Si unajua tena HR wanavyokalia viti vya kuswing maofisini anapoongea nawe kwa uhakika huku akikukazia macho kwa ukali? Yawezekana ukawa umesahau hata madai yaliyokupeleka hapo, ukaanza kutengeneza mazingira ya kutofukuzwa kazi. Kuna watu wakikalia ofisi zao wanadhani hawataondoka humo milele, wala hawataki walioko chini yao wajue haki zao. Inapogundulika kwamba haki zimejulikana wanatafuta utata wa kutumia kuwadhibiti wasidaidai haki. Meneja mzuri ni yule anayetetea maslahi ya kampuni zaidi na wala sio kutetea maslahi ya wafanyakazi. Ndio asili ya kuzaliwa umoja wa wafanyakazi.