini mpya au uswap laini.

Kinachonishangaza mimi inakuaje laini naitumia tangu 2012 halaf haimo kwenye database za airtel?

Au ni mbinu ya madogo kuuza laini za Airtel?

Mbona laini za voda, tigo zinakubali tu tena nimezitumia zamani kuliko hata hii ya airtel?

Airtel hebu acheni uhuni laini yenu niitumie halafu isiwemo kwenye system yenu?
 
Airtel wana matatizo sijui kwa nini, nilisajili line kwa fingerprint then nikamwambia nataka ni upgrade kwenda 4G matokeo yake 3G ikakata na 4G haikuwahi kutokea data ikazima jumla nilisumbuka nao nikaona wazinguaji. So hao usiwashangae hawako serious na kazi yao
 
Mzee baba wewe fundi ujenzi virile vyako vimeliwa na cement hivyo jipe likozo wiki vistari vya vidole virudi then rudi kasajili itakubali tu
 
Tanzania tunamtandao mmoja tu wa kishua Vodacom.
Tatizo ni gharama.
 
Mzee baba wewe fundi ujenzi virile vyako vimeliwa na cement hivyo jipe likozo wiki vistari vya vidole virudi then rudi kasajili itakubali tu
kaka hapa umeandika kilugha au? Unatupa shida sisi wasoma comments.
 
Back
Top Bottom